Multiverse/parralel universe au wazo la many world interprentation wenye quantum mechanics je ni wazo tu kisanyasi au lina uhalisia ndani yake

Multiverse/parralel universe au wazo la many world interprentation wenye quantum mechanics je ni wazo tu kisanyasi au lina uhalisia ndani yake

dosho12

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2023
Posts
4,965
Reaction score
13,552
Multiverse ni wazo la kisayansi linalosema kuwa kuna uwezakano wa kuwa na ulimwengu au dunia nyingi na miongoni mwao huenda zikawa sawa na dunia yetu kumaanisha kuwa na version ya watu wa dunia na kanuni sawa na za dunia,
‎
‎Wazo hili sio geni bali limeanza zamani watu kama Atomist [mwana falsafa wa kigirii karne ya 16 BC ] alihisi kunaweza kuwa na ulimwengu usio na idadi wenye kanuni kama zetu, hata kabla yake wanajimu wa dini ya kihindu walishasema kuwa kuna mzunguko mubwa wa ulimwengu kama wetu unaharibika na kuanza tena upya, kwa sasa njia pekee multiverse inaweza kuwepo ni kutokana na wazo la burble universe linalosema kama Big Bang ilitengeneza ulimwengu je hilo tukio la Big Bang lilitokea wapi, hii inaonyesha kuwa kunauwezakano mkubwa wa kuwa ilimwengu ukawa hauna kikomo na uwezakno wa kuwepo Big Bang zaidi ya moja hivyo kufanya kuwa na ulimwengu kuwa kwenye kitu kama maputo pia kama ni hivyo kutokana na mathematics uwezakano wa ulimwengu au dunia kujirudia huenda ukawa na sheria na kanuni kama zetu au kuwa na mabadiriko kidogo.
‎
‎Pia kutokana na quantum mechanics inayoelezea vitu vidogo zaidi ya atom ambapo kwenye ulimwengu wake vinakuwa mfumo wa waves ila ukifanya mahesabu zinaonekana na particles wanasayansi hawajui ni kwa nini hivyo wakaja na hitimisho kuwa particles zina ulimwengu wake walioita Quantum realm ila hii ni kwa scale ndogo kwamba kama particles zinaweza kiufanya hivyo kwa nini ulimwengu mzima pia usiwe hivyo, nadharia ya multiverse inasema kuwa uhalisia wetu unatengeneza matawi tofauti kutokana na matukio na machaguo tunayofanya, ni kama concept ya “butterfly effect” inayosema hata kitu kidogokinaweza kusabisha madhara makubwa wazo limetolewa kwenye chaos theory kwamba hata mpigo wa mbawa za kipepeo aliyepo brazil unaweza kusababisha kimbuga texa, hivyo utafauti wa vitu vidogo kama machaguo ya kupanda usafiri huu badala ya huu mpaka machaguo ya kozi ya kusoma mtu wa kuoa yanaweza leta utafauti ambapo kama ungechagua kuhama shule ya sekondari basi kuna utauti ungekuwepo, hivyo wazo la mutiverse linasema kila unapo fanya uchaguzi basi ukiacha basi kuna ulimwengu mwingine ulifanya ule uchaguzi na maisha yako yapo tofauti
‎
‎Ni kama kurusha shilingi juu na kusubiri itue, sasa kwenye maisha tunayojua au uhalisia shilingi ile itatua aidha kichwa au mwenge ila kwenye quantum mechanics uchaguzi ule utagawanyika na ulimwengu mmoja itatua mwenge na mwingine itatua kichwa wanaita superposition kitu kuwa kwenye state mbili kwa wakati mmoja
