Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Tibeli hajui what it takes kucheat kwa mwanamke. Ndio maana mwanamke kama hana “njaa/tamaa ya vikubwa” ni ngumu sana kuwa cheater.

Kumlipa mtu haki yake sio ku-cheat.
Ni haki kama haki zingine.
Akitenda wema anapongezwa kwa mema akitenda mabaya lazima mtu awajibishwe kwa kiwango kilekile.

Kumpa mtu haki yake sio kumkomoa
 
MUMEO AKIKU-CHEAT NA WEWE M-CHEAT

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Najua wapo wanaume watanimaindi kwenye hii mada lakini hiyo ndio namna Watibeli tunavyofanya mambo yetu.
Hatuna msamaha kwa mtu anayefanya jambo kwa kudhamiria. Hiyo hatuna.

Kitu cha kwanza niliwaambia binti zangu kuwa hakikisha unajiweza, upo huru, unajitegemea na unaweza kujilisha wewe na watoto na mumeo(ikiwa mumeo ataumwa au itatokea dharura ya kimaisha). Niliwaambia msipende kuhudumiwa, wala kupenda vya bure ili muilinde furaha yenu.

Mwanaume kabla hajakuoa. Mpe misimamo yako. Mwambie mimi nipo tayari kujisalimisha kwako kama mkeo. Na nitakutii na kukusikiliza kwa kila jambo lililokuwa. Kwenye shida na raha tutakuwa wote lakini sio kwenye uovu na uasi.

Mwambie kabisa unamoyo mzuri lakini haimaanishi huwezi kutenda mambo mabaya na yakutisha kwa Watu wasiokuheshimu.

Mwambie siku atakayo-cheat ndio siku hiyohiyo ambayo utaandaa mipango kabambe ya kum-cheat. Mwambie kabisa kuwa hutamsamehe pasipo kumpa adhabu hiyo.
Ili aonje ule utamu alioufanya juu yako.

Mwambie yeye a-cheat kwa bahati mbaya lakini wewe utafanya makusudi. Mwambie yeye a-cheat kwa kujificha na kwa siri lakini wewe utafanya waziwazi bila kificho.

Mwambie kama anahitaji uaminifu wako itampasa naye awe mwaminifu.

Mwambie ndoa za Watibeli sio za kitapeli (dhulma) utakachokifanya ndicho utakachofanyiwa. Haki bin haki.

Akikuletea porojo sijui huwezi mkomoa Mwanaume zaidi ya kujikomoa mwenyewe mwambia naye hawezi kukukomoa wewe zaidi ya kujikomoa yeye mwenyewe.

Usikubali akuzalishe watoto ambao hautakuwa na uwezo wa kuwatunza hata siku asipokuwepo( iwe kwa kuachana au Kufariki) zaa watoto kulingana na uwezo wako wa kuwatunza. Kulingana na kipato chako.

Binti za Tibeli sio Wajinga. Usidai pesa za matumizi ikiwa mwanaume hataki kukupa hizo pesa huko ni kujishushia heshima na kujidhalilisha. Ikiwa ataichukulia hiyo kama faida au kuvuja kwa pakacha. Badilisha majina ya mtoto na mpe majina ya Watibeli.

Usiwe na moyo safi kwa mtu mwenye moto mchafu dhidi yako.
Usiwe na upendo kwa mtu mwenye chuki na wewe.
Usiwe na heshima kwa mtu mwenye kukudharau.
Usimpe mtu kipaombele ikiwa yeye anakuona wa ziada.

Ikiwa mumeo au mwanaume anapenda ndugu au wazazi wake kuliko wewe. Anakuweka nafasi ya pili au ya tatu. Wewe mweke nafasi hiyohiyo aliyokuweka. Hiyo ndio HAKI.
Ikiwa mwanaume amekuweka nafasi ya kwanza nawe muweke nafasi ya kwanza.

Usiwe mtumwa wa yeyote. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

Usifikirie maisha yatakuwaje ikiwa mtu anataka kukuacha iwe kwa kusema au kwa matendo yake. Huo ni utumwa.

