Mume wangu hapendi ndugu zangu

Huyo mdogo wako alifikaje fikaje hapo kwako? Mlikaa na mumeo mkakubaliana au alifika kwa kulazimisha wewe?
 
Chagua moja hapo kati ya kumtoa ndugu au mume 7bu hakuna uwezekano wa hayo mawili kwa wakat mmoja
 
Bora wewe, Mie huyu Baba Kidogoli anafukuza hadi ndugu zake, hapa nilipo upande wa mume wanaona Mimi ndo nina roho mbaya, kumbe ndugu yao hana uvumilivu WA kuishi na ndugu....Yani ndugu akizingua asubuhi anakatiwa tiketi, hata Kama anasoma uhamisho utamkuta huko huko.
Nishamzoe mwenyewe, la msingi nguvu za kiume anazo, kibo na mawenzi ananifikisha wala sigombani nae, tabia zake apambane nazo mwenyewe.
 
NDOA NI YA WATU WAWILI TU.MAMBO YA KULETA SIJUI MDOGO WANGU,KAKA YANGU NA BLAABLAA NYINGINE NIKUJITAFUTIA MIGOGORO WEWE MWENYEWE.

Marko 10:6-9
6Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke. 7Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; 8na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. 9Basi alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe.
 
Pole sana kwa changamoto hiyo ya kifamilia, atakuwa mchawi huyo
 
Afu pia ikiwa huoni sababu jua kabisa huyo mumeo kashaomba tunda ila amechomolewa japo hulikubali hili ila ndo chanzo na usitegemee kama huyo ndugu yako atakuja kukuambia mana atahisi atawagombanisha ww hatakam mpelelezi vp ila jua hao ni watu wazima hasa kwenye ishu za kutongozana unaweza kukaa hata mwaka bila kujua kwahy hakuna sababu nyingne hapo
 
Nina hisia huyo mwanaume anampenda kimapenzi mdogo wako... hii naongelea kwa experience,kuna shemeji yangu alikua na tabia kama hizo nilivyomaliza form six nilienda kwa dada yangu kuwapa hi .shem akawa ni mtu wa kununa nuna tuu kugomba gomba hovyo, mara nikiongea na simu anamwambia sister aniangalie nimeshaanza anza mambo ya wanaume..nikitoka kdg hata kwenda dukani anamwambia sisy huyu mdg wako asije kutuletea mimba humu na mengine mengiii wkt mi mwenyewe enzi hizo namaliza six wala hata sijaanza matusi 😀 . Basi bwana sisy alikuja kusafiri alienda msibani akatuacha hapo na wtt wake na msichana wa kazi si ndo bwa shemeji kunambia live kuwa ananipenda sana na vile kunimind mind ni kwa sbb anaona wivu mara anashindwa kuvumilia so nimtunuku. Aisee siku hyo alijuta kunambia nilimuogesha matusi yote na nikamwambia naenda kusema na kutangaza kwa ndugu. Na kesho yake nikasepa nikamwambia sisy nawahi kuaaply tempo mahali. So my dear usikaze shingo kusema mumeo hawezi fanya hivyo... mwanaume ni mwanaume tuu dont under estimate him.
 

Ila tusihukumu upande mmoja, ukute shosti Hampi mume attention, attention anampa mdogo wake....ukizingatia hawana mtoto, unaweza kukuta muda wa kutafuta mtoto yeye yuko chumbani Kwa mdogo wake wanapiga Stori za utotoni.....wakati wa Kula ukute badala ya kumlisha mumewe yeye anataka ale jikoni na mdogo wake, mume lazima ajione ametengwa na atamchukia huyo mdogo mtu Kwa kuona anaingilia mahaba.
 
Hakuna cha gubu wala nini.Ndugu ni kikwazo cha ndoa kwa namna yoyote ile.
Mimi kwangu najihitaji mimi mwenyewe,mke wangu na wanangu basi,ndugu wapite tu kusalimia na kusepa.Wakiwa na na shida ya pesa waseme niwape.Kifupi nyumbani kwangu ninahitaji uhuru wa hata kumtukana mke wangu,kumfokea,kumkumbatia any time,kumgegeda popote pale ndani ya nyumba yangu.Na ndiyo maana watoto nimepeleka boarding huko.
 
