Mume wangu alizaa nje: Nimekuwa na chuki na kusababisha kuchepuka nje ya ndoa

Miaka kadhaa iliyopita mume wangu alimtambulisha mtoto wa nje katika familia yake ni wa kiume alikuwa ni mtu wa furaha sana na kujisifu kuwa kapata mtoto wa kiume na ndugu zake walimpongeza hasa mtoto alifanana nae. Japo mimi nilibaki na maumivu, kwani nimezaa nae watoto wawili wa kike tuu.
Katika maisha yangu nilipenda kuwa na mwanaume ambaye tutakuwa na watoto wetu tuu. Ila ijakuwa hivyo. Nimelipokea japo nina maumivu.

Mume wangu ni mtu wa mfumo dume niseme. Akiongea ndani ya nyumba ndo ishakuwa hivyo. Aliniambia tuu mtoto huyu ni wangu na ataishi hapa kama utaki basi waweza ondoka.
Nikasema tuu sawa, basi mtoto tunaishi nae hapa.

Tulijenga nyumba moja tulikuwa tunashirikiana kwa kila kitu kwa sababu mimi nina kazi na mume wangu pia na baadhi ya biashara. Na tulishaanza nyumba nyingine kujenga. Ila nilisimama baada ya tukio hilo lililonipa maumivu.

Nilishangaa sana mume wangu anatabia ya kusema tuu yeye hana uwoga. Anasema kuwa huyu ni mtoto wangu wa kiume ndio atarithi mali zangu kwa kuwa anaendeleza jina langu. Mimi namuangali tuu. Mtoto anapita nae mtaani kwa kujisifu hata mbele ya marafiki zake kwa kuwa mtoto kafananae. Na yeye mali zetu zipo kwa jina lake na mimi hata ushahidi kuwa nimeweka mkono sina ninabaki namuangalia tuu.

Miaka 3 iliyopita kuna kiwanja kimoja aliniachia marehemu Baba kipo kigamboni kule ni kikubwa kiasi. Na mume wangu ajui hiko kiwanja. Ni mimi tu ka ndugu zangu. Sasa nilipigania kuwa niwajengee watoto wangu nyumba pale japo mimi mama yao sina sio tajiri. Nikasema nitapambana tuu. Nilikuwa naweka vipesa vyangu baadhi na kujinyima. Hata pesa ya mume wangu ya matumizi nilikuwa naibana sana.
Biashara zetu na mume wangu nilikuwa nachota kiasi bila mume wangu kujua kabisa.

Nilianza msingi wa nyumba mbili kwenye eneo moja. Nyumba sio kubwa ni vyumba viwili tuu vya kulala, living na dining room, choo na store na jiko. Sio kubwa kivile.

Ilikuwa ngumu sana kwangu kuanza kujenga.
Sasa siku moja nilikutana na Baba mmoja mtu mzima na anamke na watoto wakubwa tuu. Nilikutananae karikoo kwenye nduka moja hivi. Tulizoeana mapaka kupanga nichepuke nae.
Mkewe kuna kipindi nikamjua mpaka nyumbani kwake. Ni Baba mwenye uwezo tuu tena sana.
Mimi ni mwanamke nina mvuto kwa hio niliamini hawezi nikataa yule Baba. Mara nyingi tulikuwa tunakutana kwenye hotel. Nilimueleza shida zangu akasema atanisaidia.

Alinisaidia kumaliza msingi mpaka boma kuisha za vijumba vyangu. Nilijitahidi sana mume wangu asijue kwani yeye namjua reaction yake endapo akijua.

Yule Baba alikuwa ananifurahia sana , ila alikuwa ananionya kuwa kuwa makini mumeo asijue kabisa. Mimi namwambia tuu usijali ni kweli nilijitahidi mume wangu asijue kabisa.
Nilikaanae miaka 2 yote hio niliendelea nae bila my hubby kujua.
Yeye yuko busy na mtoto wake maana namuangali tuu jinsi anavyomuaangaikia. Mwaka jana alinisaidia sana kuwezeka vijumba vyangu.
Ila mwishoni mwa mwaka jana aliamishwa na kwenda Dodoma kikazi na mahusiano na mimi yaliisha.
Nikiri tuu alinisaidia sana yule Baba. Kwa kiasi kikubwa.

Sasa mwaka huu nilikutana na kijana mmoja mgahawa mmoja nilimpenda, nilijitahidi nikapata tukabadilishana namba najua hawezi kunikataa coz mimi ni mzuri najiamini. Niliingia nae kwenye mahusiano. Na sijamwambia kuwa ni mke wa mtu. Japo vijana ni wagumu kutoa pesa ila anajitahidi kiasi chake. Naamini atanisaidia hata kwenye biashara zangu binafsi, coz yeye anaagiza vitu china.

Najua wanaume mnakasilishwa na usaliti kama huu, najua wapo watanitukana na maneno juu. Lkn hata nyinyi ni wasaliti kwa wake zenu, thread zenu za michepuko mnashauriana sana humu jf.

Mume wangu kanipa donda kubwa sana , tena hata aibu anasema huyu ndo mrithi wangu. Yeye ni wale wanaume akisema basi wote mtii.
Namuangali tuu na mwanae.

