Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa kumpiga risasi 7 kichwani, chanzo ni simu. Mume naye akutwa AMEFARIKI

Umeona eeh
Mbona wa kawaida sana tena hata mavazi yake sio ya kihivyo. .mrembo gani anashona nguo kwa fundi wa uswahilini haina hata finninshing?? Nguo isiyo na mabega alivyovaa unaona ilivyopwaya kila mahali?? Mshamba tu aliyezibuka baada ya kupata wa kumpa hela mbili tatu mjini
Wakawaida Sana,sijaona pisi hapo,
FB_IMG_16539272364923883.jpg
 
Wakuu story ni kwamba huyu jamaa kwenye picha amemuua huyo mkewe usiku wa kuamkia leo huko Mwanza ikidaiwa ni baada ya kumkataza mkewe asiende kwenye show ya Mondi.

Baada ya kumwambia asiende kwenye hiyo show ya Nasib Abdul, mke akakaidi akaenda.

Jamaa amempiga risasi saba za kichwa na inasemekana na yeye kajiua japo maiti yake haijaonekana.

Ila na nyie Wanawake mpunguze visirani. Inaonesha jinsi huyu Marehemu alikuwa mkaidi na hamsikilizi Mme wake.

Mme kakuambia sitaki uende pahala fulani then wewe unakaidi ni nini kama sio dharau na kiburi?

By the way anything else Happen for a reason.

RIP Binti Mzuri


==================================

Baada ya kifo cha Swalha Salum kilichotokea Mei 28, 2022 maeneo ya Busweli Jijini Mwanza, Mama mzazi wa marehemu, Bi Tiba Mohamed anasimulia kilichotokea kuhusu ndoa ya mwanaye na mumewe, Said Oswayo ambapo wahusika hao wamedumu katika ndoa kwa muda wa miezi mitano, kwani walifunga pingu za maisha Desemba 30, 2021.

Anasimulia: “Watoto wangu waliitwa na baba yao hapa nyumbani (Mei 28, 2022), walipofika baba yao akapata dharura hivyo hakuzungumza nao nikabaki nao tukawa tunataniana tu.

“Alikuwa akinitania kwa kufurahi kuwafunga Simba akawa anishawishi na mimi nihamie Yanga (Yanga iliifunga Simba bao 1-0 siku hiyo kwenye CCM Kirumba Mei 28, 2022).

“Baadaye baba yake akapiga simu na kusema mume wa Swalha amepiga simu kumjulisha kuwa amefika na hivyo Swalha aende akampokee Igombe.

“Swalha akasema gari yake haina mafuta, hivyo wakakubaliana wakutane nyumbani na mwanaume akasisitiza kuwa ana njaa sana, akamtaka mke wake aende akampikie.

“Nikawasindikiza hadi barabarani mida ya saa moja usiku, muda huohuo mume wake akapiga simu akiwa anafoka, nikamtaka awe na subira mkewe anakuja yupo njiani.

CHANZO CHA UGOMVI
“Kuhusu ugomvi kati yao labda ni kuhusu simu, Jumatano iliyopita alipata tenda ya kwenda kumpodoa bibi harusi Shinyanga. Alipofika huko wakati akiwa kwenye kazi mume akawa anapigapiga simu, Swalha akawa anamwambia asimpigie kwa kuwa yupo kwenye kazi.

“Ijumaa jioni akawa anamtafuta hivyohivyo na kumsisitiza arudi nyumbani, Ijumaa hiyohiyo jioni akarudi akafika nyumbani usiku, mume akawa anapiga simu, Swalha akapokea na kumwambia anaomba apumzike kwa kuwa amepodoa watu wengi na amesimama muda mrefu hivyo amechoka.

“Mwanaume akawa anaendelea kupiga simu usiku huohuo, Swalha akalala, alikuja kushtuka saa tisa usiku akakuta miss call 42. Akampigia alivyopokea wakaanza kukwaruzana tena, mwanaume akawa analalamika na kumfokea alikuwa wapi na anafanya nini mpaka hapokei simu.

“Swalha alivyoona wanazidi kugombana akaamua kuweka simu pembeni ili ugomvi usiwe mkubwa.

“Asubuhi yake mume wake akanipigia simu na kusema kuwa mke wake amemjibu vibaya. Kwa hiyo ndio akapanga kurudi Mwanza.

