Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Kwa nini unazungumza na wanaoamini tu? Kama jibu la kweli lipo nje ya imani ya Mungu hapo huoni kuwa utakuwa unauliza jibu katika imani ya uongo?
 
Kwa mimi sina mengi ila naomba usome biblia kisha uje ulimwenguni usome ulimwengu na mabadiliko ya kwanzia miaka ya 90 tu mpaka sasa utagundua ata mwanadamu afanyi mfano anakadiria
 
Kwanini mungu alimfukuza shetani (Lucifer) mbinguni, akamleta duniani, kwani kulikuwa hakuna mahali pakumpeleka?

ni uwasi gani alioufanya shetani mpaka kusababisha mungu wa hurum na msamaha, kutomsamehe shetani?

Kwanini hatujui ukweli wa kisa cha mungu na shetani kuchukiana wakati walikuwa pamoja na mpaka mmoja kuaza kumfukuza mwenzake...
Mambo ni mengi sana ya kujiuliza. Wanadai kama ulikuwa mwema ukifa unaenda mbinguni. Lakin hapo hapo kuna concept kuwa mwisho wa dunia tutafufuliwa wote na kupewa hukumu. Sasa walio mbunguni watakuja tena duniani au likoje hili!
 
Achana na spoon feeding za wazungu, dunia yetu hii haijaumbwa na huyo mungu, mungu mnayemwabufu na kumtolea fedha ni binadam kutoka sayari zingine, human existence ni project za watu kutoka sayari ya nibiru na huwa wanakuja kuangalia maendeleo yetu toka wametutengeneza hadi leondo sisi tunawaita alien, wana interaction na baadhi ya binadam, kasome vixuri area51 iliyo marekani. Hakuna kitu kinaitwa mungu, ni imani za kishenzi kuwahi kutokea. Matukio huwa yanajirudia mkuu, kwa sasa mnaona utitiri wa vimakanisa ama madhehebu, miaka 3000 mbele waliojiiita mungu wale wakenye watakuwa na wafuasi dunia nzima na kweli wataamini mungu aaka yesu alizaliwa kenya akaaishi na akapaa mbinguni, yesu pia alikuja kwa staili hiyo ndo maana ndugu zake wenyewe walimuua kwa sababu ya kukaidi sheria kali za wayahudi. Sisi ni wakristo ana tunamfuata yesu, ila nikuhakikishir yesu hakuwa mkristo alikuwa anasali dini za kiyahudi tungeamini dini za kiyahudi basi angalau, wayahudi wenyewe hawaamini katika yesu na ukimtaja unakula kifungo
Kifungo cha nin sasa? Kwahiyo hata nikisema mimi naamini ng'ombe wananofunga pia?
 
Hapa ni Open forum kila mtu yupo huru kuchangia na kutoa maoni yake.

Hapa sio kanisani au msikitini, Huwezi kumpangia mtu namna gani ya kutoa maoni.

Kama maoni yangu yanakukera niblock usione comment zangu.

Vinginevyo Huna Mamlaka yeyote ya kunipangia namna gani nitoe maoni.
Hakuna wa kukupangia lakini tumia akili pia, huyu anawauliza wale wa upande waka yaani wanaoamin ndiyo msioamini siyo lazima kuchangia. Kifupi anataka mchango wa wale wanaoamin tu
 
Hakuna wa kukupangia lakini tumia akili pia, huyu anawauliza wale wa upande waka yaani wanaoamin ndiyo msioamini siyo lazima kuchangia. Kifupi anataka mchango wa wale wanaoamin tu
Hapa ni Open forum.

Ukisha weka mada yako hapa, Regardless of what you want, kila mtu atachangia atakavyo.

Huwezi kuweka kitu Public halafu useme ni kwa wanao amini tu.

Yani hapo unataka privacy kwenye public forum.

Unaposti kitu kwenye public halafu unataka privacy ya wachache tu.

Huko nikutofikiri sawasawa.
 
Kila kitu kina asili yake au chanzo ....kwa wanaobisha uwepo wa mungu ..watengeneze dunia artificial au roho
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Uwezo wako wa kufikiria upo Chini sana...Yani Muumbaji wa Kitu na yeye unataka awe kaona sehemu ili aigilizie...Wakati yeye ndio Muumbaji( Creator)
 
Kiranga una ID ngapi jamaa? na zote umezitengeneza kwa ajili ya kupinga uwepo wa mungu
Mimi sio Kiranga.

Tatizo lenu mmeshakariri kwamba anayepaswa kupinga uwepo wa huyo Mungu ni Kiranga.

Akitokea mtu mwingine mnaona ni Kiranga huyohuyo.

Kwamba Jamii forums nzima Kiranga pekee ndio mkana Mungu..😄
 
Kama wewe sio kiranga basi una kiranga kikali
 
Unajiona uko smart sana kijana utakayebaki mifupa miaka 100 ijayo. Umeshiba na una nguvu ya kumchallenge MUNGU mwenyewe kabisa.

Unachokifanya kinadhihirisha ufinyu wa fikra na upeo hafifu kabisa wa mambo!

Ni heri ukaacha kushiriki mijadala kama hii ikiwa tu hata pa kuanzia huna ( yaani hujui ya kwamba MUNGU yupo). Unaanika ubutu halisi wa mawazo hasi yasiyopenda kujifunza.

Kama hujui kitu acha kukisemea kuliko kuja na deceptive comments kama hizi.
Acha kututisha thibitisha
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini

Aliyetengeneza simu aliona wapi?
 
Mungu alituumba kwa mfano wake, basi moja kwa moja dunia aliitengeza kwa mfano wa makazi yake huko anakoishi yy na malaika huko mbinguni.....
 
Mungu ameumba binadamu na katika hao wamebuni vitu ambavyo hawakuwa wameviona sehemu nyingine yoyote hapo kabda
Sasa mashaka yako ni yapi kuhusu uwezo wa Mungu kuiumba dunia

"Ndiye aliyezifanya nyota angani:
Dubu, Orioni, Kilimia, na nyota za kusini

Ndiye atendaye makuu yasiyoeleweka

Mambo ya ajabu yasiyo na idadi

Pata kufahamu dubu, Orioni, Kilimia na nyota za kusini ni vitu gani ili uone kwamba Mungu ni zaidi ya akili zetu zinavyoweza kumtafsiri
na dunia kwake ni kama tu tone la maji
 
Mambo ni mengi sana ya kujiuliza. Wanadai kama ulikuwa mwema ukifa unaenda mbinguni. Lakin hapo hapo kuna concept kuwa mwisho wa dunia tutafufuliwa wote na kupewa hukumu. Sasa walio mbunguni watakuja tena duniani au likoje hili!
wapi imeandikwa mtu akifa anaenda mbinguni
nyie ndo mnafanya kina kirangajr waseme hakuna Mungu. mnaongelea vitu havipo
 
Hakuna wa kukupangia lakini tumia akili pia, huyu anawauliza wale wa upande waka yaani wanaoamin ndiyo msioamini siyo lazima kuchangia. Kifupi anataka mchango wa wale wanaoamin tu
Kama ni hivyo ni! aende kanisani au msikiti hili jarida la mada na uhuru kutoa maoni, kwa wote.?
 
Back
Top Bottom