Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

4913c4d316854185ae708c3bd491211d.jpg
261cddd9491e4ad9ae7dd013bcbd27f5.jpg
 
Dada zetu mkishakuwa na sura nzuri na mishepu huwa mnasumbua sana katika umri fulani lakini at the end huwa mnatia huruma na kuwa bad mentors kwa vijana wadogo wanaochipuki kutokana na frustration za kufanya umalaya na kuachwa hamna kitu....mkipigika sasa mnabaki na stress...
 
Kitu ambacho wanaume tunasahau nikwamba utiifu wa mke unapaswa kupaliliwa kila muda.

Sio wewe ni nunda husikilizi la mtu wewe ni wewe alafu unataka binti wa watu awe anakusiliza tu. (Kwa watoto wasasa hapo imekula kwako)

Ni wanawake wachache sana ambao waume zao sio watu wakutoka alafu yeye mke awe anatoka. Hapa hii ni familia ya kula bata ila inaonekana mwanaume amekua na ubabe mwingi bata zake hapangiwi wala wife hana mamlaka ya kutia neno ila bata za wife yeye anatia ngumu.

Nimejaribu tu kuwaza kwa sauti.
Hata ikiwa hivyo, ni mkewe so hata akimletea ubabe.
 

Anayedaiwa kumuua mkewe kwa risasi naye ajiua​


Mwanza. Said Oswayo anayedaiwa kumuua kwa kumpiga risasi kadhaa mke wake Swalha Salum (28) naye amekutwa amejiua kwa kujipiga risasi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amethibitisha kujiua kwa mtuhumiwa huyo ambaye mwili wake umekutwa ndani ya maji ya Ziwa Victoria kwenye ufukwe wa Rock Beach jijini Mwanza.

"Mwili huo umeopolewa ziwani eneo la ufukwe wa Rock Beach ukiwa na majeraha ya risasi kichwani. Timejiridhisha kuwa ndiye mtuhumiwa baada ya kutambuliwa na ndugu zake," amesema Kaimu Kamanda huyo.

Amesema mwili huo ulikutwa unaelea ufukweni mwa Ziwa Victoria ufukwe wa Rock Beach ambapo Jeshi la Polisi lililazimika kuwatafuta ndugu kwa utambulisho na kuthibitisha kuwa mtuhumiwa aliyekuwa anasakwa kwa mauaji ya mke wake.

Taarifa za uhakika zilizopatikana zinaeleza kuwa askari polisi wanaopeleleza tukio hilo walipiga kambi eneo la ufukwe wa Malaika kutokana na mawimbi ya mwisho ya mawaskliano ya mtuhumiwa Oswayo kuonekana eneo hilo kwa mara ya mwisho usiku wa kuamkia jana Mei 29.

"Mawasiliano ya mwisho ya simu ya Oswayo yalifanyika usiku wa manane eneo la Malaika; ndio maana Askari Polisi waliweka kambi pale na kweli mwili wake umepatikana hapo hapo," amesema mmoja wa watoa taarifa wetu kwa sharti la kuhifadhiwa jina
 
Unaweza kuta kamwambia katika wanaume wote naowajua, ww ndio sio mwanaume nimekosea sana kukaa na ww, natamani uniue kabisa sasa hivi, akamalizia niue niuee, niuee, niuee sasa, niuee, nimechoka, nasema niueeeee, alafu kamtemea mate usoni mara kibao, alafu anampiga piga na vibao ili amuue, alafu anamkanyaga miguu, mateke ili amuue, anampiga vibao vya kila mahali ili amuue, yaani anataka kuuawa, hata ingekuwa mm nitafanyaje sasa.
Nina mambo mengi sana ya kumuuliza Eva siku nikikutana nae,
 
Mwanamke amepewa heshima kubwa sana ya kuitwa Mama, tafsiri ya mama ni mlezi wa familia na mmiliki wa majukumu yote ya nyumbani nyuma ya mwanamme, ni mlinzi na mlezi wa familia na kioo cha nyumba,mtunza siri za nyumba, mmiliki funguo za ndoa na mwisho kabisa ndiye kiumbe mwenye nafasi ya kumshape mme na familia..

Hivyo vyite juu vitawezekana san kama Mwanamke anakuwa mtulivu, mwenye heshima na hekima, mvumilivu na mwenye hofu ya Mungu na kufahamu vizuri kwanini yeye ni mwanamke na nafasi yake ni nini...
 
Kwanini wasingeenda wote mwanaume tumeshaambiwa tuishi nao wanawake kwa akili na sio mabavu, kwanini hakumshauri bibie waende wote shida ipo wapi kuna watu ni hasara sana kwa taifa
Wapo watu kuingia kwenye hizo kelele za clubs sijui matamasha hawawezi siyo hobby yao,binafsi mimi hata kwenye sherehe za kijamii za rafiki na ndugu huwa siendi na michango natoa so ni vigumu mtu kama huyu mwanamke kumshika mkono kumpeleka huko.
 
Kwa Mwanamke kufanya usaliti kwenye familia ni sawa na askari aliyeasi na kumwaga siri za nchi hadharani kwa adui..

