Muhudumu wa Restaurant hanichangamkii tena siku hizi!

Muhudumu wa Restaurant hanichangamkii tena siku hizi!

Inawezekana. Ngoja nione mwisho wake.

Unajua kwenye vita ya kuchuniana kati ya mwanamke na mwanaume, mbeleni mwanamke huwa anasalimu amri na kuomba suluhu. Wenzetu wana mioyo miepesi.

Sasa wewe na huyo ‘dada’ nani ana moyo mwepesi?[emoji23]
Kunywa maji mkuu, uendelee na mapambano mengine.
 
Wadau naomba mnisaidie kudadavua hili jambo ninaliliona.

Kuna mgahawa kuanzia kama miaka miwili nyuma hadi hivi leo huwa ninakwenda kila siku kupata chakula cha mchana au mara nyingine kuchukua takeaway.

Kuna DADA ni mmoja wa wahudumu kwenye huo mgahawa ambao ni mkubwa tu katika huu mji ninaokaa. Huyu dada siku za nyuma alikuwa akiniona nimefika, ananichangamkia na kunitania tania mbele ya baadhi ya wafanyakazi wenzake wa kike utani wa kama vile mimi ni "jamaa yake" ila mimi sikuwa na hisia nae zozote wala kumwambia lolote kutokana na utani utani wake, kwasababu nikawa nachukulia anachoifanya ni utani tu na wala sio serious anachofanya!

Sasa siku za karibuni naona huyu dada kabadilika, hataki ukaribu na mimi wala kuongea na mimi tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma.
Mfano, kuna mara mbili nimefika akaja mezani kunisikiliza alafu, oda ya chakula nikaletewa na muhudumu mwenzake, kitu ambacho kikanionesha ni dhahiri kuna kitu kinachoendelea ndani ya nafsi yake huyu dada.

Naomba kujua ndugu zangu, huyu dada anaweza kuwa amebadilika kwasababu gani?

Nauliza tu, ingawa mimi hili jambo haliniumizi kichwa kwasababu hata sina hisia nae zozote. Na hata kama huyu dada ana hisia na mimi, kwenye huo mgahawa sina mazoea wala ukaribu na muhudumu mwingine yeyote wa kike kusema labda amenihisi nina uhusiano nae kisha yeye ndio akaona wivu au kuwa na kama chuki.

Ahsanteni.
Una miaka mingapi mkuu?
 
Mbona jibu unalo boss, alikutaka ila hukumpa ushirikiano, maana yake ukaona sio type yako
Sasa unaona amekuchukia kwa sababu umemdharau kama hana
Bora ujipikie tu maana hapo utakula visivyoliwa ndio maana anampa mwingine akuletee

Yaani kumuudhi mhudumu mimi siwezi aisee nawaogopa sana anaweza akakupa uchafu ulala tu kwenye mboga ya samaki
kula mzigo au hama chaguo lako moja hapo
 
Shida huja mtongoza wala kumla, wanawake ndivyo walivyo, akikuonyesha upendo mpende pia, we piga tuu alafu tambaa ni boora kuliko kumchunia maana mwisho wa siku yeye ndiyo ata anza kukuchukia sasa.
 
Mkuu mwanamke akikuonyesha anakupenda nextime usimuignore...ishawahi kunikuta nikiwa chuo nikikumbuka huwa inaniuma sana aisee she was very cute ila ni ule uoga kwamba sina pesa sitaweza kumuhandle ndo kilichoniponza,ila huwa nataman siku zirudi nyuma kwakwel! Alionyesha wazi kuwa ananipenda ila wapi sikujiongeza kilichofata sasa akaanza kunichukia waziwazi[emoji23]
Watu kama nyie ndo mnafanya jua liwake sana dar hii,sasa mtoto anajiangusha ndani ya 18,unapaisha tuta?
 
Inawezekana. Ngoja nione mwisho wake.

Unajua kwenye vita ya kuchuniana kati ya mwanamke na mwanaume, mbeleni mwanamke huwa anasalimu amri na kuomba suluhu. Wenzetu wana mioyo miepesi.
Ivi ww n mgen wa mapenz,Wanawake au nn yaan?.Jidanganye Sasa,mwanamke akikuchukia anakuchukia mazimaaa yaan ukiona karudi kwako jua kunakitu anakitafuta hana pa kukipata.
 
Dada wakati huo alikua single anakutaka wew ukamkunjia,amepata beana ake na anajuana na wafanyakazi wenzake hapo kanin kwake sasa akikushubokea si ni noma mzee.
 
Wadau naomba mnisaidie kudadavua hili jambo ninaliliona.

Kuna mgahawa kuanzia kama miaka miwili nyuma hadi hivi leo huwa ninakwenda kila siku kupata chakula cha mchana au mara nyingine kuchukua takeaway.

Kuna DADA ni mmoja wa wahudumu kwenye huo mgahawa ambao ni mkubwa tu katika huu mji ninaokaa. Huyu dada siku za nyuma alikuwa akiniona nimefika, ananichangamkia na kunitania tania mbele ya baadhi ya wafanyakazi wenzake wa kike utani wa kama vile mimi ni "jamaa yake" ila mimi sikuwa na hisia nae zozote wala kumwambia lolote kutokana na utani utani wake, kwasababu nikawa nachukulia anachoifanya ni utani tu na wala sio serious anachofanya!

Sasa siku za karibuni naona huyu dada kabadilika, hataki ukaribu na mimi wala kuongea na mimi tofauti na ilivyokuwa hapo nyuma.
Mfano, kuna mara mbili nimefika akaja mezani kunisikiliza halafu, oda ya chakula nikaletewa na muhudumu mwenzake, kitu ambacho kikanionesha ni dhahiri kuna kitu kinachoendelea ndani ya nafsi yake huyu dada.

Naomba kujua ndugu zangu, huyu dada anaweza kuwa amebadilika kwasababu gani?

Nauliza tu, ingawa mimi hili jambo haliniumizi kichwa kwasababu hata sina hisia nae zozote. Na hata kama huyu dada ana hisia na mimi, kwenye huo mgahawa sina mazoea wala ukaribu na muhudumu mwingine yeyote wa kike kusema labda amenihisi nina uhusiano nae kisha yeye ndio akaona wivu au kuwa na kama chuki.

Ahsanteni.
Bro....kuliko kuangaika hapa na majibu...yanayo changanya changanya
Kwann usi mfate face to face

Umuulize kwann kakubadirikia?????

Mnapenda kuchosha watu!!!
 
Usoni haufurahishi na Utani, Moyoni Unautamani Uwe zaidi ya Utani
 
Wempigie pipe mkuu, utakuja kunishukuru badae
 
Back
Top Bottom