Umetuwekea andiko hapo juu linalozungumzia msamaha, ajabu wewe na wenzio mmeshindwa kumsamehe Magufuli mpaka mnamuita shetani, kwa ujinga wenu hamjui andiko lingine linalosema; "usihukumu ili nawe usije kuhukumiwa"
Nyie kila siku nawaona mmeamua kubebana kama kondoo, mnaolishana upupu na bahati mbaya asiwepo yeyote miongoni mwenu wa kumuamsha mwenzie, wajinga nyie mnajiona "malaika" mbele za Mungu mlioruhusiwa kuhukumu wengine lakini nyie hamtahukumiwa!.
Sijui ni lini mtaamka, kwa maana huu usingizi mzito mliolala, hakika hamna tofauti na mtu aliye kwenye koma amelazwa hospitalini, ndugu zake wakimtazama kwa huzuni hata wasijue ni lini mwenzao atarudiwa na fahamu zake.