Mume wa rafiki yangu anatarajia kuoa mke wa tatu wiki ijayo, rafiki yangu hana raha na ndoa yake

Mume wa rafiki yangu anatarajia kuoa mke wa tatu wiki ijayo, rafiki yangu hana raha na ndoa yake

Unique Flower

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2019
Posts
12,838
Reaction score
25,282
1621323863561.png
Wajameni kati ya kitu ninachoogopa ni kubadili dini niwe muislamu. Na ndoa yao imefunguliwa. Ipo kirahisi sana. Unaolewa leo kwa gharama kubwa akimaliza haja zake anakupa talaka tatu.

Hapo mashosti wanakucheka umeachwa unashangaa. Juzi nilienda kwa shosti yangu kaolewa huu ni mwaka wapili mie nikazani anaraha . Kumbe nikaraha huyo mwanamme alimsilimisha akawa muislamu. Halafu akapata watoto naye .

Baada yakupata watoto wakike hao ni mapacha. Akanza vitimbi akaoa bila ya ridhaa yake. Akamleta mke wa pili sasa wapo wawili . Huu ni mwaka watatu yupo humo ndani kwenye chumba chake. Sasa huyu baba anaoa tena wiki ijayo na atamleta mke ndani.

Hivi shida huwa nini?
Niambieni jamani?
Akaanza vitimbi
 
Unaolewa leo kwa gharama kubwa akimaliza haja zake anakupa talaka tatu.
Kama ni vitimbi kwenye ndoa... hakuna cha ndoa ya Kiislamu, Kikristo wala Kiyunani!! Sasa mambo yakiwa kitimtim namna hiyo si bura kila mtu ashike hamsini zake kuliko mnaishi nyumba moja wakati hakuna amani?!!

Anyway, hizo taraka zinatolewa ndivyo sivyo lakini msingi wake, ni kuepusha shari baina ya wanandoa, isjie mkafikia hadi kuuana au kudhuriana! Na hadithi inasema wazi kwamba "...talaka ni ruhusa inayochukiza"!

Ni kutokana na hilo, ndo maana mafundisho yanasema, mwanaume ukiona ndoa haivumiliki, basi toa taraka moja; na kama nyumba ni kubwa basi gawaneni upande labda hadi kwisha eda, suluhu kati yenu itakuwa imeshapatikana!!!!

Na lau kama nyumba ni ndogo, basi mwanaume toa taraka kisha mwache ex wako kwenye hiyo nyumba, huenda baada ya muda akili zitakurudia na kuamua kumrejea mke wako!!
 
Braza hili ni jukwaa letu sisi vijana, ninyi wazee kwenu ni kule juu!
🤣 😅 🤣 🤣 🤣 🤣 😅😀

Mi nilikuwa naku-zoom tu kule mnakofanya kama MATAGA wanaolazimisha kuilindi legacy ya Magu huku nanyi mkituletea simulizi za Orlando Pirates na Yanga wakati mechi zenyewe ni za tangu enzi Mwalimu akiwa bado "check bob" flani hivi!!
 
Mimi ni mkristo ila katika suala naliunga mkono ni kuoa wake wanne,ina maana yake aisee..suala la talaka naliunga mkono pia..hivi imagine kuna watu wamefunga ndoa za kikristo lakini wana ugomvi usiokoma,mke na mme wanalala vyumba viwili tofauti kwa zaidi ya miaka miwili..hakuna tendo la ndoa wala maelewano tena..wanaishi kwa kuviziana sasa si bora kupeana talaka?

Pia suala la kuoa wake wanne nalo lina umuhimu wake,wanaume tumependelewa sana imagine hatuingii P kama wanawake,hatubebi mimba,hatuzai kama wenzetu..sasa ukiwa na mke mmoja kipindi anapitia hayo unafanyaje?mtu akijifungua unashauriwa uache angalau miezi 6,je katika hali ya kawaida inawezekana kweli kwa mtu aliyezoea kufanya mara kwa mara?si ndo chanzo cha usaliti!!ni bora ukiwa na wake wanne unahamia tu..huyu akiwa P unaenda kwa mwingine..huyu akijifungua unahamishia majeshi sehemu nyingine...

Sema masuala ya dini ni magumu sana kuyajadili tuyaache kama yalivyo tu
 
Hujanielewa kwanini mnaoa leo kesho talaka halafu mnajaza wanawake nyumba moja?
 
Ukristo wa wapi?! I hope huna lengo la kuchanganya Ukristo na Wakristo!!!
Mwambie dini yetu ni mke mmoja , mme mmoja na ndio vizuri sisi sio wajinga sasa wao wanawajaza mwisho karaha bhana .
Heshima nikitu cha bure
 
Kwahiyo uko tayari mumeo aendelee kuchepuka?Akioa basi hiyo ndo heshima yenyewe sasa
 
Wajameni kati ya kitu ninachoogopa ni kubadili dini niwe muislamu.
Na ndoa yao imefunguliwa.
Ipo kirahisi sana .
Unaolewa leo kwa gharama kubwa akimaliza haja zake anakupa talaka tatu.

Hapo mashosti wanakucheka umeachwa unashangaa.
Juzi nilienda kwa shosti yangu kaolewa huu ni mwaka wapili mie nikazani anaraha .
Kumbe nikaraha huyo mwanamme alimsilimisha akawa muislamu .
Halafu akapata watoto naye .

Baada yakupata watoto wakike hao ni mapacha.
Akanza vitimbi akaoa bila ya ridhaa yake.

Akamleta mke wa pili sasa wapo wawili .
Huu ni mwaka watatu yupo humo ndani kwenye chumba chake.
Sasa huyu baba anaoa tena wiki ijayo na atamleta mke ndani.

Hivi shida huwa nini?
Niambieni jamani?
Akaanza vitimbi
Olewa huko huko uliko upate raha.
 
Back
Top Bottom