Huyo mwanamke anatumia plan B ya kukutega na atakupata tu,amekuchunia na umeumia mpaka kuanzisha uzi hapa,
Baada ya muda ataanza kukuchangamkia tena na wewe hapo utaona usifanye kosa kama la mwanzo,kifupi usipokua makini atakupata kirahisi sana,kwanza amesha anza kuziteka hisia zako kwa kuacha kukuchangamkia japo hapa unajifanya eti huna hisia nae,
Ungekua huna hisia nae usingeanzisha huu uzi,hisia sio lazima ziwe za kimapenzi tu bali umehisi kua kuna kitu kimepungua kwenye mizunguka yako kwa kutokuchangamkiwa na huyo Dada.