Kwa nini hamna mtoto mpaka sasa? There's possibly something wrong with your husband fertility and thus loosing his self confidence and hence resorts to intimidating.
 
Ndiyo mwanaume wa kweli alivyo.Tunahita uhuru tukiwa majumbani mwetu.
 
Duh.

Mwamba atakuwa aliteseka sana kisaikolojia.

Iliishaje hii?
Nilivyoondoka nikaenda home mambo ya chuo yakaja nikasoma nikamaliza nikaolewa. So huyu ni moja ya mashemeji wanaoniheshimu sana maana sijawahi mwambia mtu yoyote siri yake. Na sikutaka kuvunja au kutoa amani ya ndoa yao.
 
Me nakushauri mrudishe dogo kwanza home. Halafu jipe muda wa kukaa na mwenzako kujua shida ipo wapi.

Hapo ni kwake kama hataki kukaa na ndugu jitahidi ujue sababu ni ipi kwa utaratibu na umakini usijegombana nae.

The way umeandika ni kama unamuelewa zaidi mdogo wako kuliko mume wako. Nadhani ni busara kujali hisia za mwenzako zaidi na kujua anasumbuliwa na nini. Mdogo wako na yeye ataolewa atakuwa na mji wake, je utaenda kukaa nae huko au utabaki kwako?!

Sasa mbona unahangaika na mambo ambayo si lazima. Kumjali mdogo wako kama mwanao inauhusianaje hapo. Mbona kama unalazimisha kuwa mama kwa mdogo wako na ana mama yake ? Sasa umemuacha mama yako anakaa na nani we unachukua mdogo wako unaishi nae?!

Inaonyesha hauna mtoto bado. Kwann usitafute watoto ili uwe busy nao na kuwapenda na kuwapa hiyo attention?!


Mdogo wako atabakia kuwa mdogo wako na atatakiwa kuwa na kwake siku moja, msaidie kujiandaa na maisha yake ila sio kumkumbatia kama kinda as if ni mtoto wako.
 
Na anamuamini sana mume wake kuwa hawezi mtongoza mdogo wake.
 
Na anamuamini sana mume wake kuwa hawezi mtongoza mdogo wake.
Aaaah mambo mengine ni kuibua changamoto zisizo na ulazima. Ukishaolewa mtu pambana na kujenga familia yako. Ndugu na familia yako wasaidie kwa makubaliano na mwenzako au kwa namna ambayo haita athiri mahusiano yenu.

Kuna familia ni stress na zipo dysfunctional. Umetoka huko unaanza kuvuta tena changamoto hizo kwenye ndoa yako. Ishi na ufocus na ndoa yako. Ndio maana mahusiano haya dumu siku hizi sababu unakuta mtu analazimishia ndugu zake kuwa part ya familia mpya na hajakaa na mwenzake wakapanga lolote. Sasa kwann uliolewa au kuoa si ungebakia kwenu muishi milele.
 
Nashukuru sana. Mtoto akija anafanya vishughuli vidogo vya nyumbani then anaingia kulala. Kukaa sebleni ni hadi mimi ni lazimishe
Ila kuna mdau anasema kwa ushuhuda na umemtokea yeye akiwa kwa Shem

Shem mkali kujionyesha kumbe ni wivu na anamtamani ( mdogo mtu)

Angalia pande zote pia hamu ina Vishawishi vingi sana mchunguze mmeo au mwondoe mdogo wako hapo

Huo ni ushauri tu kwani kila kitu linawezekana chini ya Jua

Dunia hii haijaanza leo na machafu ni mengi ila yanatofautiana
Pole sana ila natumaini umepata picha kubwa hapa kwa wadau

Usikurupuke bali uwe mwangalifu pia
Dua zangu
 
Unaolewa na mtu wa kijijini ndiyo shida hapo. Wanakuwa na ushamba mwingi sana. Vumilia, yakizidi mueleze mdogo wako hali halisi na mwambie akaze roho. Walau akijua hapendwi atajua namna ya kuishi.
 
Kibongo bongo hilo ni swala ambalo familia nyingi kama imekua kawaid na kuna koo au makabila fulani kukaa na ndugu ni kama lazima hivi. So ili kuepusha matatizo ni vyema iwe kuja na kusalimia kidg na kusepa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…