Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Wapo wengi si uoe wengi sasa?
Na kabla hujaoa umwambie hiyo wa kwanza kuwa wewe ni wale wa kuoa Wake wengi. Na sio umtapeli.
Unajua maana ya kutapeli wewe? Namtapeli wakati nipo naye na Nampa kitu roho inapenda. Tunachepuka kuongeza upendo.
 
We fata ushauri wa mtoa mada tu, ila mkumbuke Wanaume waoaji wamebaki wachache huko mtaani
Halafu swala la ndoa si pekee Wanawake ni wahitaji wakubwa hata Wanaume mnauhitaji huo.
Ndoa ni furaha kama haipatikani 🤷🏼‍♂️
 
Kwa nini upumbavu wa mtu mwingine unifanye na mimi niwe mpumbavu?
Ndipo ninapokupendea hapo mke mtarajiwa.

Kwa ufupi mtoa mada anasema mwenza wako akitafuta UKIMWI nawewe utafute uupate ili muwe sawa.
 
nilichogundua wanaume tuna umoja sana hii hoja kwa asilimia 80 imepingwa

Tuache uovu.
Tusiwe wamoja kwenye uovu bali tuwe wamoja kwenye Haki.

Umoja wa kijinga.
Watu wanatetea ku-cheat
Unajua maana ya kutapeli wewe? Namtapeli wakati nipo naye na Nampa kitu roho inapenda. Tunachepuka kuongeza upendo.

Ngoja naye a-cheat ili aongeze upendo.
 
MUMEO AKIKU-CHEAT NA WEWE M-CHEAT

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Najua wapo wanaume watanimaindi kwenye hii mada lakini hiyo ndio namna Watibeli tunavyofanya mambo yetu.
Hatuna msamaha kwa mtu anayefanya jambo kwa kudhamiria. Hiyo hatuna.

Kitu cha kwanza niliwaambia binti zangu kuwa hakikisha unajiweza, upo huru, unajitegemea na unaweza kujilisha wewe na watoto na mumeo(ikiwa mumeo ataumwa au itatokea dharura ya kimaisha). Niliwaambia msipende kuhudumiwa, wala kupenda vya bure ili muilinde furaha yenu.

Mwanaume kabla hajakuoa. Mpe misimamo yako. Mwambie mimi nipo tayari kujisalimisha kwako kama mkeo. Na nitakutii na kukusikiliza kwa kila jambo lililokuwa. Kwenye shida na raha tutakuwa wote lakini sio kwenye uovu na uasi.

Mwambie kabisa unamoyo mzuri lakini haimaanishi huwezi kutenda mambo mabaya na yakutisha kwa Watu wasiokuheshimu.

Mwambie siku atakayo-cheat ndio siku hiyohiyo ambayo utaandaa mipango kabambe ya kum-cheat. Mwambie kabisa kuwa hutamsamehe pasipo kumpa adhabu hiyo.
Ili aonje ule utamu alioufanya juu yako.

Mwambie yeye a-cheat kwa bahati mbaya lakini wewe utafanya makusudi. Mwambie yeye a-cheat kwa kujificha na kwa siri lakini wewe utafanya waziwazi bila kificho.

Mwambie kama anahitaji uaminifu wako itampasa naye awe mwaminifu.

Mwambie ndoa za Watibeli sio za kitapeli (dhulma) utakachokifanya ndicho utakachofanyiwa. Haki bin haki.

Akikuletea porojo sijui huwezi mkomoa Mwanaume zaidi ya kujikomoa mwenyewe mwambia naye hawezi kukukomoa wewe zaidi ya kujikomoa yeye mwenyewe.

Usikubali akuzalishe watoto ambao hautakuwa na uwezo wa kuwatunza hata siku asipokuwepo( iwe kwa kuachana au Kufariki) zaa watoto kulingana na uwezo wako wa kuwatunza. Kulingana na kipato chako.

Binti za Tibeli sio Wajinga. Usidai pesa za matumizi ikiwa mwanaume hataki kukupa hizo pesa huko ni kujishushia heshima na kujidhalilisha. Ikiwa ataichukulia hiyo kama faida au kuvuja kwa pakacha. Badilisha majina ya mtoto na mpe majina ya Watibeli.

Usiwe na moyo safi kwa mtu mwenye moto mchafu dhidi yako.
Usiwe na upendo kwa mtu mwenye chuki na wewe.
Usiwe na heshima kwa mtu mwenye kukudharau.
Usimpe mtu kipaombele ikiwa yeye anakuona wa ziada.

