Mume wangu anatembea na house girl wa jirani

Mume wangu anatembea na house girl wa jirani

Jamani mwenzenu mume wangu ananiambia nina husuda, hii ni nini? Kisa tu nimegundua anatembea na house girl wa jirani

Kutembea na Beki 3 sio dhambi!! Dhambi wakivunja amri ya 6! "UMEGUNDUA" hapo kwenye red...fafanua zaidi.....!!
 
Jamani mwenzenu mume wangu ananiambia nina husuda, hii ni nini? Kisa tu nimegundua anatembea na house girl wa jirani
Ulitakiwa ujiulize huyo housegirl wa jirani kakuzidi nini mpaka mumeo ahamishie majeshi huko?
 
Sasa kumbe anatembea kumsindikiza labda dukani/sokoni tu mbona hakuna ubaya wowote pengine huyo house girl alimuomba amuonyeshe njia.
 
Jamani mwenzenu mume wangu ananiambia nina husuda, hii ni nini? Kisa tu nimegundua anatembea na house girl wa jirani

ila giLESi ndoa si ilifanyika april,'13 au haikufanyika tena! mbona changa sana! au ndio hivyo tena!
 
Last edited by a moderator:
Hivi inapita siku hapa bila uzi wa mume wangu anatembea na mwanamke mwingine?!!!
Wanawake mbadilike jamani...
 
Acha unyanyapaa.
Sema mumeo anatembea na mwanamke mwingine.
Kwani huyo mwanamke angekuwa banker, lawyer, doctor, .....ungepostije?
Tatizo lake anamdharau huyo binti kwa kuwa eti ni housegirl wakati mumewe akifika kwa huyo binti anapumua kama vile kawekwa kwenye VENTILATOR.
 
Badilisheni mtaa mhamie mitaa mingine huo uhusiano utaisha
 
..Mimi nilikuwa na Mume wa mtu ananizoea zoea kwa vocha, Mpesa na lift. Nikastukia tu siku Mtu ananipigia! Mimi Mama S, Mke wa flani? Nikasema tume toba yarabiiiiii! Nachanwa na viwembe! Nikajikaza kumuuliza nikusaidie nini Mama? Nakusalimia tu Mwanangu! Wala usiwe na shaka! Mmmmmh! Nikasema anaitumishia Jini kwenye simu nini? Nikamwambia haya nashukuru (Mwenyewe kauzu zaidi ya dagaa) Hivo hivo kila siku asubuhi na jioni! Ananiambia watoto wametoka shule salama, leo tumekula mchicha tu, mara tumekula maharage, Mara nashukuru mwanangu leo tumeachiwa hela ya nyama! Mwisho yakanifika kooni, Nikamtukana tukana yule jibaba sikumwambia kama ni simu ya mkewe ndo imenitisha! Mwanamke ana gubu kanifanya mpaka dhamira inisute! Khaaaaaaaaaa!
lara 1 , you have made my day!
 
Last edited by a moderator:
haya Lara1,soma limeeleweka!

We ulimuuliza wanini? Mambo ya sasa ukijua Mumeo ana nyumba ndogo wala humcomfront, coz there is no way aka confess, na kutubu au kujuta! Sana sana ata eliminate all the evidence na kukugeuzia kibao cha kutokuwa na imani nae. Kama hivo anavokufanyia. Hio yote ni kupoteza maboya tu na kusanua soo liishe.

Ukipata ushahidi dnt panic, we withhold evidence na kuzidi kuiaccumulate mpaka itoshe kumconvict directly. Unakuwa na defence ya kontena kama chelsea ili asipate upenyo wa kuchomokea.

Na sio taarifa ya mashtaka unamsomea wewe, afu hakimu wewe tena! Atakuomba msamaha uwongo na kweli afu haina maana, resources zote zimepotea na mda.Taarifa anaipata kwa Nyumba ndogo a.k.a mgoni wako kuwa huku hali si shwari mkeo kaja kama bomu la B52 lenye Uranium na Nuclear kwa mpigo! Akirudi huku wewe wamchekea tu kama sio wewe! Lazima ahisi wataka kumpoison kama sio kumkaba na mto usiku!

Akijikosha unamwambia nani kakuuliza baba? Wala usinichoshe! Mwenzio keshapata full dose na kapona ugonjwa wake wa umala.ya bado wewe sasa dawa yako inachemka!

Nyumba ndogo za siku hizi sugu kuliko hata Mr. 2 mwenyewe! Ukijifanya mstaarabu atambeba jumla jumla! Nenda pale anzisha kumsuta kistaarabu na kumchimba biti, akijibu fyoko tu anzisha varangati afu wahi kushtaki polisi umefanyiwa fujo na kamuweke yule Beki tatu ndani wiki 2, afu mwambie ampigie mumeo akamtoe kama anampenda! Mumeo ilitakiwa apate taarifa apewe na Beki tatu akiwa ndani. Ndo ajue wewe sio mwepesi!

Mimi nilikuwa na Mume wa mtu ananizoea zoea kwa vocha, Mpesa na lift. Nikastukia tu siku Mtu ananipigia! Mimi Mama S, Mke wa flani? Nikasema tume toba yarabiiiiii! Nachanwa na viwembe! Nikajikaza kumuuliza nikusaidie nini Mama? Nakusalimia tu Mwanangu! Wala usiwe na shaka! Mmmmmh! Nikasema anaitumishia Jini kwenye simu nini? Nikamwambia haya nashukuru (Mwenyewe kauzu zaidi ya dagaa) Hivo hivo kila siku asubuhi na jioni! Ananiambia watoto wametoka shule salama, leo tumekula mchicha tu, mara tumekula maharage, Mara nashukuru mwanangu leo tumeachiwa hela ya nyama! Mwisho yakanifika kooni, Nikamtukana tukana yule jibaba sikumwambia kama ni simu ya mkewe ndo imenitisha! Mwanamke ana gubu kanifanya mpaka dhamira inisute! Khaaaaaaaaaa!
 
lara 1 kiukweli huwa sikupatii mfano kwa michango yako ktk jamvi hili la MMU!

Keep it up
 
Last edited by a moderator:
Huyo beki 3 anakuzidi nini
Unashindwaje kumhamisha mjini badala yake unalalamika lol!
 
Huyo mmeo anakuheshimu sana. Sijui unalalamika nini. Assume kule anapewa tgo, je angekuomba ungempa au ungeitisha vikao!?

ungekuwa hapa karibu yangu ningekupa bonge la fyoooooooonzo ila sijui linaandikwaje. Kwanza ndo mana jina lako Jambazi
 
Back
Top Bottom