Muliro: Tutashughulika na Makundi yanayopanga kufanya vurugu Novemba 6, hukumu ya Lissu

Muliro: Tutashughulika na Makundi yanayopanga kufanya vurugu Novemba 6, hukumu ya Lissu

View attachment 3703916

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewaonya watu wanaopanga kufanya vurugu siku ya hukumu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu itakayotolewa Novemba 6, 2026 katika Mahakama Kuu Masjala ndogo ya Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 3, 2026, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema wanazo taarifa za watu "Wanahamasishana kuja Dar es Salaam baadhi yao wakiwa na malengo ya kufanya fujo au vurugu."

Amesema jeshi hilo halitasita kuwashughulikia watu hao, huku akieleza kuwa mipaka na idadi ya watu wanaotakiwa kuingia mahakamani inafahamika hivyo.

..Polisi washughulike na chanzo.

..kwanini kuna wananchi wanahamasishana kufanya vurugu?

..je, ni kwasababu wananchi hao hawana imani na mahakama?

..Je, wananchi hawana imani na mahakama kwasababu inatumika na Ccm kuwakandamiza?
 
amani ndio msingi wa maendeleo

nawaunga mkono majeshi ya nchi hii
 
Hii ni ishara...

Na of course tumeielewa maana yake...

Sisi ni nani bhana, watu wadogo sana sisi...

Twamwachia Mola wetu mkuu atanena nanyi...

Sisi maguvu hatuna, mtapambana na mola wetu mkuu...

Wazee Lissu anafungwa bila kosa.
 
Halafu hamna hatari yoyote, polisi ni chanzo cha taharuki nchini

Upo sahihi

Tayari polisi washaleta taharuki katika jamii na wame shaonyesha pengine hukumu ya T. Lisu inaweza ikawa mbaya

Kwa viashiria hivyo itafanya wafuasi wa T. Lisu wajipange mapema na wajihandae kwa mashambulizi ya kupinga hiyo hukumu

na pia hata hukumu ikawa kuachiwa huru, furaha ya wafuasi wa T. Lisu itakuwa fujo na vurugu badala ya furaha maana tayari watakuwa wameshajiandaa kupambana na polisi
 
Roho za watu wasio na shida zitakuandama uzeeni mwako utakuwa hata njee unaogopa kukaa nani kwako saivi unaraha maana unaishi kwa wewe nikijana
 
Back
Top Bottom