“Baba yake alivyomuita hapa nyumbani nadhani alitaka wazungumze kuhusu hilo, lakini ikatokea wamepishana na mume alivyofika nadhani ugomvi utakuwa uliendelea.

KUHUSU KUPIGWA RISASI
“Taarifa ni za kweli, pale ndani (wanapoishi Swalha na mumewe) kulikuwa na watoto watatu wametuambia risasi zilipigwa.

“Wanasema huyo baba alikuwa na kawaida ya kuijaribu silaha yake, mara nyingine anapiga hewani, hivyo walivyosikia mlio wa risasi wakaendelea kulala.

“Ni hadi waliposikia Swalha amepiga kelele mara moja tu lakini risasi zikawa zinaendelea kupigwa. Mtoto mmoja akaenda kusikiliza mlangoni kwa Swalha kisha akatoka mbio kwenda kuwataarifu majirani.

“Wakaenda Polisi, kumbe yule mtoto alivyotoka tu yule baba naye (mume wa Swalha) akaondoka. Polisi walivyofika wakauchukua mwili wa Swalha.

“Taarifa za tukio sisi tulianza kuzipata kutoka Kisiwani huko anapofanyia kazi (mume wa Swalha), ndipo majirani wa Swalha na askari wakaja kutoa taarifa wakisema mwanangu ana hali mbaya ameshambuliwa kwa risasi.

“Baba Swalha akaondoka na ndugu zangu kwenda huko maana nilibaki nyumbani, niliishiwa nguvu baada ya taarifa hizo, nikashindwa kwenda, saa tisa usiku wakarejea na ndipo nikajulishwa kuwa Swalha ameshafariki dunia.

“Marehemu hakuwa na mtoto na sijajua nini kinaendelea mpaka sasa.

“Kuhusu huyo mume wake haijulikani yuko wapi, kwani Polisi mara ya mwisho walisema wameangalia simu yake ikaonekana yupo maeneo ya Tunza.”

JESHI LA POLISI LINAMSAKA MTUHUMIWA
Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ramadhani Ng'anzi ni kuwa ni kweli tukio hilo limetokea kutokana na mgogoro wa ndani wa kifamilia na mtuhumiwa ametoroka, anaendelea kusakwa kwa kuwa alitoroka baada ya tukio.

Kuhusu madai kuwa mtuhumiwa ni mtu wa usalama kama inavyodaiwa na baadhi ya watu amesema sio kweli, ni mvuvi na anamiliki silaha yake kihalali. Jina lake halijatajwa kutokana na sababu maalum.


MUME NAYE AKUTWA AKIWA AMEFARIKI
Said Oswayo anayedaiwa kuhusika na mauaji ya mkewe, Swalha Salum ikidaiwa alimuua kwa kumfyatulia risasi kadhaa amekutwa amefariki na mwili wake kuokotwa kando ya Ziwa Victoria katika Ufukwe wa Rock Jijini Mwanza, leo Mei 30, 2022

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Mairi Makori amesema: "Mwili umekutwa kandokando ya ziwa na umetambuliwa na mmoja wa ndugu zake. Umekutwa na tundu kichwani."

"Inavyoonekana hajafia hapa, aliletwa na maji, inasadikika amejiua kwa risasi lakini uchunguzi unafanyika na tutatoa ripoti kamili."


Huyu bwana pia ni kada?😂
 
Aisee madini wanayotoa warembo wa jf yanakushawishi uweke mke ndani lakini unabaki unajiuliza hawa wa jf sii ndio hawa hawa wa mtaani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Tulia
 
Hahahahahaha wakiwa huko nje wanakuwa kama marehemu mbishii
Kabisa wabishi na jeuri juu....lakini hapa sii unasema wife material ndio hawa bwana.🤣🤣🤣🤣

Sasa kwenye vikao vyenu muwage mnawaalika hawa pisi kali naonwapate funzo
 
Tuachane na Saidi unaemuita kolo, hiyo kazi aliyokuwa anafanya Swalha inayomfanya ashindwe kujaza mafuta kwenye hako ka IST au Raumu unakokaona ni hovyo, ni kazi gani? Si bora abaki nyumbani tu sasa kuliko kuzurura hovyo😂.

