Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

"Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa. Matumizi ya miti shamba yaonekana kuwa na faida," amesema Prof Maseru.
 
Yaani kuvuta hayo mamivuke buku 5, kwamba kila mtu hawezi kutengeneza nyumbani kwake.....hivi mnauelewa kwamba mazingira ya humo ndani na idadi ya watu watakaoingia itachochea zaidi maambukizi ya korona na magonjwa mengine kama TB, hivi nchi hii wote wamegeuka waganga wa kienyeji?
Hii nchi ina ombwe la uongozi
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.

Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru.

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.


Mwananchi
hao wagonjwa wanapimwa na kuambiwa wana maambukizi kabla ya kuingia humo?
usafi ukoje? maana hakuna sehemu inayobeba magonjwa ya bakteria na virus kemkem kama steam bathing za public zisipofanyiwa Usafi takanishi.
Bubiji (Uponyaji)
maji ya mvuke kwa mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika...?! hata mpita njia.
aisee tunacheza na teknolojia na ugonjwa wa virus huu
 
Ulitegmea zifanyiwe utafiti kwa nyani? Zipo zinafanyiwa utafiti kwa binadamu na majibu yake yatachapichwa "The Lancet"


Kufanyiwa utafiti kama inafanya kazi vyema kabla ya kuwekwa kwenye "real practice", hivi sasa imewekwa kwenye "real practice" kwa maana kwamba watu wanakuwa na matumaini ya kupona wakati kitu chenyewe ni bado it is on trial.
 
Wazungu wakiona ndo watasema wao ndo wajinga maana hawakujua iyo nyungu na sauna hazina tofauti hii lazma wajione wajinga ni swala la language barrier sasa wao waki implement na kuboresha kuweza kufanya icho chetu basi watakua wamefanya la maana ila mchina alishashituka maana pia kwenye Mila zao huwa wanapga nyungu
Sauna za wazungu ni sawa sawa na nyungu ? Maana wao walisema hazifai katika kipindi hiki cha kovidi, labda wataalamu watakuwa wameweka vya ziada ili kuzifanya salama na tofauti na hizo za wazungu
 
"....unampa Caron dioxide kwa wingi." Hapo mkuu sijuhi ulikuwa una maana gani.....jinga sana wewe!
We ndiyo fala, huo mvuke unaotoka una kiasi gani cha Oxygen? mnauwa watu kwa makusudi nyie. Afu unakuta prof mzima wa udaktari wa binadamu anashadadia hii mivuke eti inatibu Virus.
 
Wakati Dunia ikihaha kutafuta Chanjo ya COVID-19, Tembelea Tanzania uone ma-Professa wa udaktari wa binadamu wanavyoshiriki kujenga mitambo ya kutibu Corona kwa njia ya mvuke.

Safi sana, Covid haina chama!! "Jenga nyungu - piga nyungu" usione aibu- Nyungu si ushirikina bali ni sayansi ya asili.
 
Msiojua hii ni sauna ipo toka zamani, hakuna hoteli kubwa isiyokuwa nayo, kazi yake kutoa sumu mwilini nk, inasaidia sana hata magonjwa nyemelezi ngumu kupata anayefanya sauna
Ni kwasababu inafanywa namtanzania ndyo maana watu wanaidharau. Watanzania tuna hulka mbaya sana. Ingekuwa mzungu kafungua SAUNA watu wangekimbizana kwenda lakini kwasababu ni mtanzania ndyo katengeneza tunaona ni utopolo mtupu[emoji119]
 
Hivi kweli madakatari wetu wanapendekaza kujifukiza kutibu kovidi? Ewe mwenyezi Mungu wanusuru Watanzania.Ijumaa hii nasujudu ,ewe Mwenyezi Mungu wanusuru Watanzania. 6
 
View attachment 1717355
Tatizo nadhani siyo kupinga sayansi bali kwa mbaaaali tunakale kaugonjwa kuwa lazima aanze kwanza mzungu ndio inakuwa sayansi ya ukweli.
Ngozi nyeupe wametumia sana mivuke ya Eucalyptus na sisi tunaita Bupigi.
Wataalamu wetu wafanye clinical trials.
Unaengelea miaka gan hyo mkuu?! Ujue zama zmebadilika hata dhaman watu walikua wana jistili tuu sehemu za siri then wana ingia mtaani fanya hvo sahv uone kama hautaonekana kichaa the inshu zama zilipita na hyo practice ilionekama siyo poa sasa sis tunataka kurud hukooo😂😂😂
 
Kumbuka kuna watu hawana uwezo kama wewe. Hivyo hiyo ni kwa ajili ya watu wakipato cha chini.
Kwa hiyo mtu wa kipato cha chini atoke kwake, apande usafiri, afike MNH na atoe TZS 5000 ili apige nyungu kisha arudi kwake tena!
 
