Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Umeshasema "Mfano mtu" Sasa unamlinganisha Mungu na mtu? Hayo unayoyajua na kuyaamini wewe yapo kwenye dimension zako binadamu, sio dimension za Mungu.Yapo mengi usiyoyafahamu wala kuweza kufahamu!
 
Hata nyie kusema ulimwengu uliumbwa ni maneno tu.
Kauli hii inathibitisha wazi huwezi kuthibitisha hoja yako kwamba ulimwengu ulikuepo milele,.. na ndiyo maana umeamua kujifananisha na wanaosema ulimwengu uliumbwa.

Kafanye tafiti juu ya hoja yako,. ukipata uthibitisho lete.
 
Hata nyie waamini Mungu hamuwezi kuthibitisha kwamba ulimwengu uliumbwa na huyo Mungu kwa hiyo swala la kusema kwamba ulimwengu uliumbwa bado pia halina uthibitisho.
 
Hata nyie waamini Mungu hamuwezi kuthibitisha kwamba ulimwengu uliumbwa na huyo Mungu kwa hiyo swala la kusema kwamba ulimwengu uliumbwa bado pia halina uthibitisho.
Kama ni hivyo,..bora useme kwamba hujui mechanism iliyotumika mpaka ulimwengu ukawepo,.....kuliko kuwaambia watu kila siku humu kwamba Ulimwengu haujaumbwa bali ulikuepo milele...

Ukisema moja kwa moja Ulimwengu haujaumbwa maana yake una uhakika 100% haujaumbwa...Hivyo utapaswa kuleta ushahidi,..Lakini ukisema "hujui" unaacha nafasi kwamba siku moja nikipata elimu juu ya mechanism iliyotumika mpaka ulimwengu ukawepo ndiyo nitahitimisha na nitakua na uhakika kama umeumbwa ama la.

NB: Waamini Mungu hatuna jukumu la kuthibitisha kama Dunia iliumbwa ama la....labda kama wewe haujui nini maana ya Imani......Faith is for something you can't see, hear, touch, or feel but that logically makes sense!
 
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.

Ukweli hauendani na imani, Hivyo ukisema Ulimwengu uliumbwa kwa imani automatically ni uongo.
 
Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.

Ukweli hauendani na imani, Hivyo ukisema Ulimwengu uliumbwa kwa imani automatically ni uongo.
Mbona hakuna Mtu aliyesema ulimwengu umeumbwa kwa imani..., au umemaanisha nini hapa?

Nimalizie kwa kusema kwamba..,Si kila imani ni uongo kama unavyodai bali zipo imani ambazo kwenye hali na muda sahihi zinathibitishika na kuwa Hakika kabisa na ipo mifano isiyohesabika juu ya hilo.
 
Mpaka pale imani hiyo itakapo thibitishika ndipo itakuwa ukweli.

Vinginevyo imani bila uthibitisho ni uongo.
 
Turudi katika perspective ya religion scriptures.

"Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na ardhi."

At the same time, vitabu vinadai Mungu ni wa milele yani yupo siku zote hata kabla ya huo uumbaji.

Lakini Vitabu havijaeleza Mungu alikuwa eneo lipi wakati akifanya huo uumbaji.

Na hilo eneo liliumbwa na nani?

Na kama hilo eneo liliumbwa, je ni sahihi kusema mbingu na ardhi ndio uumbaji wa mwanzo?

Unaweza kutusaidia majibu ya hayo maswali?
Ndugu, unapaswa kuelewa maana ya maneno yaliyotumiwa kwenye Biblia. Mfano neno "Mbingu" kwenye Biblia lina maana zaidi ya moja na hiyo ni kutokana na tafsiri iliyofanyika kutoka original manuscripts za Agano la kale zilizoandikwa kwa Kiebrania kwenda lugha ya Kiyunani na lugha zingine.

Mbingu inamaanisha;
  • anga (atmosphere)
  • Mfumo wa jua (solar system)
  • ulimwengu (the universe)
  • Mbinguni makao ya MUNGU ( Heaven)

"Hapo mwanzo MUNGU aliumba mbingu na nchi". Sentensi hii haizungumzii "mwanzo wa MUNGU", bali inazungumzia "mwanzo wa uumbaji" wa ulimwengu.

Neno mbingu katika hiyo sentensi linamaanisha anga (atmosphere) na nchi ni dunia. Biblia katika kitabu cha Mwanzo inazungumzia mwanzo wa uumbwaji wa ulimwengu (the universe including our solar system).

Biblia haizungumzii uumbwaji wa makao ya MUNGU ambayo ni "Mbinguni" (Heaven).