Mwanamke unapomsaliti mwanaume, au Mwanamme anapowaza umemsaliti basi tambua ni sawa na nchi iliyovamiwa na kutekwa na adui...HAPA NDIO MAANA TUNASEMA NAFASI YA MWANAMKE NI KUBWA SANA KWENYE NDOA..

kwenye uumbaji mwanamke ameumbwa kumilikiwa na mwanamme mmoja ndio maana usaliti wa mwanamke kwa mwanaume huwa na impact kubwa kuliko Mwanamme akimsaliti mwanamke...."hili ni suala la uumbaji".....Ni ngumu Mwanamme kusamehe usaliti wa mwanamke lakini ni rahisi mwanamke kusamehe usaliti wa mwanamme hata kama kamfuma kitandani....this is nature...
 
Mama wa marehemu kasema simu ya mwanaume ilosoma maeneo ya tunza.Tunza ni maeneo ya mwambao wa ziwa na mwanaume ni mvuvi na kutoka buswelu mpaka tunza ni karibu kupitia kiseke mimi naamini jamaa yupo kakimbia mjini tu.
Inawezekama amekimbia na boat, sasa kama alikimbia na boat, basi aliwaliliana na watu kabla ya kuondoka, kama ni dereva wake wa boat, au msimamizi wa boat zake, yani mnyororo wa kumpata ni mwepesi sana, usiku asingeweza nunua line mpya, ina maana alifanya mawasiliano na line yake tu. Hao watu wa mwisho kufanya nao mawasiliano wanajua wamemuacha kisiwa gani.

Japo kama alikuwa na mkwanja mrefu sasa hivi atakuwa ashavuka boda, yupo Uganda, anaenda anza maisha mapya.
 
Huyu Dada hakuwa na Utii na Mme Wake, Hakuna watu ambao wanaumizwa na majibu ya Mwanamke kama Mwanaume.
.
Hatuwezi Jua baada ya Marehemu Kurudi Huko Alimjibu Nini Mwanaume Wake.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Ndio maana inatakiwa mbali na kuangalia kigezo cha "pisi kali" kuna vigezo vingine vya ziada vya kuendana na yule unaeoa / olewa nae au kumfanya aendane na kile ambacho unakiamini. Ukute amemchoropoa huko huko kwenye club na tena alikuwa na mtu wake ila kwa kuwa yeye alikuwa muoji demu akaingia king na ukiangalia na muda wa hiyo ndoa yao inaonyesha kabisa bado walikuwa kwenye window period ya kuwekana sawa.

All in all naungana na wewe kwamba hatuwezi jua alimjibu nini mme wake huko
 
Mungu anasema atakupa wa kufanana nawe
Kama jamaa hakupenda mambo ya kutoka usiku au ya starehe why alioa wa hivyo?
Tukifatisha maandiko yanavyosema kwa habari za ndoa mambo kama haya yatapungua sana!
Biblia inasema enyi wake watiini waume źenu,imagine hujamuoa ila wala hakuheshimu unadhani atakuheshimu mkiwa kwenye ndoa?
Wanaume jifunzeni kwa huyu mwenzenu,ukitaka kuoa tafuta unaeona anaendana na maono yako!la sivyo mtaua sana na mtaozea jela,
 
Hakuna sababu yeyote ile inayo halalisha mauaji let alone hizo petty reasons.

Mtu aende kwenye show ndo sababu ya kumuua au kisa hakusikilizi ndo umuue?

Mke sio mtumwa wako akose uhuru wake na kuacha Kila kitu anachopenda na kufanya unayotaka wewe tu sio kifungo hicho.

Hii victim blaming inabidi iishe na watu wajue ndoa sio utumwa. Mkishindwana mnaachana it's that simple sio kutoa uhai wa mtu. Imagine dada au Binti yako anauwawa kwa hivi visababu uchwara. Hakuna sababu yeyote ile inayo guarantee kutoa uhai wa mtu.
Tatizo uhuru huo ndo unasababisha usaliti, hakuna mwanaume anaweza vumilia kuchapiwa hiyo ni asili, so nyie wanawake inabidi kabla hujamsaliti mme wako ni bora ukaondoka hapo kwa mwanamme, sio unafanya usaliti then unarudi kupata hifadhi.
 
Inawezekama amekimbia na boat, sasa kama alikimbia na boat, basi aliwaliliana na watu kabla ya kuondoka, kama ni dereva wake wa boat, au msimamizi wa boat zake, yani mnyororo wa kumpata ni mwepesi sana, usiku asingeweza nunua line mpya, ina maana alifanya mawasiliano na line yake tu. Hao watu wa mwisho kufanya nao mawasiliano wanajua wamemuacha kisiwa gani.

Japo kama alikuwa na mkwanja mrefu sasa hivi atakuwa ashavuka boda, yupo Uganda, anaenda anza maisha mapya.
Inawezekana ikawa hivyo kwa mazingira ya tukio jamaa alijiandaa mapema
 
Back
Top Bottom