Tshs 5,000/-tu
Hospital ya taifa
Hivi lengo ni kutokomeza ugonjwa nchini au ndio tena ishakua fursa?
Mngeweka bei ya Tshs 200 au 500 kungekuwa na hasara gani?
 
We ndiyo fala, huo mvuke unaotoka una kiasi gani cha Oxygen? mnauwa watu kwa makusudi nyie. Afu unakuta prof mzima wa udaktari wa binadamu anashadadia hii mivuke eti inatibu Virus.
Wamekufa watu wangapi hadi leo kwa kupewa hicho unchoita Oxygen?....Aliyekwambia inatibu virus ni nani mkuu? Tumia muda wako wa ziada kujikumbushia uliyosoma shule ya msingi....inalipa sana!
Wazungu wenyewe wanajifukiza hata kabla ya corona kuja....tuliopata bahati ya kusoma tiba zao ona wanavyofanya:

Steam Inhalation: What Are the Benefits?​

What are the benefits of steam inhalation?​

A stuffy nose is triggered by inflammation in the blood vessels of the sinuses. The blood vessels can become irritated because of an acute upper respiratory infection, such as a cold or a sinus infection.
The main benefit of breathing in moist, warm steam is that may help ease feelings of irritation and swollen blood vessels in the nasal passages. The moisture may also help thin the mucus in your sinuses, which allows them to empty more easily. This can allow your breathing to return to normal, at least for a short period of time.
Steam inhalation may provide some temporary relief from the symptoms of:
While steam inhalation can provide subjective relief from the symptoms of a cold and other upper respiratory infections, it won’t actually make your infection go away any faster.
Steam inhalation doesn’t actually kill the virus responsible for the infection. At best, steam inhalation might make you feel a little better as your body fights your cold.
One review of six clinical trials evaluating steam therapy in adults with the common cold had mixed results. Some participants had symptom relief, but others didn’t. Additionally, some participants experienced discomfort inside the nose from the steam inhalation.
Another recent clinical trial looked at the use of steam inhalation in treating chronic sinus symptoms. The study, however, didn’t find that steam inhalation was beneficial for the majority of sinus symptoms, except for headache.
Although the results of clinical studies have been mixed, anecdotal evidence claims steam inhalation helps alleviate:
  • headache
  • congested (stuffy) nose
  • throat irritation
  • breathing problems caused by airway congestion
  • dry or irritated nasal passages
  • cough

Sisi tunaongeza an dawa zetu kama bupeji....nk
 
Hivi kwa nini tusipende vya kwetu? Shida ni nini iwapo na sisi watalam wetu wameona njia bora mojawapo kua ni hiyo? Kwani na sisi hadi tuige kwa kwingine? Naunga mkono msimamo wa Nchi yangu
Mkuu suala la afya sio eti kuleta uzalendo sio mpira huo!!yaani watu wanaumiza vichwa na pesa nyingi sana, kufanya tafiti za kina kugundua chanjo tena za virus, wewe unaamka asubuhi na kuja na MATOGWA, MIBANDA MIKUBWA, eti kujifukiza, mala kirusi kwenye joto la centigrade kadhaa kina pasuka kweli??!!"by mtaalam wa kemia"kwanza jiulize kwani hii covid 19, ndio ugonjwa wa kwanza, mbona hamjawahi gundua dawa yoyote ile, na ikaumika duniani kote?!!yaani sasa hivi ndio unawaona waganga wa kienyeji wanavyofumuka utafikiria ndio kwanza wamezaliwa hawakuwepo!!tuache siasa hiyo chanjo haikwepeki ni suala la muda tu, na baadaye atakapo kubali mtaanza tena kumsifia kuwa ni mzalendo!!hata hamueeweki
 
Back
Top Bottom