View attachment 2244083
Wanawake tujitahidi kumaliza ujana kabla ya kuingia kwenye ndoa.
Pumzika kwa amani dada hukustahili kifo kama hiki na hakuna kosa lolote linaweza kuruhusu ufanyiwe unyama kama huu..
Mi naamini ni muhimu sana mwanamke ujue unataka nini maishani mwako na tuwasome saikolojia ya waume zetu.
Ukiingia kwenye ndoa ujue tu kwa Afrika chini ya mume,kama unataka amani ya ndoa yako kubali hilo utaishi kwa furaha,muhimu msome mume akili yake nk kama atafaa kuwa kiongozi kwako....
Nimekumbuka kuna siku nilimjibu mume jibu la hasara sana,mimi niliona ni jibu la kawaida lakini yeye lilimkwaza sana maana sikuwahi kuona hasira kama ile,nashukuru alikuwa safari laiti angekuwa karibu ni siku ambayo ningepigwa kwa mara ya kwanza.Talaka ilikuwa nje nje either nichague kuwa chini yake Au niondoke [emoji28][emoji28][emoji28]toka hio siku nipo makini sana na kauli zangu