Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

Mume wa mwimbaji Injili adaiwa kumbaka shemejiye

Hivi kwanini Flora ulienda kuishi guest/ lodge??? Alikosa kabisa mahali pengine ambapo ni salama??
 
"Tatizo linakuwa kubwa kwa sababu yeye mwenyewe haonekani na taarifa ni kwamba amekimbia," alidai Flora. "Sasa kama kweli hajafanya kitendo hicho, kwa nini anajificha? Ajitokeze... aende polisi na huko ndiko akatoe maelezo yake. Kuzungumza na vyombo vya habari haisaidii kabisa."




porojo kibao kwa nini haendi polisi uku akiwa na muda wa kuongea na mwandishi? haya majangiri yanayojificha nyumma ya injili yamulikwe.

mimi sijui nani hasa anasema ukweli lakini namwelewa yeye kujificha, mtu asije akakutuhumu ukakakimbilia kule eti huna hatia, baadhi (wengi) ya polisi wetu wamegeuza "lock up" kitega uchumi kwani ukifika watakuweka ndani na kama hakuna mtu wa kukuangaikia (kuwaonga) utateseka sana. Pale ni sehemu ambayo kuingia ni BURE lakini kutoka lazima ulipe tuu.

Kuna jamaa yangu alibambikiwa kesi eti kaharibu mali, basi akashauriwa yeye akasema mimi naenda sina hatia basi akatiwa ndani kituo cha kwa Yusuph na dana dana kibao, watu wa kumdhamini wapo lakini wapi, eti lazima dhamana itolewe na mkuu wa kituo ambaye alikuwa eti kwenye msafara, halafu eti wanafunga saa kumi jioni, hadi kesho yake, hiyo ilikuwa kuanzia saa nne kama si ndugu zake kutumia mamlaka ya juu pasinge tosha kwani alitoka kumi na moja jioni.

Pia kwa wenye magari, ukikwaruzana (ukigongana) na gari la mtu mwingine mkaamua kwenda mbele, "Be prepared for the worst". Jamaa wanakutia ndani hivi hivi (kama hautakuwa tayari kushirikiana nao!) na unaweza ukalala ndani hivi hivi hasa kituo cha oysterbay.
 
Mtamsafisha lakini hatasafishika ng'oooooooooo!AIBU YA YAO AIBU YA EMMA?AIBU YAO WENYEWEEEEEEE,FLORA MA MZINZI MWENZIE!NA TUNAMTAKA BOLD WETU!
 
Hizo Ndio ndoa....na hio ni robo tu, ndoa zinahitaji uvumilivu mkubwa sana sana Yaani mkikatiza miaka mitano ni kumshukuru MUNGU
 
Sustain your arguments so that we can believe that your concerns has been proven beyond reasonable doubt . na hayo tu , vinginevyo itakuwa ni mipasho kama ile ya Mh. kapuya....si unakumbuka???
 
Haha nyie mnaangalia na kuhukumu kwa ukomo wa akili zenu hamjui wanaishije wala walikutanaje hadi kufikia hapo kwahiyo mambo ya ndoa yao wanayajua wao wenyewe acheni kukurupuka kwa kujifanya mnaifahamu sana ndoa yao, oeni na nyie ndio mtaijua ndoa ilivyo pale mtakapohukumiwa 😡
 
Kuna member mmoja anaitwa TAMKO alikuja na uzi wa kukanusha kuhusu huu mgogoro,sasa akisoma hii habari sijui atasemaje.
 
Last edited by a moderator:
Usikimbilie kuwa judgemental kwa kusikiliza upande mmoja wa shiling. Hili suala ni pana kuliko unavyofikiria
Tokea habari iandikwe magazetini kwa mara ya kwanza alikuwa kukanusha? kama ni msafi kwa nini ajifiche muda wote huo?

Halafu kwa taarifa yako tu, tunafuatilia mambo yanayotokea nchi hii kwa ukaribu na tuna kumbukumbu pia. Ni huyo huyo Emmanuel Mbasha unayemtetea kwa kivuli cha utumishi wa Mungu, miaka kadhaa nyuma kabla ya kifo cha Moses Kulola, Mbasha huyo huyo aliwahi kumpiga mtu nyuma ya jukwaa kisa kupewa muda chache wa kuimba mkutanoni... alipigwa marufuku kuimba kwenye mikutano ya injili...

