Mume adaiwa kumuua mkewe kwa risasi huko Bunju, Dar es Salaam

Baada ya utimamu kumrudia ndio maana akakimbilia police yaonekana huyu hakua na nia alikua provoked mpaka akarukwa na akili

kuna taarifa nimesikia jana kwa mtu. Anasema kuna ndugu yake kamuambia. Ambaye yeye (ndugu yake) yuko karibu na hiyo familia.

Jamaa Aliachishwa kazi siku nying kidogo. Mama ndio analea familia, Jamaa akawa ana mtuhumu mke wake kuchepuka.
Kwahiyo ugomvi wao siku nyingi ndio huo.
mke alivyoona jamaa hasamehi akawa anataka kufanya process za Talaka . Ili mali zibaki kwa watoto.

Sasa nadhan ishu sio Mali kubaki kwa watoto. Ishu ni mwanaume hakusamehe ule usaliti.
fukuto na maneno yakawa mengi baina yao na ndio mwanamke akaamua kuanzisha mchakato wa talaka.

Ila mwanaume akaamua kumleftisha kabisa ili na huyo mwanaume anayemla amkose.
 

Nimesikia story kama hii.

Itakuwa ni kweli Jamaa uchumi umeyumba.
Na jamaa alikuwa anahisi mke wake ana mwanaume mwingine.
Na pia ana process talaka.

Kwahiyo vyote hivi Mwanaume ameshindwa kuvivumilia. Akaamua wakose wote.
 
Kwamba niache mali zangu nilizozihangaikia miaka yote kisha nikawe mpangaji tena kwenye gheto kama Genz?hilo haliingii akilini aisee
Kwani hizo mali ulihangaika peke yako? Imagine huyo mwanamke inaonekana wana watoto wanne!!! Hivi katika maisha hadi mnapata watoto wanne ni miaka mingapi hapo imepita???!!!!

Kwa hesabu za harakaharaka siyo chini ya miaka 10!!! Mke alikuwa anafanya kazi. Ni mambo mangapi mke kachangia katika ukuaji wa hiyo familia?

Inasemekana hapo Bunju wamehamia hata mwaka haujamalizika which means that hiyo nyumba imejengwa wakiwa ndani ya ndoa. Sasa kwa nini wachangiaji wengi humu mnaona kuwa hizo mali zilizopatikana ni haki ya huyo mwanaume tu??? Wanaume acheni ubinafsi.
 
Mbona huzungumzii sehemu inayosema kuwa huyo mwanaume naye hakuwepo nyumbani kwa muda wa miezi miwili? Alikuwa hajui pia watoto wanaishije. Why lawama ni kwa mwanamke tu? Men acheni ubinafsi na kujiona nyie ni malaika.
 
Sioni justification yoyote ya kumuua huyo Dada.
 
Kwa hiyo tulijenga nyumba ili tugawane au ili kujenga familia?
 
Tatizo unyanyasaji bro
Halafu wao wanaona sawa tu!!! Eti mwanamke naye ni mali ya mwanaume!!!! Mimi ndiyo sababu huwa napinga sana kuhusu mwanamke kutolewa mahari!! Wanaume wanaona ni kama ANAMNUNUA Mwanamke kwa hiyo anakuwa ni sawa na ng'ombe, mbuzi, gari na kitu chochote mwanaume anachomiliki!!! Ataku-treat the way he likes!!!! Shit!!!!!!
 
Tena nyumba ndogo ziwe zaidi ya mbili.... As long as uwe na uwezo wa kuzihudumia vzuri,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…