Muimbaji wa injili Goodluck achoma moto gari alilopewa zawadi na mchungaji

Alibadili gari rangi? Iliyochomwa inaonekana kuwa na rangi nyeusi, tofauti na hii, licha ya namba za usajili kufanana T256 DRC

Si angeirudisha tu Kwa aliyempa? Chakula nacho amekitapika?
Madhabahu ya kichawi lazima yachomwe moto.
 
Atapata wapi hiyo million 2 na tayari anadai nyota yake imesepa na nabii,, asitufanye watu ni wajinga bwana Kuna mengi nje ya pazia anayaficha ila muda utasema.
Sema amekosa washauri huyu jamaa,. Hadi anatia huruma
 
Uongo mtupu.
1. Kwanza alipewa gari nyeupe/silver
2. Angalia tukio vizuri mwanzo mwisho...hajachoma chochote
Ko ww ulieangalia mwanzo hadi mwisho baadae mwisho alionekana akiondoka nalo, Au? Afu kuhusu rangi huko kwenu hamjui kama gari inabadilishwa rangi au? Yote kwa yote wewe ni bogus na m'bishi kenge.
 
Ile milioni mbili ya mafuta na tairi aliyopewa na chakula alichoshiriki ni hatari zaidi kuliko gari alilolichoma, sijaona ikipigwa moto.
Vijana tunaingia kwenye maagano kimyakimya sana ila kuchomoka siyo rahisi
 
Ko ww ulieangalia mwanzo hadi mwisho baadae mwisho alionekana akiondoka nalo, Au? Afu kuhusu rangi huko kwenu hamjui kama gari inabadilishwa rangi au? Yote kwa yote wewe ni bogus na m'bishi kenge.
We huwezi ku reason bila kutukana?
Ubogus si ndio huu wa kwako?
 
Gari aliyochoma na aliyopewa zinatofautiana rangi, aliyopewa ni nyeupe aliyochoma ni dark blue ukweli ukoje?.
 
Amshukuru Mungu kwa kumfunulia hilo.
Apambane kuikomboa nyota yake iliyoshikwa na ile madhabahu ya uwongo.
Ndomana tangu apewe zawadi amezimika kama mshumaa... Mungu amrehemu
Ilikuwa lazima kuchukua video wakati anaichoma hiyo gari ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…