Sijaleta kama sifa ni matokeo ya maumivu niliyopata sikuwa na hio tabia kabisa.
Mwenye kuleta povu na alete tuu.
GentleMen rule no 2: Never go back to the woman who cheated.
 
Si uliambiwa kama huwezi kuvumilia utoke,sasa kwanini uendelee kuwa kinga'ng'anizi na kuchafua nyumba ya watu kwa umalaya?
 
Kwahiyo nawewe unajitahidi ili umletee wakwako wakiume au we lengo lako nikumalizia nyumba tu wanao wapate urithi!?,

Ila huandai urithi tu lakin pia unajiandalia na sehem yakufikia maana najua ipo siku tu utajikanyaga na atajua.. mzee wa mfumo dume atakutimua alafu hapo atakuja huyo mzaa vidume maana ameshajua shimo linatoa vidume tayari atalitaka alisogeze kabisa liwe ndani..

We endelea na kutafuta vijana wakusaidie kumalizia nyumba.

Alafu we nimpambanaji dada angu mtu akikuvutia tu unajivunia mvuto wako kumuingiza kwenye 18 zako aiseee!
 
Wewe ni mzinzi kiasili hata asingekuwepo huyo mtoto.
Kwani sheria za mirathi uzijui hadi uteseke na kauli za mme wako.
Huyo ni kaka Yao na hao ni dada zake Wana unganishwa na damu.
 
Na hio nyumba unayoijenga ipo siku atajua tu hakuna Siri Duniani,jiandae kwa hilo
 
Msipende kuhalalisha dhambi kupitia dhambi,haya maisha relax kwani nani anajua yupi atatangulia.
Mtoto wa nje anaweza akawa na akili kuliko hata watoto wa ndani na akaja kuokoa na kuisimamia familia familia,mifano ni mingi.
 
""Sijaleta kama sifa ni matokeo ya maumivu niliyopata sikuwa na hio tabia kabisa.""

Nimekuelewa sanaa madam.
Pole sanaaa.

#YNWA
 
Hujui unachotafuta,umemsaliti mumeo kwa kumegwa na mume wa mwanamke mwenzio,kilicho kuumiza kwa mumeo na wewe ukawa tayari kumfanyia mwanamke mwenzio na akose amani aanze kumegwa na mume wa mwingine tena,na mkija tunawamega kweli,HAPA MWENYE MAKOSA NI WEWE UNAETAMANISHA WANAUME WAKUTONGOZE NA AKILINI UNAWAZA PESA,HUNA TOFAUTI NA SLAY QUEENS/GOLD DIGGER,MAKAHABA WENYE IPHONE..
Huu ni ukweli mchungu
 
Mme wako anajua kua umekuja kuumiza wanaume humu? Kama una lengo la kuumiza wanaume ambao siyo huyo Mume wako utakua hujafanya Jambo lolote la maana.
 
Unaadhibu dhambi kwa kufanya dhambi? Omba rehema kwa Mungu unafanya dhambi ya uasherati kwa kisingizio cha kuletewa mtoto wa nje. Hapo kwa haraka umetenda dhambi ya chuki Kwa mtoto na baba yake, umelipa kisasi na bado unazini na bado una hasira. Tubu Mungu ni mwenye rehema usishupaze shingo bado Mungu anakupenda sana.
 
pole sana mkuu kwa yaliyo kupata,lakini kabla ya yote jiulize kuchepuka kulipiza kisasi kuna faida gani kwako,tangu umechepuka umepata nini? maana jamaa hajui na haumii,nitoshe kusema tu wewe ulikuwa na roho ya kuchepuka tu sema ulikosa sababu tu,nikuulize tu kama umeibiwa vitu unaweza lipiza kwa kuibia wengine kama huna roho hiyo ya wizi? angalia dada angu usije waacha watoto ya tima kwa uzembe wako maana kwatabia uliyo anzisha matokeo yake nikupeleka ukimwi nyumbani.katika kuchepuka kwako ushapata mtoto wakiume? mali hizo ni mali yako na mume wako kwanini ujiumize? anafanya hivyo kumtambulisha huyo dogo ili ufanye uwezavyo ili nawewe upate mtoto wa kiume.angalizo chepuka ila jamaa lazima atajua tu.na huyo dogo angalia usije ukamuthuru maana shaona shetani ashakamata ufahamu wako.kuzaa utazaa tu mtoto wa kiume halaka ya nini kama unatambulika we ni mke halali wa jamaa?.jamaa akijua ndo kwisha habari yako. n.b ,mtangulize mungu kwa mapito unayopitia
 
Hahahaha Wanawake wanaojionaga wazuri hahaha wanakuaga Wajinga sana kwakweli !!

Wengi wa Wanawake wazuri hawaolewi, wakiolewa ,ujue mwanaume ana Moyo wa uvumilivu sana.

Simnaona Kila Aya anasema "Coz najiamin mie mzuri "😂😂😂
Huyo hamna kitu na Hana uzuri wowote ni rapurapu(nguo isiyo na ubora au hadhi au thamani sawa na nguo nyingine yenye kufanana nayo)
 
Back
Top Bottom