AU kuna uchunguzi aliofanya mwanasayansi Erwin schrodinger unaofahamika kama Schrodiger's cat ambapo alisema fikiria” umemfungia paka kwenye boksi na ndani ya boksi kuna atom zinazotoa mionzi baada ya kuharibika pia kuna kifaa cha kupima pindi atom zinapo anza kuharibika pia kuna sumu inayoachiliwa baada ya atom kuharibia” hivyo kama hizo atom zitaharibik basi kifaa kitajua na kuachia sumu na paka atakufa au atom hazita haribika hivyo paka atauwa salama, hivyo kabla hujafungua bosi basi yule paka atakuwa amekufa na mzima kwa wakati mmoja, hivyo huenda kunauhalisia ambapo Afrika haikutawaliwa na wakoloni, uhalisia mwingine uliamua kuwa mwigizaji,daktari au hata haipo kabisa sababu baba yako aliamua kupanda basi lingine na hakukutana na mama yako hivyo hawakuonana
‎
‎Je kama kuna dunia nyingi na uhalisia huo upo wapi, kutokana na many worlds ulimwengu mwingine upo hapa hapa unatuzunguka ila hatuwezi kuona sababu zipo kwenye Dimension nyingine hivyo kwenye chumba chako una version nyingi zako, kuna mwingine unasoma kitabu, mwingine unaanalia Tv,Mwingine kuna watu wengine wanaishi, ulimwengu mwingine Melo hakutengeneza jamii forum hivyo watu wengine hatujuani.
‎
‎Unaweza kusema hili ni wazo tu la wanasayansi na pia kwenye movie za sci-fi ila wanasayansi wanafanya uchunguzi kwenye maabala za CERN na FERMI wakijaribu kufanya uchunguzi kutafuta dimension nyingine wa kugonganisha protons wa kasi ili kuona kama ile energy italeta particle kama Graviton ambayo ndio inabeba gravity na gravity inasemekana inaweza kuvuka dimension ingawa kutafuta hizo particle za graviton ni vigumu
‎
‎Huenda hizi dunia na ulimwengu mwingine upo ila changamoto inakuja inakuwa haiwezekani kwenda kuzitembelea sababu ya theory ya relativity kwamba hata uifanikiwa kwenda kwa kutumia Wormhole ambapo inasemekana unaweza kusafiri bila matatizo pia kutokana na principle una uwezakano wa kuunda Artificial wormhole ila ukirudi itakuwa ni miaka elfu imepita, pia kuna uwezakano wa ku experience huo uhalisia kupitia Mandela effect ambapo inasema kuwa kuna hali ya baadhi ya watu wakawa na kumbu kumbu za matukio ambayo hayajawahi kutokea, pia deja vu kuhisi ulishafika sehemu au kumjua mtu ambaye humjui pia hata ndoto inasemekana ni aina flani ya kupitia uhalisia wa ulimwengu mwingine inayoitwa Multiverse
‎
‎Wazo la kuwa na version nyingi za wewe kwenye dunia nyingi halisapotiwi sana kwenye abrahamic religions ila wazo la kuwa na ulimwengu tofauti na huu sio geni mabapo dini hizo zinasema uwezakano wa ulimwengu mwingine upo, pia kuna interpreations kwenye vitabu kama cha hebrew 1:2 wanatumia neno “ionas”ambapo inweza kuaamisha dunia au ulimwengu kwa wingi pia kwenye quran 17:70 inasema “tumempa cheo/kumapndisha mwanadamu juu ya viumbe wengi ila sio wote” na kwenye ukubwa waislamu wanaamini malaika,majini na wanyama wapo chini yao hivyo ni viumbe gani ambao wapo juu yao, inaweza kumaanisha vitu kama muda, kalamu na kitabu chenye matukio yote au hata mkunazi wenye kikomo pia inaweza kuwa tafsiri inayoongelewa , hii ni aina moja wapo ya kutafsiri ingawa vitabu vya dini haviaweka wazi uwepo wa dunia nyingine
‎
‎
‎Haya yote yanaweza kuwa kweli au sio kweli, haujulikana ila inaacha mawazo kuwa kama wazo hili linaweza kujadiliwa na watu toka enzi za zamani inaacha swali kuwa huenda kuna ukweli ndani yake na huenda siku za mbeleni sayansi inaweza kujibu haya maswali
‎
 
