Mungu alimtoa sadaka mwanae wa pekee, ikiwa yeye ndie Mungu Sadaka aliitoa kwa nani?

Mungu alimtoa sadaka mwanae wa pekee, ikiwa yeye ndie Mungu Sadaka aliitoa kwa nani?

Mbona hili swala linajadiliwa mara kwa mara Ombeni Access kule jukwaa la dini. Mkasomee
 
Habari wadau

Mafundisho ya kanisani na hata biblia yanafundisha Mungu alimtoa sadaka mwanae wa pekee.

Je, Mungu alimpa nani hiyo sadaka ikiwa yeye ndie Mungu?
Kwanini unamuomba Mungu ikiwa yeye anajua mahtaji yako?
 
Siku pi hiyo nafasi good night uku kwetu ni usiku sana

Hunipi nafasi hiyo wakati wewe ndiye umeni tag hapa, unajielewa unataka nini?

Wewe hujaelewa kuwa kukosa dini si upagani.

Wapagani nao wana dini zao.

Mimi sina dini na hivyo si mpagani.

Soma ujielimishe, usiharibu maneno ya watu yenye maana maalum.
 
Hujawahi toa sadaka kwa wasiojiweza Ukiwapa hao ndo watatoa ushuda wa kupewa sadaka
 
Duh . Umekisoma ulichokiandika lakini ?

Mungu aliwapa watenda dhambi sadaka ? Mbona kanisani hatupewi sadaka wanasema sadaka zote ni za Mungu ?
Sadaka inayotolewa na Binadamu ni ya Mungu na sadaka inayotolewa na Mungu ni ya Binadamu.
 
Mungu alimtoa mwanae wa pekee ili akafanyike mbegu ya ukombozi wa wanadamu!

Kiufupi Mungu alionesha fomula ya kwamba ili UVUNE lazima uwe utoe Mbegu!
Hata leo ili mkulima avune huwa ni lazima atoe mbegu yake iliyobora kwa ajili ya kuharibu shambani (anaitupa/anaizika ) Ili kwa punje moja ikalete punje nyingi!

Mungu alitoa msingi kwamba huwezi kuvuna pasipo kupanda!

Hivyo Mungu Alitoa Mali (sadaka) yake kama kafala ili ikafanyike kuwa mbegu kwa kuukomboa ulimwengu kwa kila AAAMINIYE! (hakusema kwa kila mtu hapana, bali kwa kila AAMINIYE)
Hivyo yule anaeutazama msalaba wa Yesu kwa Imani ya ukombozi Hupokea Uponyaji (elewa neno Aaminiye)

Hivyo Mungu ni mkulima wa kwanza kupanda mbegu kwa faida yake mwenyewe!

Ndiyo maana bibilia inasema Mungu husamehe kila roho inayotubu kwa Faida ya Mungu mwenyewe!

Alitoa sadaka ya Yesu kama mbegu bora kwa Faida yake Mwenyewe!
 
Kwanini unamuomba Mungu ikiwa yeye anajua mahtaji yako?
Hata wewe mbona unajinyenyekeza kwa Mme wako, wakati yeye kama mwanaume anatambua jukumu lake kwako
 
Habari wadau

Mafundisho ya kanisani na hata biblia yanafundisha Mungu alimtoa sadaka mwanae wa pekee.

Je, Mungu alimpa nani hiyo sadaka ikiwa yeye ndie Mungu?
Majibu utayopata hapa ni "Biblia huwezi kuielewa kama huna upako na roho mtakatifu"
 
Back
Top Bottom