Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Muhimbili na Mloganzila zafunga mashine za kujifukiza. Kupata huduma hiyo ni Tsh. 5,000 tu

Sayansi inasimama yenyewe haihitaji validation kutoka kwa mzungu. Kuleta hoja za "mbona wao wana sauna" na picha kama hizi kutafuta validation ndio inferiority yenyewe, na inaonesha kutokuwa na uelewa wa sayansi...
Naamini ulisoma sentensi yangu ya mwisho. Suala la validation ya inferiority litabaki kuwa ni mtazamo ambao ni uhuru wako. Nilichokuwa nakilenga ni kuepeku mawazo kuwa kila matibabu yetu ya asili ni ushirikina ila hicho hicho kikifanywa na white skin ndio sayansi. Narudia madaktari wetu wa tiba asili nao wafanye clinical trials zenye sample size na data za kutosha.
 
  • Thanks
Reactions: len
Wakisema steaming utakubali lakini wakisema nyungu unadharau. Waafrika tuna shida kwenye ubongo wetu hasa mnaojifanya mmesoma kumbe mmekariri hamkuelimika kabisa. Unajua kuwa virus wa corona ni inflammatory? Na kwamba virus wanauwawa na joto sasa steaming au nyungu ndiyo njia mwafaka ya kuwazuia.wasiendelee kuongezeka puani na njia za hewa mdomoni? Elimikeni kwanza then mpinge kwa akili basi nyinyi utopolo.
We jamaa unavyoongea kama unajua vile. Hivi unaelewa hata pathophysiology ya corona virus disease? Na thermoregulation of the body?vipi structure ya virus? Unaifahamu respiratory system vizuri?na hiyo "inflammatory" unaijua kweli?
Unavyoongea kama kweli vile kumbe utumbo tu.
 
View attachment 1717207
View attachment 1717208
View attachment 1717209
View attachment 1717216View attachment 1717215
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili hii leo imezindua rasmi mashine maalumu ambayo itatumika kutoa huduma za kujifukiza katika hospitali hiyo kuu ya rufaa nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Muhimbili Prof Lawrence Maseru ameeleza kuwa, mgonjwa atatumia dakika tano akivuta mvuke wenye mchanganyiko wa dawa asili.

Hata hivyo, wataalamu wengi wa afya pamoja na shirika la Afya Duniani (WHO) hawakubali matumizi ya mvuke kama tiba ya corona wakionya mvuke unaweza kusababisha madhara makubwa kwenye mfumo wa upuamaji ikiwemo kujaza mapafu maji.

Kuhusu katazo hilo la WHO, Prof Maseru amesema miti shamba imeonesha kuwa na tija.

"Hadi sasa hakuna Tiba ya covid hivyo kila dawa inapaswa kujaribiwa. Matumizi ya miti shamba yaonekana kuwa na faida," amesema Prof Maseru.

Uongozi wa Muhimbili pia umeeleza kuwa kwa sasa idadi ya wagonjwa wenye 'matatizo ya upumuaji' wamepungua hospitalini hapo.

Mashine tatu zaidi zinatarajiwa kufungwa katika hospitali hiyo na nyengine ikitarajiwa kufungwa katika tawi lake la Mloganzila lililopo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.

Mwaka uliopiita rais Magufuli alinukuliwa akisema kwamba wagonja wa virusi vya corona katika hospitali mbali mbali walikuwa wamepungua licha ya serikjali kutotoa takwimu rasmi za viwnago vya maambukizi.

Kiongozi huyo mara kwa mara amesisitiza kwamba watu hawafai kuwa na hofu kuhusu ugonjwa huo.

Serikali ilisitisha utangazaji wa takwimu za ugonjwa huo mara kwa mara mwezi Aprili baada ya rais kulalamika kwamba desturi ya kutangaza idadi ya wagonjwa ilikuwa inaongeza hofu.

Aidha serikali ya Tanzania ilisema ina wasiwasi kwamba kuwafungia watu kwa lengo la kuzuia maambukizi kunaweza kuwa na athari kubwa kwa maisha ya watu na uchumi, na pia hatua kama hiyo inaweza kuathiri sekta muhimu ya utalii.
Dkt Magufuli pia alitilia shaka usahihi wa matokeo ya vipimo vya corona vilivyokuwa vikifanywa na maabara ya taifa, baada ya sampuli za paipai na mbuzi kuonyesha zilikuwa na virusi.
 
