Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

RIP dada mzuri,

Huyu dada alikua ni make up artist na designer, na ni maarufu mwanza, pia ndoa yao ilikua ina migogoro tangu mda kisa ni Usaliti, mwanamke alikua na jamaa mwingne nje.

Siku ya tukio, Dada na mumewe walienda kwa match ya simba na yanga, baada ya hapo wakarudi home, baadae dada akaomba ruhusa ya kutaka kwenda kuangalia mpira wa UEFA, mumewe akagoma, ktk mabishano bidada akaamua kuondoka kwa kiburi chake.

Sasa kumbe huko kwa Mpira wa UEFA ndo alikua na mchepuko wake, kuna watu walimuona wakamtonya mumewe, machale ya bidada yakamcheza wakaondoka na jamaa ake pale eneo, mumewe alivyofika pale hakuwakuta, kila akimchek kwa cm kimyaa, bidada cm alizima, mumewe akarud home kumsubiri.

Bidada naye baada ya kutosheka huko alikokua na jamaa, akaamua kurudi home, kufika home ndo akakutana na mumewe ktk maulizano bidada akatoa maneno ya kashfa kwa mumewe, mume uvumivu ukamshinda akaamua awashe kitu cha moto, paah paah paaah paaaah paaah, nayeye kusepa hapo hapo.

Marafiki na watu karibu wa huyu dada wanasema alikua anawaambia ukweli kuwa hampendi kwa dhati mumewe, ila yupo nae kwa kuwa ana pesa, na amemsaidia vingi ktk maisha, ila upendo wa dhati kwake hana. Mwishoe ndo haya yaliyotokea.

Mtu km humpendi bora umuache hata km ana pesa, wee kuwa na unaempenda mtafute wote, huku kujidanganya kuwa unaweza fake, matokeo yake ni hataree. Mapenzi yana nguvu mnoo na hayafichiki.

RIP dada mzuri, Tamaa mbele, Mauti nyuma.
angemkuta na huyo jamaa nadhani angeuwa wote
 
Nakumbuka moja ya mahusiano yangu niliyopitia niliwahi kuwa na mwanaume mpigaji niliambiwa na wadogo zake na rafiki zake ila kwangu hakuwahi nipiga hata kofi yeye mwenyewe alikuwa anajishangaa.
Kauli za wanawake wa Tanga unajikuta tu unashindwa kunyanyua mkono. Ukarimu wa mwanamke kwa mumewe huleta maelewano bila kutumia nguvu
 
hatari
FB_IMG_1653919476246.jpeg
 
Hata mke anitukane matusi yote hakuna tusi jipya sio kumuua mtu,sasa unampiga mke risasi kwa vile huna nguvu za kumpiga vibao...ukiona mke hamuwezani achane nae uongeze siku za kuishi
Hayajakukuta wewe!!!
 
Ukimuoa mtu haujanunua uhuru wake?

Kwa hiyo ukiolewa unarudi home unarudi muda unaojisikia? Unaenda popote unapotaka? Acha muendelee kula risasi za.kichwa tu.
Sawa na jamaa yenu kajiua nae
 
Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri

==================================

Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe ambao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakawandelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kwa kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.

Dah RIP mrembo
 
Wanawake mnapenda wanaume wenye pesa ila hamna uwezo wakuwatimizia mapenzi while wanaume mnapenda Wanawake wazuri ila hamna mioyo yakukabiliana na warembo wazuri na mwisho mnauwana
 
Kupata mwanamke anaekusikiliza na kukuheshimu kama baba yake ni baraka kubwa sana ambayo wengi wanaikosa katika kizazi hiki, Asante Mungu.

Muda mwingine sisi wanaume tunashindwa kusimamia uanaume wetu, hivi Mungu kakujalia Pesa na afya ya nini kung'ang'ania mwanamke anaekuumiza akili?? Najua mapenzi yanauma na pengine labda kuna watu wapo humu jf muda huu wanapitia fukuto la mahusiano, nawashauri mfanye maamzi ya kiume kabla hamjachelewa.

"Every woman in any given reletionship, is taken as the man's project".

Project imekushinda, achia wengine wahangaike nayo kwanini uumie?
"Project" nzuri hivyo kama Marehenu Swalha alivyo unawezaje kuiacha kirahisi rahisi hivyo wanaume wengine waendelee nayo?
Damn! That woman was beautiful. The guy had all the rights to be jealous, who wouldn't?
 
Sasa huyo Ngosha na yeye ndo mwisho wake. Ataishia jela incase akiwa bado hajajiua. Hakuna faida atakayoipata kwa kuondoa uhai wa Swalha. Si angempa talaka 3 tu.Tena Waislam ni rahisi sana kutoa Talaka.
Kajipa kazi ya kutoa uhai wa mwanadamu ambayo si yake, hukumu ya Mungu yamhusu! inaelekea kabisa alikuwa anatumia nguvu ya pesa wakati hakuwa anapendwa na inaelekea alikuwa anajua kuwa hapendwi. Pesa kamwe haiwezi nunua kila kitu.
 
Back
Top Bottom