Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Tshs 5,000/-tu
Hospital ya taifa
Hivi lengo ni kutokomeza ugonjwa nchini au ndio tena ishakua fursa?
Mngeweka bei ya Tshs 200 au 500 kungekuwa na hasara gani?
Ukitaka kutawala kwa raha, piga mkwala kwanza kila mtu anyweee!!ndio uanze kufanya kila ulitakalo!!hakuna wa kusema, kipimo cha covid19, kilikuwa 40, 000 sasa ni 230, 000, nchi, nyingi ni bure, kwa raia wake!!wamepiga mkwala mask za nje, kumbe wanakuja na zao toka mcd!!leo nimesikia tena wanakuja na sanitizer!!!ni biashara tu, huko tena wizara ya afya kuna acc imefunguliwa yankuchangia mfuko wa covid19!!!nani wa kuhoji hayo?!!!
 
Naona unawapigia debe ma- white wizard wenzio, Waafrika huwataki!???
 
Hivi kweli madakatari wetu wanapendekaza kujifukiza kutibu kovidi? Ewe mwenyezi Mungu wanusuru Watanzania.Ijumaa hii nasujudu ,ewe Mwenyezi Mungu wanusuru Watanzania. 6
Tatizo hujui kovidi kuwa ni mafua tu makali. Kujifukiza kunaboost natural immunity mwilini ambayo matokeo yake ni kupambana kifanisi dhidi ya virusi. Chanjo inaingiza foreign antigens mwilini ambazo zinakuwa kama sampuli za SARS-COVID Virus wa corona, matokeo yake kinga ya mwili inakuwa aktiveted kupambana na REAL Corona virus.
 
Kwa hiyo mtu wa kipato cha chini atoke kwake, apande usafiri, afike MNH na atoe TZS 5000 ili apige nyungu kisha arudi kwake tena!
Hiyo imewekwa kwa madhumuni ya watu wanaoenda Muhimbili kumbuka Muhimbili watu wengi wanaenda hapo wa kipato tofautitofauti.
 
Hiyo imewekwa kwa madhumuni ya watu wanaoenda Muhimbili kumbuka Muhimbili watu wengi wanaenda hapo wa kipato tofautitofauti.
Sasa boss si ulisema imelenga watu wa kipato cha chini? Imekuaje tena unaongelea watu wa kipato tofauti tofauti?
Pili, ulimjibu mtu aliyesema kuna haja gani ya kuwepo hiyo wakati mtu anaweza kufanya hivyo nyumbani kwake? Wewe ndiyo ukasema ya MNH imelenga wananchi wa kipato cha chini!
Lipi unalolisimamia sasa?
 
Acha ubwege wewe baradhuli. Kuna tofauti kubwa kati ya inflammatory na infectious ( inflammation na infection) Tofauti kama iliyopo kati ya mass na weight!
 
Acha ubwege wewe baradhuli. Kuna tofauti kubwa kati ya inflammatory na infectious ( inflammation na infection) Tofauti kama iliyopo kati ya mass na weight!
Hujui chochote! Umekariri
 
"Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa. Matumizi ya miti shamba yaonekana kuwa na faida," amesema Prof Maseru.
Inanitia uchungu na hasira. Profesa kuna nini kinaendelea? Nadhani unajua kuna magonjwa bila dawa yanapona kwa siku saba na kwa dawa yanapona kwa wiki. Maana yake dawa haijasaidia chochote.
Pia unajua kuwa ukiona ugonjwa mara fulani katumia dawa hii amepona. Wa pili naye ugonjwa huohuo kapona kwa dawa tofauti. Wa tatu, wa nne na kuendelea, kila mmoja anapona kwa dawa tofauti. Huo ugonjwa haujapata dawa.
Wote ni mashuhuda wa jambo fulani la ajabu la magonjwa. Unasikia mgonjwa aliyepima na kukutwa na malaria anapona kwa panadol tu. Na mwingine anatumia dawa zinazofahamika kutibu malaria haponi mpaka labda drip ya quinine!
Magonjwa yasababishwayo na virus ndio ajabu kabisa. Mtu ni hiv+(true+) kwa miaka 20 sasa hajaumwa. Kuna wengine walikuwa hiv+ (confirmed) baada ya muda wakawa hiv-. Kuna tofauti kati ya kuwa mgonjwa na kuumwa. Wagonjwa ni wengi. Wanaoumwa ni wachache!
Yote haya yana maelezo yake kitabibu. Profesa unajua. Si ajabu hiyo mitishamba kuonyesha faida( neno lako) tena zama za covid-19 kutokuwa na tiba. Si ajabu hata kidogo. Ni ajabu daktari (licha ya kwamba wewe ni orthopedic surgeon) tena wa cheo chako kutamka vitu ulivyosema na kufanya. Inatisha!
 
Kama hutaki nenda USA kama unajari sana vya wazungu. Sisi tumepona kwa dawa zetu za miti shamba.
 
Waseme tu kuwa wamebuni chanzo cha kukusanya kodi, hivi kweli mtu ambaye anategemea akauze nyanga, au atembee nguo atajifukiza atatoa 5,000 badala ya kuwanunulia watoto wake chakula
 
Hujui chochote! Umekariri
I'm in a dilemma. Don't argue with a fool, people might not notice the difference. Ninaye baradhuli mmoja mbele yangu. Anahubiri ujinga. Kwa wengi ni sumu. Ni mwache asambaze sumu? Hapana. Nataka kumshughulikia bila ya samahani. Atoe tofauti kati ya inflammatory na infectious. Kama hawezi akae tu asome wanaojua wanaandika nini. Akiendelea kuandika apuuzwe apuuzwavyo mpuuzi. Na ajue kuwa katika kujifunza kukariri hakukwepeki!
 
Kama hutaki nenda USA kama unajari sana vya wazungu. Sisi tumepona kwa dawa zetu za miti shamba.
You fool don't fool around me. What I've written is not for fools like you. Kuna dawa kwa ajili yako nimetoa tayari. Tulia. Kujua kusoma na kuandika tu kama wabunge wa Tz haitoshi.
 
Wewe zoba kabisa. Kujua kusoma na kuandika haitoshi. Ungejua kwa nini wagonjwa wanawekewa oxygen ungenyamaza. Covid-19 inaingia lower respiratory tract bila hodi. Hiyo rejea yako inasema steaming haiui virus hata huko kwenye upper respiratory tract. Sijui huyu mdudu MATAGA atabakiza mtu. Huyu ni hatari kuliko corona virus!
 
Si tumekubaliana lugha ni Kiswahili sasa swanglish ya nn
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…