Ilisuluhishwa kiutu uzima na sakati kuisha kimya kimya...
 
Wiki Hili mitandao, magazeti, na majukwaa ya watu wasio na KaZi wanaoishi Kwa kushiba majungu na umbea hasa inshu za Ndani ya nguo, wameshibishwa Bonge la Uongo unaohusiana na mambo ya kubaka hasa wakituhumu mume wa Mwimbaji huyu mashuhuri Flora Mbasha.

Wakiwa wenye Furaha Flora Mbasha na Mumewe wameonekana wakiimba Ndani ya Kanisa la Ufufuo na Uzima Kwa Firaha wakigongana Kwa staili ile Yao maarufu. Baadhi ya watu tulipigwa mshangao na shutuma kali kabisa juu Yao. Na bila kupoteza Muda Mara Baada ya Ibaada tuliwakimbilia Kujua kulikoni na kuwakuta wakicheka HATA huyo mbakwa mwenyewe yupo ana furaha zake. Tulipohoji kulikoni wakatuambia HATA Uvumi usio na ukweli juu ya mzee wa liliondo uliwafanya HATA viongozi wa Nchi kutimkia huko wakiamini kubugia kikombe Cha maji machafu yasoyochemshwa eti kutawaponya ukimwi, Nchi Hii maarufu ambayo Siasa na matukio ya uvumi Ndiyo yanayopewa kipaumbele na kuongoza jamii kubwa ya wajinga.

Hadi naondoka Kwenye viwanja hivi najiuliza maswali mengi bila majibu, Nani katengeneza Uvumi huu na Kwa nini?!?. Kama Ni Flora na Mumewe ili iweje au Ni Gia ya kuwapaisha Kwenye chati tena manake ukitaka Kuwa maarufu Kwenye Nchi ya wajinga jisingizie mambo ya chupini lazima utakamata Akili Za maelfu ya wajivuni. Kama ni Adui wa Flora WHY?!? ..

Nikajikuta najiapiza kutofuatilia ujinga na upuuzi Kama huu tena. Bora nifanye KaZi Kwa bidii kuifanya familia yangu iende Chooni sio kung'ang'ana na UZUSHI naonekana kuku tu..

RIP mama Zitto Kabwe..tuko pamoja na Wewe Kamanda Zitto..

Flora Mbasha na timu yake wakiimba kwa furaha Ufufuo na Uzima na kutuzwa maelfu ya fedha na washirika. kilikuwa kipande kikubwa cha furaha watu kumtuza zaidi ya box zima la spika limejaa fedha.

Hawa watu wa makanisa ya kijasiriamali huwa ni waongo sana !!!!

Sijui huya TAMKO anadanganya kwa faida ya nani.

Hebu someni hapa

Mumewe Flora Mbasha ajitokeza, afichua siri - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Kwa maendeleo na ustawi wa taifa hili naomba Invisible uweke-pause hii thread ili watu tufanyekazi asubuhi hii then uta resume saa kumi na moja jioni, tafadhali mod tuonee huruma wenzio tutashindwa kufanyakazi kabisa kwa kufatilia taarifa hii huku tukizid kuhoji usalama wa The bold
CC: masai dada TATIANA J.lee tweenty4seven Heaven on Earth
WAONE WALIVYONUNA

Cc Active, Moderator, Mhariri

kazi haziendi hapa............ nashika mafile kidogo the huyo nazama ndani

nikimuona The bold ndio roho yangu itatulia sa hivi hapana
 
Last edited by a moderator:
naomba ufafanuzi zaid juu ya uhusiano uliopo kati ya flora na Gwanjima

Nisije nikasutwa sijasema uhusiano wa kimapenzi...

Uhusiano ni Gwajima kumhamishia Flora GEST, kumpa cheo kikubwa kanisani, kumpeleka chuoni Uingereza na kumtembelea mara kwa mara, kuzunguka naye kwenye mikutano nchi nzima. Yote hayo AMESAIDIA huku mumewe Flora amebaki nyumbani.
 
Back
Top Bottom