Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Mumeo akiku-cheat na wewe m-cheat

Binti zako waambie wasome, kisha wafanye kazi za uzalishaji mali. Alafu ndoa itakuja tuu.
Kuliko ndoa ije ya kuumizana.

Wanaume tuache ku-cheat na kama tutafanya kufanya usaliti basi malipo yetu yawe vilevile tulivyofanya.
Hiyo ndio Haki
We mzee leo unazingua.

Kwahiyo umekosa kabisa ushauri wa kuwapa Wanawake zetu hadi uwape ushauri wa hivyo?
 
Hakuna dawa ya kumkomoa mume. Muhimu ukae naye chini umtulize.

Waoaji wamebaki wachache ujue
Mwanaume Msaliti anatulizwa kwa njia gani?
Maumivu yanatulizwa kwa kulea watoto wasio kuwa wenu.
 
We mzee leo unazingua.

Kwahiyo umekosa kabisa ushauri wa kuwapa Wanawake zetu hadi uwape ushauri wa hivyo?

Sipendi uonevu.
Sipendi mtu awe na haki ya kufanya uovu dhidi ya mwingine.

Sisi wanaume tumejipa uhalali wa kufanya baadhi ya uovu kwa kisingizio cha Uanaume. Huo ni uovu na sio HAKI.

Lazima tujenge jamii yenye kupenda haki. Kuwa tayari kuipokea na kuitumikia.
Sasa kama mwanaume anacheat kwa nini asilipwe sawasawa na matendo yake?

Hapo pointi kubwa ilikuwa wanaume tusicheat na sio niambiwe kuwa nisiwashauri wanawake wasilipe kisasi ilhali hiyo nsio Haki
 
Sipendi uonevu.
Sipendi mtu awe na haki ya kufanya uovu dhidi ya mwingine.

Sisi wanaume tumejipa uhalali wa kufanya baadhi ya uovu kwa kisingizio cha Uanaume. Huo ni uovu na sio HAKI.

Lazima tujenge jamii yenye kupenda haki. Kuwa tayari kuipokea na kuitumikia.
Sasa kama mwanaume anacheat kwa nini asilipwe sawasawa na matendo yake?

Hapo pointi kubwa ilikuwa wanaume tusicheat na sio niambiwe kuwa nisiwashauri wanawake wasilipe kisasi ilhali hiyo nsio Haki
Hivi unajua anayeoa siku zote ni Mwanaume?

We walishe matangopori wenzako
 
Unacheat Kwa makusudi mwanamke unajiathiri kisaikolojia mara mbili. Kwanza mumeo ka kucheat una mawazo, unakwenda kucheat Kwa makusudi hufurahii mashine inavyoingia, na bado umeokoteza mwanaume eti tu ulipe kisasi pumbafu. Wanaume tunapocheat sio kwamba hatuwapendi jamani, tunawapenda mnooo, ila mko wengiii. Wengine wataishije, hivi nyie hamuna huruma Kwa wenzenu?
 
Hakuna dawa ya kumkomoa mume. Muhimu ukae naye chini umtulize.

Waoaji wamebaki wachache ujue

Kila Muovu anadawa yake bila kujali ni mwanaume au mwanamke.

Kusema mwanaume hakomolewi wakati kila siku Watu wanapata Stroke, Presha, na wengine kujiua kisa wanawake ni kujidanganya na kudanganya wajinga.

Wangapi wanaingizwa kingi kwa kulea damu zisizozao? Hapo bado haujashikishwa adabu?,

Unachosema ni sawa na kipindi kile Watu walikuwa wanaamini mzungu Hafi na hawezi kukomolewa lakini ukweli ulidhihirika.

Ukishakuwa Muovu dawa yako ipo. Na dawa ya uovu ni uovu tuu.

Ndio maana hata kwenye dini, washambuliaji na waovu watamlazimisha Mungu kutenda uovu kuwa katili (kwa kuwachoma moto)
 
Unacheat Kwa makusudi mwanamke unajiathiri kisaikolojia mara mbili. Kwanza mumeo ka kucheat una mawazo, unakwenda kucheat Kwa makusudi hufurahii mashine inavyoingia, na bado umeokoteza mwanaume eti tu ulipe kisasi pumbafu. Wanaume tunapocheat sio kwamba hatuwapendi jamani, tunawapenda mnooo, ila mko wengiii. Wengine wataishije, hivi nyie hamuna huruma Kwa wenzenu?

Wapo wengi si uoe wengi sasa?
Na kabla hujaoa umwambie hiyo wa kwanza kuwa wewe ni wale wa kuoa Wake wengi. Na sio umtapeli.
 
Wanawake wengi ni wanafiki kwa sababu ya umaskini. Kuwa tegemezi. Lakini kanuni hizi zinatumiwa na Wadada wote wanaojiweza.

Huwezi leta dharau alafu ukadai heshima
NA WALIO WENGI WANAOFUATA KANUNI HIZO, EIDHA NDO IPO MATATANI AU WASHAACHIKA TAYARI..!!
 
Haki bin Haki.
Ndio maana ninawaambiaga hawa mabinti wajitegemee. Ili kuondoa manyanyaso na utumwa.
Najua hujui thamani ya wazazi yaani baba na mama kuwa pamoja sababu wazazi wako walikuwa wazinzi wakaachana ukaenda kulelewa na bibi na babu.
Uliandika mwenyewe hapa hivyo akili zako za ki single mother.
 