Binti zangu msijesema Baba yenu sikuwaambia namna ya ku-deal na wanaume. Hivyo ndivyo mtakavyoishi kwa furaha. Kamwe usiwe mtumwa wa mtu mwingine hasa asiyemtumwa wako.
Kama mume au mwanaume anajitumikisha kwaajili yako nawe jitumikishe kwaajili yake.
Mpe kile alichopanda. Nawe usione shida kulipwa kile ulichopanda. Hivyo ndivyo mambo yalivyo.

Usiogope kuwa sijui atakupiga au atakuua. Usiwe mwoga kama nilivyokufundisha. Woga utakufanya uonewe. Ni bora akuue kuliko akufanye kuwa mtumwa wake.
Akikufanyia uhalifu wapo Watu wa haki watakaodili naye ikiwemo sisi Watibeli.

Acha Baba yenu nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Hapo kwenye bold hapo, ndo patamu..!! Ndo wanaposhindwia wengi..!!! Huwezi rudishia ku-cheat kwa anayekufanyia kila kitu..!! Kwamba akiyakata anayokufanyia umeisha..!!
 
Hapo kwenye bold hapo, ndo patamu..!! Ndo wanaposhindwia wengi..!!! Huwezi rudishia ku-cheat kwa anayekufanyia kila kitu..!! Kwamba akiyakata anayokufanyia umeisha..!!

Wanawake wengi ni wanafiki kwa sababu ya umaskini. Kuwa tegemezi. Lakini kanuni hizi zinatumiwa na Wadada wote wanaojiweza.

Huwezi leta dharau alafu ukadai heshima
 
Kuna mwanamke alitaka anipe penzi nikamuuliza vipi utake kunipa penzi penzi na una mume? Alinijibu mume wake anafanya nje na yeye anataka afanye. Yupo mwingine naye alikuja kushitaki kwangu kuwa mume wake ana michepuko mingi na yeye anataka awe nayo mingi ili ngoma iwe droo. Alishitaki kama mume wake anafanya na yeye atafanya. Wanawake wengine waume zao ni wababe wakifanya nje watakabaliwa na kipigo cha kufa mtu
 
Mkuu leo umezingua na hii mada yako.

Alafu tangu lini Asiye oa akamshauri aliye oa?

Wanawake please, kama mnaipenda ndoa yenu msije kufata ushauri wa huyu Mtibeli.

Anataka kuwapotosha ili muachike huko kwenye ndoa zenu alafu mje Michelle humu.

Kumbukeni,

Mwanamke mpumbavu atavunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ....
 
Mkuu leo umezingua na hii mada yako.

Alafu tangu lini Asiye oa akamshauri aliye oa?

Wanawake please, kama mnaipenda ndoa yenu msije kufata ushauri wa huyu Mtibeli.

Anataka kuwapotosha ili muachike huko kwenye Mwanamke ndoa zenu alafu mje Michelle humu.

Kumbukeni,

Mwanamke mpumbavu atavunja ndoa yake kwa mikono yake mwenyewe ....

Suleiman aliyeandika hiyo aya mwenyewe aliandika kuwa aziniye na Mwanamke jana akili kabisa. Alafu yeye akazini na wanawake miatatu
 
Kuna mwanamke alitaka anipe penzi nikamuuliza vipi utake kunipa penzi penzi na una mume? Alinijibu mume wake anafanya nje na yeye anataka afanye. Yupo mwingine naye alikuja kushitaki kwangu kuwa mume wake ana michepuko mingi na yeye anataka awe nayo mingi ili ngoma iwe droo. Alishitaki kama mume wake anafanya na yeye atafanya. Wanawake wengine waume zao ni wababe wakifanya nje watakabaliwa na kipigo cha kufa mtu

Kipigo cha kufa Mtu😆😆
 
Wakumbushe mtaani Wanaume waoaji ni wachache sana, bora watulia na ndoa zao

Binti zako waambie wasome, kisha wafanye kazi za uzalishaji mali. Alafu ndoa itakuja tuu.
Kuliko ndoa ije ya kuumizana.

Wanaume tuache ku-cheat na kama tutafanya kufanya usaliti basi malipo yetu yawe vilevile tulivyofanya.
Hiyo ndio Haki
 
Back
Top Bottom