Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Ushirikina ni kitendo cha kuikataa sayansi na kufuata njia zisizothibitidhwa kama ile ya maombi na ile ya kujifukiza moshi ili kujaribu kuua virus ndani ya mwili wa binadamu.

Wakati mgonjwa anahitaji oxygen kwa wingi wewe unampa Caron dioxide kwa wingi.
 

Hospitali ya taifa ya Muhimbili na Mloganzila leo hii imezindua rasmi mashine maalum ya itakayotoa huduma ya kujifukiza kwa kutumia mitishamba kwa ajili ya kujikinga na kutibu changamoto za upumuaji/kujifukiza (kupiga nyungu).

IMG_20210304_182234.jpg


Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Lawrence Maseru ameeleza kuwa, mgonjwa atatumia dakika tano akivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili,
kwa kutumia mashine zilizotengenezwa na Shirika la Viwanda vidogo SIDO kwa Gharama ya kujifukiza ni Sh 5,000 kwa nusu saa.

"Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa. Matumizi ya miti shamba yaonekana kuwa na faida," amesema Prof Maseru.

Mashine tatu zaidi zinatarajiwa kufungwa katika hospitali hiyo na nyengine ikitarajiwa kufungwa katika tawi lake la Mloganzila lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
 
Ushirikina ni kitendo cha kuikataa sayansi na kufuata njia zisizothibitidhwa kama ile ya maombi na ile ya kujifukiza moshi ili kujaribu kuua virus ndani ya mwili wa binadamu.

Wakati mgonjwa anahitaji oxygen kwa wingi wewe unampa Caron dioxide kwa wingi.
Ha ha ha
 
Soon tutaona video za wakuu kunadi tiba hii.Upo msemo " Vita ni vita Muraa" hivyo tusipuuze silaha iliyo karibu.
 
nyungu unatakiwa upige umevua ngua zote ikiwezekana baki na kabati tu ili dawa iingie mwilini vizuri sasa unaingia humo uku umevaa nguo ni kujifurahisha
 
Haya ndiyo maswali ya kuuliza. Asante. Utapata majibu.
====

Soma post namba 226 ya uzi huu utapata majibu.

Kwani dawa ya kujifukizia ambayo india wameifanyia majaribio na ikaonyesha mafanikio ndiyo dawa tunayoitumia sisi kujifukizia?India wamefanyia majaribio dawa zao za kujifukizia na zimeonyesha mafanikio,mimi nimeuliza juu ya dawa yetu ya kujifukizia wala sijauliza juu ya dawa za nchi nyingine!Hii dawa yetu ya kujifukizia imejaribiwa wapi na lini ikaonyesha mafanikio?Na hayo mafanikio yalikuwa ni asilimia ngapi?
 
Kumbe issue yaa kujifukiza ni serious?hongera kwa muhimbili kutekeleza mawazo ya mheshimiwa.
Dah kwa hiyo saivi OPD ukionekana tu hueleweki Dkt anaandkaa prescription ya "kujifukiza 30mins bd× 3/7"
 
Haya ndiyo maswali ya kuuliza. Asante. Utapata majibu.
====

Soma post namba 226 ya uzi huu utapata majibu.

Asante sana kwa kutuletea jaribio/utafiti waliofanya India.

Natamani kama Tanzania tungeonyesha kisayansi kama wenzetu walivyofanya. Tungeweza hata kuchangia utatuzi wa hili janga.

Nilichogundua kwa majaribio waliyofanya India:
  • Wametumia mvuke ila hawajesema kama waliongeza chochote kwenye mvuke
  • Waliokuwa steji mbaya ya ugonjwa hawakujumuishwa kwenye hili jaribio
  • Wamesema bado kunahitaji utafiti zaidi na kwa upana zaidi.

Kungekuwa na hatua za kisayansi katika kuthibitisha uwezo na ufanisi wa nyungu, tungepunguza kelele za mashaka.
 
Back
Top Bottom