Mume wangu hapendi ndugu zangu

Sasa huyo ndo Mwanaume sasa hana mbambamba siyo mnafiki.
 
Asante kwa ushauri. Nishamwambia mara nyingi niambie
Kama nimfukuze basi ili nijue maana naona kila anachofanya ni kero. Hata mimi naumia unavosikitika najiona mimi ndo tatizo. Hajibu
Please usiwatenge ndugu zako sababu ya mume. Wanaume sisi hatutabiriki na sometimes tuna ujinga ujinga wetu wa kiume ( kuna nyapu nyingi nk nk)! Siku majanga yakikupata the only people watakaolia na wewe bila unafki ni ndugu zako wa kuzaliwa nao. So usithubutu kuwatenga kisa mume wako au unau-sugarcoat ubinafsi/ mapungufu yake!
 
Wanawake bwana yaani kweli karne hii una muamini mwanaume kwa kumletea mdogo wako pisi kali nyumbani kwenu....aisee lazima nipite nae tuu.
Tatizo anamuamini sana mume wake as if ni malaika (hana tamaa).

Kukaribisha mwanamke aliepevuka nyumbani kwako ni hatari kwa hizi ndoa za vijana.
 
Bado haitosaidia kwakuwa ww utafanya kwa lengo la kumuonesha mumeo ila mumeo hafany kwa lengo la kukuonesha ww kwani anajua kitu anafanya
 
Hii ndo comment pekee inayoshauri hivi. Yani najiuliza wangapi wamefukuza ndugu zao kwasababu ya penzi? Siku mume akikengeuka mimi ntakua mgeni wa nani
 
Akapange au akae hostel mambo ya kurundikana kwa shemeji sio mpango
 
Pole sana...kiufupi mume wako ni mchoyo ile kabisakabisa. Na hii ni mbaya sana kuwa na mwenza mchoyo maana ni tabia iliojengeka tangu akiwa mdogo..na wengi wanakua ni watu waliokulia vijijini kwenye aina fulani ya umaskini (simaanishi wote walokulia kijijini wanatabia hizo). Hii hali ilimtokeaga mdogo wangu wa kike ni lecturer,mme wake akaanzaga hizo mambo na nnadhani alidhani sisi ni maskini...baadae alizima fegi mwenyewe na huwa anajubaraguza sana maana anatamani ifutike kabisa kwenye kumbukumbu zetu. Na hii huwa ni common mwanzoni mwanzoni mwa ndoa within 3 years
 
Hii ndo comment pekee inayoshauri hivi. Yani najiuliza wangapi wamefukuza ndugu zao kwasababu ya penzi? Siku mume akikengeuka mimi ntakua mgeni wa nani
dada umekuja kuomba ushauri au kutafuta mtu wa kuside na wewe?trust me there is something and you need to think beyond
 
Dah ni mtihani.
 
Dah ni mtihani.
Mwambie nawewe unaanza kuwakazia ndugu zake,japo sidhani kama itasaidia na ukizingatia si tabia yako. Kiufupi ni tabia za baadhi ya watu walokulia maisha duni afu akapata unafuu ukubwani..na pia wanakuaga na ushamba mwingi
 
Hii ndo comment pekee inayoshauri hivi. Yani najiuliza wangapi wamefukuza ndugu zao kwasababu ya penzi? Siku mume akikengeuka mimi ntakua mgeni wa nani
Dada, fanya hata vibiashara ili uondokane na hii low self esteem.
Yaan kumbe unahofia ukija fukuzwa,hakuna atakaye kupokea kwenu kwa kuwa hukuishi nao? Huoni kama huo ni wajibu wao kukupokea kwa kuwa ni ndugu yao wa damu..lakini mumeo siyo ndugu yao.
So chagua ndoa ama ndugu zako.
 
Mwambie nawewe unaanza kuwakazia ndugu zake,japo sidhani kama itasaidia na ukizingatia si tabia yako. Kiufupi ni tabia za baadhi ya watu walokulia maisha duni afu akapata unafuu ukubwani..na pia wanakuaga na ushamba mwingi
Hivi nnavokwambia ndugu yake yuko hapa, af vile vyote ambavyo mdogo wangu alikua anakatazwa kufanya, wa kwake anafanya. Hivi unaambiwa vumilia ndoa kwa mke kuhudumia ndugu tena ambae sio wa damu kabisa tena kwa upendo ila wa kwako ananyanyaswa. Wanawake tuna kazi
 
Pole sana aisee... Usikubali kuumia kwa kinyongo. It's either usichoke kumchana hadi aache, or nawewe ufanye waziwazi kwa ndugu zake kwa makusudi ili afeel the same. Na uache kuwachangamkia ndugu zake tena na ajue wazi
 
Dah. Tutafika tu Mungu atupe mioyo
 
Kuna uzi fulani mwamba anacomplain mdogo wa mke wake anadharau sana,anamjibu anavotaka na anamuambia ni bora wagawane mali na dadaake waachane,ni kama dada huwa anamsimulia mapungufu ya mwamba kwa mdogo wake..pia mwamba alikuwa hashirikishwi ujio wa baba mkwe,anashtukia tu anapewa taarifa baba mkwe anakuja maana alikwisha tumiwa na nauli kbs

Nakonekti doti tu jameni[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Katika vitu sivipendi katika maisha yangu ni kuishi nyumba moja na ndugu wa pande zote wangu au mke wangu hata wawe wazazi, waje kusalimia siku 2 wasepe kuishi kwa kweli hapana labda kwa jambo maalum
Ishawahi tokea nilijikuta namchukia sana yule mdogo angu wa kike japo sikumuonyesha wazi.
Napenda niishi mimi mke na watoto imeisha hiyo.....

Mtoa mada unajaribu kumtetea mdogo ako lkn unamkwaza mmeo, nani muhimu kati yao? Pengine anachukia kuishi na ndugu yoyote yule wewe ndio unalazimisha, kua makini hatufanani mitazamo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…