Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Asante mkuu.

Nime note point moja ya msingi "kumjua Mungu kunabaki kuwa fumbo asilia"
 
Sasa we bro! Mbona unauliza maswali, marahisi ya, kindergarten, waliotengeneza samsung, i phone, diesel engine, Instagram, Facebook, drone, bulb, waliangalia wapi?
Kabla ya ICBM intercontinental ballistic missile, aliyetengneneza aliangalia wapi? Bro kila kitu ni mawazo tu, aliyetengenenza chanjo ya pepopunda, tete kuwanga, aliangalia wapi? Kama mwanadamu anauwezo, huo!sembuse Muumba!
 
"uumbaji ilikuwa ni udhihirisho wa kile kilichokuwepo tayari"

Hicho kilicho kuwepo tayari ndiyo hicho mimi nakitafta kilikuwaga wapi na kilikuwa katika hali gani kabla hakijaumbwa, maana umesema kilikuwa tayari.
 
Kwenye kila ulicho kitaja hapo juu sidhani kama ilikuwa ni wazo jipya.

Zaidi naona tu ilikuwa ni uboreshaji wa vitu ambavyo tayari vilishakuwepo awali hata kama havikuwa fanisi
 
Hata wewe swali lako hili la "Mungu aliona wapi dunia ndio akaiumba hivi" Halina logic wala reasoning.

Kwa vile hakuna uthibitisho wowote ule wa uwepo wa huyo Mungu na hakuna uthibitisho wowote ule wa kwamba ulimwengu uliumbwa.

Ulimwengu haujaumbwa, ulimwengu ulikuwepo, upo na utaendelea kuwepo.
 
Hakuna kitu kinaitwa "kilikuwepo" kwenye hii universe apart from God himself.

Hicho kisayansi cha nature kinachokusumbua kichwa mimi nna idea nacho kuliko hata wewe hapo.

Labda Kiranga pekee ndiyo anaweza kuongea kuhusu hilo ndiyo nikamwelewa ila siyo wewe ambae hoja zako ni nyepesi sana kama uji wa mtoto
 
Ulikua katika maono/mawazo/fikra za Mungu mwenyewe mkuu πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
Hicho kilicho kuwepo tayari ndiyo hicho mimi nakitafta kilikuwaga wapi na kilikuwa katika hali gani kabla hakijaumbwa, maana umesema kilikuwa tayari.
Hata haya magari kabla hayajavumbuliwa, dhamira na taswila kamili ya gari ilikua katika fikra, mawazo, maono ya mvumbuzi.

Na hata hivi sasa kuna watu wanamaono fulani, so idea ya hicho kitu ipo katika fikra ila haijadhihirishwa bado Kwahiyo ni suala la muda kama mtu huyo atapata neema ya kutekeleza na kulikamilisha idea yake basi tutapata kuona kitu kipya.
Mungu ni mwingi wa maono, na kila kitu kilianza kama maono katika fikra za mtu... Kwanza mtu anakua na maono => baadae linakua wazo=>ndipo inapatikana taswira halisi ya kitu => kazi inabakia katika utekelezaji kuunda kitu hicho
 
Hakuna kitu kinaitwa "kilikuwepo" kwenye hii universe apart from God himself.
Hata huyo God wako hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
Hicho kisayansi cha nature kinachokusumbua kichwa mimi nna idea nacho kuliko hata wewe hapo.
Hicho kiimani chako cha huyo God ni kiimani uchwara tu, Cha watu wajinga wajinga kama wewe mnaotaka kufosi mawazo yenu uchwara yasiyo na uthibitisho wowote ule.
Labda Kiranga pekee ndiyo anaweza kuongea kuhusu hilo ndiyo nikamwelewa ila siyo wewe ambae hoja zako ni nyepesi sana kama uji wa mtoto
Kumbe unaongea kitu ambacho tayari ulisha eleweshwa ila unataka kuendelea kuulizia maswali yasiyo na mantiki.

Wewe ni Tabularasa ..!!
 
Kwani mtu wa kwanza kabisa kujenga Nyumba,alitoa wapi ramani au mfano wa Nyumba? Aliyetengeneza Gari,Meli,Ndege,Simu,Viatu,Saa,Tv....nae alitoa wapi ramani au mfano wa hivyo vitu?

Ukipata majibu ya hayo maswali yangu utakua umepata jibu la swali lako.
 
Na Mm naongezea swali.

Tunaambiwa mwanzo ilikuwa inaitwa Pangea pamoja na muundo tofauti na wa sasa, kwahy maana yake ni kwamba Mungu alikosea kuumba dunia hvy akarudi tena field akatengeneza tena na kuwa na muundo huu wa sasa?
 
Mnahangaika sana kumwelezea na kumuongelea huyo Mungu kwa vile Hayupo na hajawahi kuwepo kujiongelea mwenyewe.
 
Jibu swali
 
Mungu yupi? Unaweza kuthibitisha huyo Mungu yupo?
 
Siyo lazima aione anaweza akabuni mwenyewe
 
Kwanini mungu alimfukuza shetani (Lucifer) mbinguni, akamleta duniani, kwani kulikuwa hakuna mahali pakumpeleka?

ni uwasi gani alioufanya shetani mpaka kusababisha mungu wa hurum na msamaha, kutomsamehe shetani?

Kwanini hatujui ukweli wa kisa cha mungu na shetani kuchukiana wakati walikuwa pamoja na mpaka mmoja kuaza kumfukuza mwenzake...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…