Ikiwa mumeo au mwanaume anapenda ndugu au wazazi wake kuliko wewe. Anakuweka nafasi ya pili au ya tatu. Wewe mweke nafasi hiyohiyo aliyokuweka. Hiyo ndio HAKI.
Ikiwa mwanaume amekuweka nafasi ya kwanza nawe muweke nafasi ya kwanza.

Usiwe mtumwa wa yeyote. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

Usifikirie maisha yatakuwaje ikiwa mtu anataka kukuacha iwe kwa kusema au kwa matendo yake. Huo ni utumwa.

Binti zangu msijesema Baba yenu sikuwaambia namna ya ku-deal na wanaume. Hivyo ndivyo mtakavyoishi kwa furaha. Kamwe usiwe mtumwa wa mtu mwingine hasa asiyemtumwa wako.
Kama mume au mwanaume anajitumikisha kwaajili yako nawe jitumikishe kwaajili yake.
Mpe kile alichopanda. Nawe usione shida kulipwa kile ulichopanda. Hivyo ndivyo mambo yalivyo.

Usiogope kuwa sijui atakupiga au atakuua. Usiwe mwoga kama nilivyokufundisha. Woga utakufanya uonewe. Ni bora akuue kuliko akufanye kuwa mtumwa wake.
Akikufanyia uhalifu wapo Watu wa haki watakaodili naye ikiwemo sisi Watibeli.

Acha Baba yenu nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Wana wa Israel walikuwa na kanuni moja ikisema Tit for Tat yaani jicho kwa jicho lakini Bwana Yesu alipokuja aliirekebisha na kuiondoa.Naona wewe mwenzetu bado unaiendeleza.
 
Halafu swala la ndoa si pekee Wanawake ni wahitaji wakubwa hata Wanaume mnauhitaji huo.
Ndoa ni furaha kama haipatikani 🤷🏼‍♂️
Umesema sahihi Mkuu, lakini kwa asili sisi Wanaume tunaweza kuvumilia kuibiwa hela, kuliwa nauli, kuibiwa hati ya kiwanja/nyumba n.k

Lakini sio kusalitiwa.

Hata mimi pamoja na kuwa nipo kwenye late 78, lakini siku nisikie Bibi yenu wamemkula kimasihara wale vijana wa rikiboy basi ndiyo siku kila mtu atalala kitanda chake ikiwezekana kila mtu chumba chake 😢
 
Wanawake wengi wanaolewa kwasababu ya ugumu wa maisha, hawana uhakika wa kutoboa haya maisha bila mwanaume.
Aliyesema ndoa ni ajira hakukosea.
Ndoa ni hitaji la kila Mwanamke Mkuu

Ndiyo maana sisi miaka ile ya 1963 hadi 1971 ilikuwa ni ruksa kuoa wake hadi 12, muhimu uweze kuwatunza tu.
 
Watoto wako wa kike ni wake wa wanaume wengine hapo baadae.

Unakaa kuharibu wake za watu sasa hiv huku wewe unakaa kulia lia na mibandiko yako mireeefu hapa jukwaan kila siku ukiwaponda wanawake mara "usimuonee huruma mwanamke" na blah blah zako nyingi.

Sasa we endelea kuharibu wake za watu (watoto wako) halaf wakija huku mtaani watakutana na vyuma vya kiume unavyovipaga madini kila siku jinsi ya ku deal na mwanamke jeuri.

Watakurudia tena wakuombe ushauri
Huyo jamaa ujuaji ni mwingi mnoo.
 
Kamwe sifundishi hiki.Ntafundishaa maaadili sitaki kuwa mtumwa Jehenamu na sehemu ya laana Kwa vizazi kuanzia kizazi changu mpaka cha tatu duniani maana laana hudumu vizazi vitatu
 
Ndoa ni hitaji la kila Mwanamke Mkuu

Ndiyo maana sisi miaka ile ya 1963 hadi 1971 ilikuwa ni ruksa kuoa wake hadi 12, muhimu uweze kuwatunza tu.
Hujawahi kuwa mwanamke unajuaje hitaji lao?
Ndoa ni huko zamani sio sasa hivi majanga matupu.
Mimi ni mwanamke naona ndoa ni upuuzi sasa unasemaje ni hitaji la kila mwanamke?
 
Back
Top Bottom