Wanasayansi wetu wanaokula minoti ya kodi, na kujimwambafy kwamba wao ni wasomi wanafanya nini? yaani waganga wa jadi ndio wametake place sasa?maana wameshanakiliwa na wanaojiita wasomi na watafiti, wao kama wao wamekwama kabisa,
Ama kweli corona imekuja kuumbua watu
 
Naamini ulisoma sentensi yangu ya mwisho. Suala la validation ya inferiority litabaki kuwa ni mtazamo ambao ni uhuru wako. Nilichokuwa nakilenga ni kuepeku mawazo kuwa kila matibabu yetu ya asili ni ushirikina ila hicho hicho kikifanywa na white skin ndio sayansi. Narudia madaktari wetu wa tiba asili nao wafanye clinical trials zenye sample size na data za kutosha.
Kwa nini unaingiza rangi ya ngozi kwenye hili? Hiyo picha ya eucalyptus umeiweka hapa Kwa nia gani? Muhimbili na Mloganzila wametangaza clinical trial au wameanza kutoa huduma Kwa sh 5000 Kwa wagonjwa?
 
Hapo ndio unaposhindwa kuelewa kabisa. Sijaingiza mimi, ni majibu ya implications za huko juu. Chukua muda usome taratibu maana maswali yako sijui unayaibulia wapi!
 
Kumbe ni mashine ambazo bado hazijafanyiwa utafiti?

Very ridiculous.
Ulitegmea zifanyiwe utafiti kwa nyani? Zipo zinafanyiwa utafiti kwa binadamu na majibu yake yatachapichwa "The Lancet"
 
Ushirikina ni kitendo cha kuikataa sayansi na kufuata njia zisizothibitidhwa kama ile ya maombi na ile ya kujifukiza moshi ili kujaribu kuua virus ndani ya mwili wa binadamu.

Wakati mgonjwa anahitaji oxygen kwa wingi wewe unampa Caron dioxide kwa wingi.
"....unampa Caron dioxide kwa wingi." Hapo mkuu sijuhi ulikuwa una maana gani.....jinga sana wewe!
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.

Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru.

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.

Mwananchi
Profesa Lawrence Museru ameamua kuwa sawa na Profesa Vulata au Maji Marefu. Yale mambo yote aliyosoma kwenye PhD mpaka akawa Profesa wa MUHAS ameyazika rasmi. Haya mwambieni Museru arudishe vyeti vya Digrii zake kwenye vyuo alivyosoma
 
Yaani kuvuta hayo mamivuke buku 5, kwamba kila mtu hawezi kutengeneza nyumbani kwake.....hivi mnauelewa kwamba mazingira ya humo ndani na idadi ya watu watakaoingia itachochea zaidi maambukizi ya korona na magonjwa mengine kama TB, hivi nchi hii wote wamegeuka waganga wa kienyeji?
Dakika 5+ nyingi mno.aisee
 
Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na Mloganzila zimefunga mashine nne za kujifukiza.

Wakati Muhimbili zikifungwa mashine tatu, Mloganzila imefungwa moja. Gharama ya kila mashine ni Sh7.5 milioni na kila moja ina uwezo wa kuhudumia watu sita kwa wakati mmoja wanaopaswa kukaa kati ya dakika tano hadi 10.

Ili mtu aweze kujifukiza katika mashine hizo anapaswa kulipia Sh5,000 na yeyote anaruhusiwa hata wapita njia.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashine hizo zilizopewa jina la Bupiji Sauna leo Alhamisi Machi 4, 2021 mkurugenzi mtendaji wa MNH, Profesa Lawrence Museru amesema kuanzishwa kwa mashine hizo kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya kujifukiza kwa watu wote wanaohitaji.

“Kujifukiza huku kunaenda sambamba na matumizi ya dawa za asili ambazo zimekuwa zikitumiwa na zimeonyesha kusaidia, mashine hii inatumia dawa ya Bupiji inayowekwa katika maji ya mvuke na mgonjwa au mtu anayetaka anaingia ndani atakaa dakika tano hadi 10,” Profesa Museru.

Profesa Museru amesema uwepo wa mashine hizo kutawawezesha madaktari kujua kama njia hiyo inasaidia kwa kiwango gani vita dhidi ya corona.

Mwananchi
Habari bila picha ni kama habari mfu
 
Back
Top Bottom