Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Alighahiri kujiua?

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa risasi naye ajiua​

Mwanza. Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) naye amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa mtuhumiwa huyo ambaye mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Timejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Taarifa za uhakika zilizopatikana zinaeleza kuwa askari polisi wanaopeleleza tukio hilo walipiga kambi eneo la ufukwe wa Malaika kutokana na mawimbi ya mwisho ya mawaskliano ya mtuhumiwa Oswayo kuonekana eneo hilo kwa mara ya mwisho usiku wa kuamkia jana Mei 29.

"Mawasiliano ya mwisho ya simu ya Oswayo yalifanyika usiku wa manane eneo la Malaika; ndio maana Askari Polisi waliweka kambi pale na kweli mwili wake umepatikana hapo hapo," amesema mmoja wa watoa taarifa wetu kwa sharti la kuhifadhiwa jina
 
Kabisa!

Nilifanya maamuzi magumu mapema sana ,na kama nisingefanya hivyo huenda tungebadilishana majengo ya serikali
Binafsi nimetemana nae sina hata mwezi nae ni style hii pamoja na kuwa tuna watoto...
 
Kama muhusika amefariki,na mwingine hajulikani nyie mmejuaje kuwa alimkataza??
Mbongo mpe picha Tu. Stori ataiandika yote, mpaka nukta na alama za mishangao!
Kajiua huyo mwanaume mwili haujaonekana Ila kajiua, sasa Ka hakuna mwili ina uthibitisho gani kajiua!?
 
Anayedaiwa kumuua mkewe kwa risasi naye ajiua​

Mwanza. Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) naye amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa mtuhumiwa huyo ambaye mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Timejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Taarifa za uhakika zilizopatikana zinaeleza kuwa askari polisi wanaopeleleza tukio hilo walipiga kambi eneo la ufukwe wa Malaika kutokana na mawimbi ya mwisho ya mawaskliano ya mtuhumiwa Oswayo kuonekana eneo hilo kwa mara ya mwisho usiku wa kuamkia jana Mei 29.

"Mawasiliano ya mwisho ya simu ya Oswayo yalifanyika usiku wa manane eneo la Malaika; ndio maana Askari Polisi waliweka kambi pale na kweli mwili wake umepatikana hapo hapo," amesema mmoja wa watoa taarifa wetu kwa sharti la kuhifadhiwa jina
Mhh! Isijekuwa fake body for fake death! Watu wa Ziwani wana mambo ya ajabu
 
hata mie sijielewi kama nipo kwenye kadunia kangu ka peke yangu yaani, mwanamke hujawai nikwanza , mwanamke hujawai nikasirisha sio mwepesi wa kujibu, daah! Mda wote umekuwa furaha yangu.. tanga acha paitwe tanga umenimaliza [emoji41][emoji41]
Umeshaonja pepo yakhe. Kama huyo jamaa aliyeuwa inawezekana alikuwa kwenye tanuru kali la moto
 
Back
Top Bottom