Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Baada ya utimamu kumrudia ndio maana akakimbilia police yaonekana huyu hakua na nia alikua provoked mpaka akarukwa na akili

kuna taarifa nimesikia jana kwa mtu. Anasema kuna ndugu yake kamuambia. Ambaye yeye (ndugu yake) yuko karibu na hiyo familia.

Jamaa Aliachishwa kazi siku nying kidogo. Mama ndio analea familia, Jamaa akawa ana mtuhumu mke wake kuchepuka.
Kwahiyo ugomvi wao siku nyingi ndio huo.
mke alivyoona jamaa hasamehi akawa anataka kufanya process za Talaka . Ili mali zibaki kwa watoto.

Sasa nadhan ishu sio Mali kubaki kwa watoto. Ishu ni mwanaume hakusamehe ule usaliti.
fukuto na maneno yakawa mengi baina yao na ndio mwanamke akaamua kuanzisha mchakato wa talaka.

Ila mwanaume akaamua kumleftisha kabisa ili na huyo mwanaume anayemla amkose.
 
Kumbe za ndani, mwamba na huyo dada wote familia bora.Huyo jamaa familia yake kila mtu anaifahamu nikiitaja, wana kiwanda n.k
Jamaa uchumi uliyumba, kapata frustration akapigwa na kisukari.Demu kawehuka kaanza kuomba talaka na kutaka kuuza mali - jamaa kagoma anamwambia mali za watoto.Dada kiburi kikajaa, kaanza kuzingua, aliondoka nyumbani mwezi mzima hayupo huyo dada, anakolala anajua mwenyewe.Jamaa naye akaenda zake Moshi.Dada kurudi juzi, majirani wakampigia simu, mkeo karudi, jamaa katoka moshi, kapanda chuma cha usiku, anaingia kwake saa 11 asubuhi.Kakuta dada wa kazi anaandaa watoto kwenda shule, kauliza mama yuko wapi kaambiwa chumbani, kwenda huko kilichotokea hakijulikani, milio ya risasi ikaunguruma.Jamaa katoka kaenda kwa dada wa kazi, kamuambia nimeishamalizz kazi yangu kaenda zake kawe kituoni kujisalimisha, Dada ndo kwenda chumbani kakuta jamaa kafumua kichwa

Nimesikia story kama hii.

Itakuwa ni kweli Jamaa uchumi umeyumba.
Na jamaa alikuwa anahisi mke wake ana mwanaume mwingine.
Na pia ana process talaka.

Kwahiyo vyote hivi Mwanaume ameshindwa kuvivumilia. Akaamua wakose wote.
 
Kwamba niache mali zangu nilizozihangaikia miaka yote kisha nikawe mpangaji tena kwenye gheto kama Genz?hilo haliingii akilini aisee
Kwani hizo mali ulihangaika peke yako? Imagine huyo mwanamke inaonekana wana watoto wanne!!! Hivi katika maisha hadi mnapata watoto wanne ni miaka mingapi hapo imepita???!!!!

Kwa hesabu za harakaharaka siyo chini ya miaka 10!!! Mke alikuwa anafanya kazi. Ni mambo mangapi mke kachangia katika ukuaji wa hiyo familia?

Inasemekana hapo Bunju wamehamia hata mwaka haujamalizika which means that hiyo nyumba imejengwa wakiwa ndani ya ndoa. Sasa kwa nini wachangiaji wengi humu mnaona kuwa hizo mali zilizopatikana ni haki ya huyo mwanaume tu??? Wanaume acheni ubinafsi.
 
Mambo haya ...mtu kashazoea kujiweka status kua yeye wako na pesa na Ile kukaa na marafiki kujimwambafai na mashosti una hela, mume ana hela, kujiweka status Instagram na TikTok, mwenzio kayumba kidogo , badala u play a role as a loving wife and supporting wife kama ambavyo alikua anafanya hivyo kwako, wewe ndio unamuongezea matatizo, halaf eti unataka kuuza Mali ambazo watoto ndio mnawatengenezea kesho yao, halafu unaondoka nyumbani mwezi mzima, watoto hujui wanakula nini ama vipi, aise inahitaji moyo wa kipekee sana kutokuua. Tena ANARUDI na kujilalia zake, watoto wanaandaliwa na dada wa kazi
Mimi kama nisingeua basi ningemchukua dada wa kazi kama mke mpya
Mbona huzungumzii sehemu inayosema kuwa huyo mwanaume naye hakuwepo nyumbani kwa muda wa miezi miwili? Alikuwa hajui pia watoto wanaishije. Why lawama ni kwa mwanamke tu? Men acheni ubinafsi na kujiona nyie ni malaika.
 
Huyu jamaa kama nilisikia story yake, clouds FM Asubuhi.

Nilisikia kwamba walikuwa na nyumba ambayo hati imeandikwa majina ya watoto na ya WAZAZI wote, yaan mume na mke.


Wakasema pia mke akaanza taratibu zakubadilisha majina ya umiliki amtoe mume,

Kesi ilikuwa mahakamani, wakati kesi ikiwa mahakamani mwanaume akapata taarifa kuwa mke wake amejenga nyumba kigamboni akatafuta ushahid akauleta mahakamani

Kwa lengo nayeye akitaka wagawane hiyo nyumba ya kigamboni.

Then walimuhoji house girl wao alikuwa wameishi nae Kwa miaka nane alisema kuwa walikuwa wanamigogoro ya kimya kimya
Ndipo siku ya siku mwanaume kamshuti mwanke

Wanaume tunapitishwa kwenye motooo saana
Sioni justification yoyote ya kumuua huyo Dada.
 
Kwani hizo mali ulihangaika peke yako? Imagine huyo mwanamke inaonekana wana watoto wanne!!! Hivi katika maisha hadi mnapata watoto wanne ni miaka mingapi hapo imepita???!!!!

Kwa hesabu za harakaharaka siyo chini ya miaka 10!!! Mke alikuwa anafanya kazi. Ni mambo mangapi mke kachangia katika ukuaji wa hiyo familia?

Inasemekana hapo Bunju wamehamia hata mwaka haujamalizika which means that hiyo nyumba imejengwa wakiwa ndani ya ndoa. Sasa kwa nini wachangiaji wengi humu mnaona kuwa hizo mali zilizopatikana ni haki ya huyo mwanaume tu??? Wanaume acheni ubinafsi.
Kwa hiyo tulijenga nyumba ili tugawane au ili kujenga familia?
 
Tatizo unyanyasaji bro
Halafu wao wanaona sawa tu!!! Eti mwanamke naye ni mali ya mwanaume!!!! Mimi ndiyo sababu huwa napinga sana kuhusu mwanamke kutolewa mahari!! Wanaume wanaona ni kama ANAMNUNUA Mwanamke kwa hiyo anakuwa ni sawa na ng'ombe, mbuzi, gari na kitu chochote mwanaume anachomiliki!!! Ataku-treat the way he likes!!!! Shit!!!!!!
 
JUZI KATI HAPA NILIWAAMBIA SULUHISHO LA HAYA NI NYUMBA NDOGO....
Sasa huyu bwashee ndio kafanya nini,,,,,,, mwana kashindwa jizuia manake aliwekeza hisia kwa kiwango kikubwa...kama angekuwa na nyumba ndogo haya yasingetokea....hasira zikipanda unapotelea nyumba ndogo kwa kitambo mpaka upone.
Tena nyumba ndogo ziwe zaidi ya mbili.... As long as uwe na uwezo wa kuzihudumia vzuri,
 
Back
Top Bottom