Unauliza kwa hela gani ila wengi humu hata kuingiza 1M kwa nguvu na akili zenu hamuwezi bila ya kutegemea wanaume, ni either mdange au muombe waume wenu. Wanawake wenye akili za kutengeneza pesa zao zisizo na makandokando ni wachache sana Tz hii

Achenu dharau.
Tuko wachache sana. Mimi nategemea kipato changu 100% , sijawahi tegemea hela ya mtu toka nimeanza maisha. Wanawake wanaopenda starehe mara nyingi hela sio za jasho lau, hela unayoipata kwa kukomaa ni lazima uitumie kwa staha. Mapenzi yanaumiza , lakini ukiona mtu huendani naye mwache aende, usifanye maamuzi ambayo yatakufanya uumie maisha yako yote. Bora uumie kwa muda
 
Badili mindset kuona mke ni wakumtandika na silaha yoyote brother love is good hasa ukimpata anaekustahili
Binafsi sina mtizamo huo hata kupigi sina uwezo huo. But kama mtu anahasira inafaa ajitahid kuwa mbal na vileta hasira na afunge mikkono yake mawe mazito ashindwe kupiga ama kubeba zana ya kumdhuru mtu
 
Binafsi sina mtizamo huo hata kupigi sina uwezo huo. But kama mtu anahasira inafaa ajitahid kuwa mbal na vileta hasira na afunge mikkono yake mawe mazito ashindwe kupiga ama kubeba zana ya kumdhuru mtu
Kweli brother, they deserve to ave a second chance muache aishi na akaishi na mwanaume mwingine, hakuna adhabu kali kama kumuacha mwanamke uliemjali ukampa kila kitu na uliempenda haswa, muache akaanze maisha na mwanaume mwingine atakufa kwa kuwaza uzuri uliempa, na sio kumuua
 
Plus filter ndugu
Angekuwa mrembo kuanzia ndani asingewahishwa ahera kwa risasi.
Kuna mwanaume alisema wanaume huwa wanamtoa thamani mwanamke anayewadharau na kuwakaidi hata akiwa mrembo vipi...
Ni kweli,mwanamke mazingira

Mwanamke jitunze,jiheshimu,heshimu mume,

Sema siku wengi tunaolewa na hatujui ndoa ni nini???
 
Kabisa wabishi na jeuri juu....lakini hapa sii unasema wife material ndio hawa bwana.[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Sasa kwenye vikao vyenu muwage mnawaalika hawa pisi kali naonwapate funzo
Niliwahi kwenda geto kwa mdada flani ambaye anadanga... anavyojipodoa sasa utasema mke si huyu..
Basi siku ya siku kuna shoga yake sijui alitaka kumkomoa au vipi si akanipitisha kwake bila yeye kujua maana huwa anaachiwa funguo...weeee vyombo vilivyotumika toka asubuhi vimetapakaa chini na havijaoshwa tangu mchana na mda huo napita ni saa 11 jioni, kitanda hakijatandikwa, miguo imepatapakaa tu haieleweki... basi siku nyingine nikiwa huo mkoa huo nikawa nimeishiwa hela baada ya malipo flani nimebaki na nauli tu. Nikamwambia naomba nije kulala kwako...kwani alikubali?? Alinipeleka kwa rafiki yake.
Wanawake waone tu barabarani wamependeza ila wengine hata kufuta watoto wao makamasi ni tatizo...
Kama unaoa hawa basi Acha kumiliki bastola, panga, shoka, kisu , bisibisi na vifaa vingine vyenye ncha kali
 
Umeona eeh
Mbona wa kawaida sana tena hata mavazi yake sio ya kihivyo. .mrembo gani anashona nguo kwa fundi wa uswahilini haina hata finninshing?? Nguo isiyo na mabega alivyovaa unaona ilivyopwaya kila mahali?? Mshamba tu aliyezibuka baada ya kupata wa kumpa hela mbili tatu mjini
MH, hapa kuna chembechembe za jealous dhidi ya huyo dada
 
Tunajua nyie hampendani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23]mzab niache kwanza,,,hapa nimejivisha ngozi ya chui[emoji41]

Halafu eti mke unaendaje kwenye shoo??
 
Kweli brother, they deserve to ave a second chance muache aishi na akaishi na mwanaume mwingine, hakuna adhabu kali kama kumuacha mwanamke uliemjali ukampa kila kitu na uliempenda haswa, muache akaanze maisha na mwanaume mwingine atakufa kwa kuwaza uzuri uliempa, na sio kumuua
Kweli kabisa mkuu. Yafaa siku zote kutengeneza akili zetu katika mtizamo chanya zaid
 
Back
Top Bottom