TIMING
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 28,186
- 15,549
Apumzike kwa amaniMwigizaji Mkongwe na Maarufu nchini Tanzania, Grace Mapunda amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es Salaam alipokuwa amelazwa kwa matibabu.
Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na Aziz Ahmed ambaye ni Muongozaji wa Tamthilia ambaye alikuwa akifanya naye kazi kwa ukaribu kwa muda mrefu.
Imeelezwa kua Grace hakuumwa muda mrefu, ila alipelekwa Hospitali juzi na usiku wa kuamkia leo Novemba 2, 2024 akapoteza uhai. Msiba upo nyumbani kwake Sinza Vatcan.
ILA hawa wanaoremba dada zetu siku hizi aisee
Wamekandika uso mzima chokaa hadi mtu anapoteza uasilia wake