Mimi ni shahidi (shahidi binafsi anayejithibitishia mwenyewe) wa Jambo linalohusiana na Hilo, lakini sina uwezo wa kumthibitishia yoyote yule Kwani itaonekana kama ngano tu za kale, Baadhi ya vitu nilivyokutana navyo ni aidha ni dimensions nyingine Hapa hapa duniani au ni dunia nyingine ya mbali...Hadi leo nikifikiria hilo jambo najawa na hofu nisiyojua inatoka wapi.
 
Mimi ni shahidi (shahidi binafsi anayejithibitishia mwenyewe) wa Jambo linalohusiana na Hilo, lakini sina uwezo wa kumthibitishia yoyote yule Kwani itaonekana kama ngano tu za kale, Baadhi ya vitu nilivyokutana navyo ni aidha ni dimensions nyingine Hapa hapa duniani au ni dunia nyingine ya mbali...Hadi leo nikifikiria hilo jambo najawa na hofu nisiyojua inatoka wapi.
tupe kisa hata kimoja mkuu
 
Hayo yote ni mawazo ya kutokubaliana na ukweli kwamba ukifa umekufa, kunawatu wanajaribu kujipa matumaini kwamba wakifa leo watazaliwa tena kwenye dunia nyingine au ijayo baada ya hii.
Ndio upo sawa ni mawazo tu yanayosapotiwa na equation, ila uhalisia ni nini, ni ule unao uona wewe au ? Mfano ukienda kwenye jamii ambayo haijawa exposed na tecnnolojia ukiwambia kuna kifaa kinaweza tuma ujumbe kwa mtu aliye mbali na ujumbe kufika kwa haraka watakwambia pia hzo ni hadithi za abunuasi ila kwa wanajua wataona ni kawaida, hivyo kwa kuwa hatujui uhalisia tunatakiwa ku fikiria uhalisia kamili ni upi na kuna zaidi ya tunavyojua na kuona
 
Ndio upo sawa ni mawazo tu yanayosapotiwa na equation, ila uhalisia ni nini, ni ule unao uona wewe au ? Mfano ukienda kwenye jamii ambayo haijawa exposed na tecnnolojia ukiwambia kuna kifaa kinaweza tuma ujumbe kwa mtu aliye mbali na ujumbe kufika kwa haraka watakwambia pia hzo ni hadithi za abunuasi ila kwa wanajua wataona ni kawaida, hivyo kwa kuwa hatujui uhalisia tunatakiwa ku fikiria uhalisia kamili ni upi na kuna zaidi ya tunavyojua na kuona
Ni kweli acha tuupe wakati nafasi.
 
tupe kisa hata kimoja mkuu
Inshort, siku moja nilishawahi kuona silver object ikiwa ina "hang" angani, iko kama Yai vile, tena Hapa hapa Tanzania ( kaskazini mwa TZ) Niko kwenye usafiri na mwenzangu, nilidhani ndoto vile, Kila nilipozidi kusogea nayo inasogea, nilfikicha na kufumba macho ili nione ni ndoto lakini ilikuwa kweli, dakika kadhaa baadae kikapotea ghafla, ndani ya sekunde ni kama kikayeyuka vuuup...

sijui niseme ni kifaa au ndege au chombo cha usafiri Kwa jinsi nilivyoona kipindi hicho, kuna hali Fulani nilihisi ngumu Sana kuelezea, ni kama vile unahisi kuna interaction ya viumbe usiowaona ila wao wanakuona, unahisi mtu anasema "We are watching you" Inakuja strong feeling Kuwa Sisi species yetu ni ndogo Sana hasa kiakili na kimaarifa as if unaambiwa yako maisha Yana species za muda mrefu na zenye maarifa mengi ila ziko very humble...Hizi mambo huja maeneo ya karibu na maji.

It's so hard to explain Kwa yoyote ambaye hajakutana na Hali kama hizo, so hard Kwa kweli maana hakuna proof utakayotoa zaidi ya maneno ambayo ni ngumu watu kuamini, siku hizi nasoma Sana historia na kuzidi kutafuta mitandaoni watu waliokumbwa na vitu vilivyonikumba.
 
Proof moja ya existence ya multiverse ni ulimwengu wa roho na mwili, imagine mtu anatoka nje ya mwili anaenda kuwanga location nyingine kisha anarudi. Au anapaa kwa njia zisizo za kawaida kwa kasi ya umeme kwa njia za kichawi, ataebisha kuhusu hili tumeona mara nyingi wachawi wakoanguka na wengine hadi walirikodiwa na vyombo vya habari.
 
Yawezwkana
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    39.3 KB · Views: 33
  • E3JM3ZOXwAEM_IM.webp
    E3JM3ZOXwAEM_IM.webp
    72.8 KB · Views: 34
It's so hard to explain Kwa yoyote ambaye hajakutana na Hali kama hizo, so hard Kwa kweli maana hakuna proof utakayotoa zaidi ya maneno ambayo ni ngumu watu kuamini, siku hizi nasoma Sana historia na kuzidi kutafuta mitandaoni watu waliokumbwa na vitu vilivyonikumba.
Upo sahihi, binadamu huwa tunachukia na kupinga chochote kile ambacho hatukielewi, toka zamani watu walichomwa moto na kutengwa kutokana na mawazo na mitazamo yao
 
Multiverse ni very probable kabisa.

Kwanza elements zote ambazo zinaunda miili ya viumbe hai wote duniani, pamoja na vile visivyo hai, elements hizo zinapatikana popote kwa wingi mkubwa kwenye universe hii tunayoijua yenye umri wa miaka zaidi ya bilioni 13.

Elements hizo kama oxygen, carbon, hydrogen, iron, nitrogen, nk.

Msingi wa maisha ya viumbe wote duniani ni vinasaba (DNA). Na elements zinazounda DNA ni kama: carbon, hydrogen, nitrogen, phosorous, nk.

Kwa mantiki hiyo ni kwamba: It is very much possible that you may have an identical twin with similar and Identical DNA makeup as yours not even in another universe but in uknown planet existing here in our universe that we know and live.
 
Back
Top Bottom