Wanawake wengi wanaolewa kwasababu ya ugumu wa maisha, hawana uhakika wa kutoboa haya maisha bila mwanaume.
Aliyesema ndoa ni ajira hakukosea.



Huo ndio ukweli mchungu.

Asomae na afahamu.
 
Jomba una undugu wowote na huyu papa wa katoliki aliyeko madarakani? Siku hizi mada zako zinaendana na tamko alilotoa majuzi. Inaonekana wewe bado ni kinda bado hujafikia ya kuitwa mwanaume. Huu uzi ni ushahidi. Nikushauri wewe na wanawake wote wanaokuunga mkono kuwa HAKUNA MWANAMKE ANAYEWEZA KUSHINDA AKISHINDANA NA MUME WAKE. Labda kama talaka ndo ushindi.
 
MUMEO AKIKU-CHEAT NA WEWE M-CHEAT

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Najua wapo wanaume watanimaindi kwenye hii mada lakini hiyo ndio namna Watibeli tunavyofanya mambo yetu.
Hatuna msamaha kwa mtu anayefanya jambo kwa kudhamiria. Hiyo hatuna.

Kitu cha kwanza niliwaambia binti zangu kuwa hakikisha unajiweza, upo huru, unajitegemea na unaweza kujilisha wewe na watoto na mumeo(ikiwa mumeo ataumwa au itatokea dharura ya kimaisha). Niliwaambia msipende kuhudumiwa, wala kupenda vya bure ili muilinde furaha yenu.

Mwanaume kabla hajakuoa. Mpe misimamo yako. Mwambie mimi nipo tayari kujisalimisha kwako kama mkeo. Na nitakutii na kukusikiliza kwa kila jambo lililokuwa. Kwenye shida na raha tutakuwa wote lakini sio kwenye uovu na uasi.

Mwambie kabisa unamoyo mzuri lakini haimaanishi huwezi kutenda mambo mabaya na yakutisha kwa Watu wasiokuheshimu.

Mwambie siku atakayo-cheat ndio siku hiyohiyo ambayo utaandaa mipango kabambe ya kum-cheat. Mwambie kabisa kuwa hutamsamehe pasipo kumpa adhabu hiyo.
Ili aonje ule utamu alioufanya juu yako.

Mwambie yeye a-cheat kwa bahati mbaya lakini wewe utafanya makusudi. Mwambie yeye a-cheat kwa kujificha na kwa siri lakini wewe utafanya waziwazi bila kificho.

Mwambie kama anahitaji uaminifu wako itampasa naye awe mwaminifu.

Mwambie ndoa za Watibeli sio za kitapeli (dhulma) utakachokifanya ndicho utakachofanyiwa. Haki bin haki.

Akikuletea porojo sijui huwezi mkomoa Mwanaume zaidi ya kujikomoa mwenyewe mwambia naye hawezi kukukomoa wewe zaidi ya kujikomoa yeye mwenyewe.

Usikubali akuzalishe watoto ambao hautakuwa na uwezo wa kuwatunza hata siku asipokuwepo( iwe kwa kuachana au Kufariki) zaa watoto kulingana na uwezo wako wa kuwatunza. Kulingana na kipato chako.

Binti za Tibeli sio Wajinga. Usidai pesa za matumizi ikiwa mwanaume hataki kukupa hizo pesa huko ni kujishushia heshima na kujidhalilisha. Ikiwa ataichukulia hiyo kama faida au kuvuja kwa pakacha. Badilisha majina ya mtoto na mpe majina ya Watibeli.

Usiwe na moyo safi kwa mtu mwenye moto mchafu dhidi yako.
Usiwe na upendo kwa mtu mwenye chuki na wewe.
Usiwe na heshima kwa mtu mwenye kukudharau.
Usimpe mtu kipaombele ikiwa yeye anakuona wa ziada.

Ikiwa mumeo au mwanaume anapenda ndugu au wazazi wake kuliko wewe. Anakuweka nafasi ya pili au ya tatu. Wewe mweke nafasi hiyohiyo aliyokuweka. Hiyo ndio HAKI.
Ikiwa mwanaume amekuweka nafasi ya kwanza nawe muweke nafasi ya kwanza.

Usiwe mtumwa wa yeyote. Hivyo ndivyo Watibeli tulivyo.

Usifikirie maisha yatakuwaje ikiwa mtu anataka kukuacha iwe kwa kusema au kwa matendo yake. Huo ni utumwa.

Binti zangu msijesema Baba yenu sikuwaambia namna ya ku-deal na wanaume. Hivyo ndivyo mtakavyoishi kwa furaha. Kamwe usiwe mtumwa wa mtu mwingine hasa asiyemtumwa wako.
Kama mume au mwanaume anajitumikisha kwaajili yako nawe jitumikishe kwaajili yake.
Mpe kile alichopanda. Nawe usione shida kulipwa kile ulichopanda. Hivyo ndivyo mambo yalivyo.

Usiogope kuwa sijui atakupiga au atakuua. Usiwe mwoga kama nilivyokufundisha. Woga utakufanya uonewe. Ni bora akuue kuliko akufanye kuwa mtumwa wake.
Akikufanyia uhalifu wapo Watu wa haki watakaodili naye ikiwemo sisi Watibeli.

Acha Baba yenu nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Dawa ya moto sio lazima iwe moto inaweza kuwa maji pia...

..usikariri
 
Back
Top Bottom