Mume wangu kaniambia kwa kuwa nina bima niende hospitali mwenyewe

Mume wangu kaniambia kwa kuwa nina bima niende hospitali mwenyewe

Ni unajipa tu umuhimu kwenye maisha ya mtu ilihali huenda huna huo umuhimu.

Mkuu kosa la jamaa ni lipi sasa hapo?? mbona unakua Mzigo wa misumari kwa ndugu yetu.

Mtu anawahi harakati zake anakupa hela uende hospital unalalamika,,, asingekupa pia ungelalamika...nini Jema kwako???

Mmeo ni mtu mzima,, kutokana na hali yako ameona unaweza kwenda mwenyewe,,, ungekuwa wa kuhitaji msaada angefanya hvo pia akupeleke.....nini sasa unalia lia humu ndugu.
 
Eti nauliza mtu akitaka kujua kuwa huyu mume nilie naye ananipenda first of all nini kinamfanya mtu adhibitishe kuwa anapendwa.

Kwa maana leo badala ya mume wangu kunipeleka hospitalini ananipa hela yakwenda hospitalini. Naharaka hela hiyo hapo nenda hospitali siuna BIMA.

Basi kaishia .........Mapenzi niliyozoea kwenye hii miaka alikuwa ananipeleka hospitali nakutaka kujua hali yangu..... Ila kwa siku hizi mapenzi kwetu nikudharauliana kama hivyoo. Seriously mimi mama JJ leo nimeachwa mataa. Naumwa hapa sana .

Ila mwenzenu yupo busy. Siuna Bima seriously anakupa hela kama mfanyakazi wake so nimemzalia watoto ndio kazi nilikuwa nafanya kwake. Hii imenikeraa.

Goodmorning soon to be afternoon
Kwahiyo unataka aache kwenda kazini akusindikize hospitali!?

Hebu kuwa serious na maisha
 
Mbona kuna wanawake wengi wanaenda wenyewe hospitalini na wako kwenye ndoa, na ndoa zao ziko freshi tu,punguza kudeka haya maisha muda mwengine ni kupambana, mama hospital na kule mzee anatafuta pesa, maisha yanakuwa matamu tu
 
Back
Top Bottom