Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

Muna Love: Wakati naolewa na Peter nilikuwa na mimba ya Casto ya miezi miwili

Kila msiba una sababu, Mungu ni mwema sana mpaka kaamua kumsitiri huyu mtoto kabla hata umri wake haujafika mbali.
Hebu chukulia huyu ni mama yako mzazi umefikia umri mkubwa unamsikia anafanya mambo kama haya huoni utatamani dunia itoboke uzame kabisa?
Kwanini uliolewa ukijua una ujauzito wa mtu mwingine , wangapi wameolewa baada ya kuzaa na heshima zao zimebaki na kama uliamua kufanya hivyo kwanini leo hii uliseme?
Kosa kubwa ni kuolewa akiwa na ujauzito wa mwanaume mwingine, kamkatili sana peter.
 
Kwanini asingekua mkweli tuu kabla ya kufunga ndoa?
Kweli dhambi huzaa mauti... maskini kichanga wa watu hana hata dhambi... anyway hujui MUNGU kamuepusha na nini maana naona giza hapo.
 
Muigiza Maarufu Bongo, Muna Love, amezungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuweka wazi jinsi ambavyo alikutana na Peter Zakaria Komu, mwanaume ambaye hivi karibuni ilisemekana kuwa ndiye baba wa mtoto wake Marehemu Patrick.

“Nilikutana na Peter jijini Mbeya tukiwa tunafanya kazi Safari Pool Table, tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi miwili tukaingia kwenye ndoa, lakini kuna vitu nilivyokutana navyo kwenye ndoa hiyo nikaamua kuachika.

“Wakati naingia kwenye mahusiano na Peter nilikuwa nina mimba ya Casto ya miezi miwili, Casto aliikana mimba hiyo. Baadaye alirudi wakati mtoto Patrick akiwa na miaka mitatu. Kwa sababu nilizaa nikiwa kwenye ndoa na Peter ndiye alisimamia hata ubatizo ndizo picha zilizosabaa, lakini hata yeye Peter anaujua ukweli kuhusu mtoto huyo.

“Tulifanya taratubu na Casto za kubadilisha jina la mtoto pale RITA lakini kuna ugumu uliotokea, lakini tulikuwa tunaendelea kufuatilia,” amesema Muna.
MALAYA TU WA MJINI HAWA HAWANA JIPYA ZAIDI YA KUTAFUTA KICK
 
Tutafutapo wake inabidi tufunge na kusali kweli, sometime hizi mila za Unyago zina vitu vizuri vya kumfunza mwanamke. Siku hizi watu social networks, zimewatawala vichwa vyao, hivi maswala nyeti ya kifamilia kuweka insta, ili iweje. Haitoshi mshazika mtoto lkn bado unaona haitoshi bado unaita press conference kueleza siri za familia (hapa ndio unaona umuhimu wa Unyago). Kwa mara ya pili tena umejizalilisha ww na umemdhalilisha marehemu mtoto wako, sometime inabidi ujue habari ya kuiweka social networks, nyingine siri zinabaki kuwa za familia na Kuna siri nyingine unakufa nazo ww kwani kwa kuongea unaweza sababisha amani na mtafaruku mkubwa kwenye jamii. Huyu ashukuru yule mume wake mkimya lkn kama ingekuwa mtu mwengine sasa hivi tungekuwa na msiba zaidi ya mmoja.
 
Angekua ni dadaangu walahi angekula bakora 50 za mkia wa taa
 
Muigiza Maarufu Bongo, Muna Love, amezungumza na waandishi wa habari leo nyumbani kwake maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam na kuweka wazi jinsi ambavyo alikutana na Peter Zakaria Komu, mwanaume ambaye hivi karibuni ilisemekana kuwa ndiye baba wa mtoto wake Marehemu Patrick.

“Nilikutana na Peter jijini Mbeya tukiwa tunafanya kazi Safari Pool Table, tulikaa kwenye mahusiano kwa miezi miwili tukaingia kwenye ndoa, lakini kuna vitu nilivyokutana navyo kwenye ndoa hiyo nikaamua kuachika.

“Wakati naingia kwenye mahusiano na Peter nilikuwa nina mimba ya Casto ya miezi miwili, Casto aliikana mimba hiyo. Baadaye alirudi wakati mtoto Patrick akiwa na miaka mitatu. Kwa sababu nilizaa nikiwa kwenye ndoa na Peter ndiye alisimamia hata ubatizo ndizo picha zilizosabaa, lakini hata yeye Peter anaujua ukweli kuhusu mtoto huyo.

“Tulifanya taratubu na Casto za kubadilisha jina la mtoto pale RITA lakini kuna ugumu uliotokea, lakini tulikuwa tunaendelea kufuatilia,” amesema Muna.
Huu ni ukichaa Mara ulikaa na Peter kwa miezi miwili mkafunga ndoa alafu happy hapo wakati unaolewa ulikuwa na mimba ya casto ya miezi miwili,kwahiyo wakati unamahusiano na Peter hiyo miezi miwili huku unatiwa mimba na casto utamwaminisha vipi mtanzania mwenye uelewa mdogo Kama Mimi kwamba hiyo sio sinema ulikuwa unacheza??
 
huyo maimuna ni kielelezo sahihi cha tabia ya wanawake wengi wa kitanzania
kama mimba ya casto kwa nini pesa alikua anachukua kwa peter?
halafu anajifanya kaokoka,huyo atapata tabu sana na utapeli wake,mwisho atakwenda tu kumuangukia mumewe
 
Fertile communication and confidentiality are very important in any relation! Huyu mwanamke anakosa vyote viwili japo nimemhukumu but ni funzo kwa wengine!
Kukataliwa kwa mimba siyo sababu ya kumpa zawadi mwanamme mwingine bali alitakiwa kusimama kwenye haki na wangewasiliana vyema na huyo aliyemuoa ili amzalie wa kwake ili kubalance! Huku kuropoka kwa waandishi hakumsaidii kuondoa makosa na dhambi ya unyang'anyi wa mtoto! Amtafute counsellor amsaidie kuliondoa tatizo alilo nalo na sio waandishi ambao watakuzidishia maumivu ya moyo! Anyway, sorry for her illiteracy!
 
mnh,kuna kitu kinaitwa assertive tactics in impression management..

msimcheke muna, labda na nyie mngekua kama yeye,mngefanya the same...

desperate need to repair image ambayo imekua tarnished,

pole Muna,mie nakuelewa unachofanya,

ila ,

iwe mwisho kuwasiliana na waandishi,

unamwaga petrol kwenye moto tayari…

wataendelea kukusema tu..

wanadamu wabaya..

watavunja ndoa yako for real
Ndoa ipi??
 
Back
Top Bottom