Unapaswa kufahamu kuwa Mbinguni (heaven) sio sehemu ya Ulimwengu (the universe). The heaven is not part of the universe. Mbinguni ni nje ya Ulimwengu, Yes, this will suprise you, lakini ukisoma Biblia utaona kuna mahali imeandikwa; 2 Wakorintho 12:2-4

2" Namfahamu mtu aliyekuwa ndani ya Kristo ambaye miaka kumi na minne iliyopita alijikuta katika mbingu ya tatu. Kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 3 Na ninafahamu ya kuwa huyu mtu alijikuta yuko Paradiso, kama alikuwa katika mwili au katika roho mimi sijui, Mungu anajua. 4 Naye alisikia mambo ambayo hayawezi kusimuliwa, ambayo mtu hawezi kuyatamka."

Mbingu ya tatu ni ipi?

Kama kuna "mbingu ya Tatu" basi ni dhahiri kuwa ipo mbingu ya kwanza na ya pili.

Mbingu ya kwanza ni "anga" au atmosphere.
Mbingu ya pili ni "ulimwengu" au the universe with all its galaxies, planets, stars, comets, asteroids, moons etc.
Mbingu ya tatu ndio "Mbinguni" makao ya MUNGU au heaven.

Mbingu ya tatu iko mbali sana na mbingu ya kwanza na ya pili. Kwa kifupi "Mbingu ya tatu" sio sehemu ya ulimwengu huu (the universe).

Biblia haisemi Mbingu ya tatu iliumbwa lini. Biblia inatuambia kuna mambo ni siri, siri hiyo anaijua MUNGU mwenyewe na kuna mambo ameyafanya kuwa siri mpaka atakapoamua kuyaweka hadharani Yeye mwenyewe.

Soma Kumbukumbu la Torati 29:29

"Mambo ya siri ni ya Bwana, Mungu wetu; lakini mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu milele, ili tuyafanye maneno yote ya sheria hii".

"Yaliyofunuliwa" ndiyo hayo yote yaliyoandikwa kwenye vitabu vya Biblia. Ambayo hayajaandikwa kama ni lini "Mbingu ya tatu" iliumbwa au MUNGU alikuwa anaishi wapi kabla ya kuumba makao yake, hayo yote ni SIRI.

Na MUNGU amefanya kuwa siri sababu hata kama angetufunulia bado yasingetusaidia lolote.

Yale yenyewe ambayo MUNGU aliona yanafaa tuyajue ili yatusaidie KUMTII na kuishi kama apendavyo, ametufunulia, yameandikwa, ametufundisha, lakini tumeshindwa kuyashika. Tunahangaika kutafuta yale yasiyokuwa na faida kwetu.

Tumeshindwa kuzishika Amri za MUNGU, tunahangaika kutafuta SIRI za MUNGU.

Mafarisayo walipomuuliza BWANA YESU KRISTO awaonyeshe ishara itokayo Mbinguni, alisema hivi;
"Kizazi kiovu na cha uzinzi kinatafuta ishara, lakini hakitapewa ishara yoyote isipokuwa ishara ya Yona.” Yesu akawaacha, akaenda zake.
 
"Hapo mwanzo MUNGU aliumba mbingu na nchi". Sentensi hii haizungumzii "mwanzo wa MUNGU", bali inazungumzia "mwanzo wa uumbaji" wa ulimwengu.
Najua sentensi hiyo haizungumzii mwanzo wa Mungu.

Nachotaka mimi kujua kabla ya Mungu kuanza kufanya huo uumbaji, yeye alikuwa akiishi wapi au makazi yake yalikuwa wapi?

Kwasababu yeye ni wa milele alikuwepo tangu na tangu. Sasa kama saizi vitabu vya dini vinadai makazi ya Mungu yapo mbinguni je kabla ya mbingu na ardhi havijaumbwa yeye alikuwa wapi?

Na hapo alipokuwa paliumbwa na nani?
 
Neno mbingu katika hiyo sentensi linamaanisha anga (atmosphere) na nchi ni dunia. Biblia katika kitabu cha Mwanzo inazungumzia mwanzo wa uumbwaji wa ulimwengu (the universe including our solar system).
Concerning yangu mimi ni kujua mazingira gani aliyokuwepo Mungu kabla ya uumbaji.

Yani aliumba huu ulimwengu akiwa wapi, kwasababu logic inakataa kufikiri kuwa Mungu aliumba ulimwengu akiwa ndani ya ulimwengu.

Hapo alipokuwa kabla ya huo uumbaji ndio mimi napopataka, ni wapi?
 
Dunia haijawahi kutokuwepo kwa sababu hakuna uthibitisho wowote ule unao onyesha kwamba Dunia haikuwepo kisha ikawepo.

Yani hakuna wakati wowote ule ambao imethibitishika kwamba Dunia haikuwepo kisha ikawepo.

Kila mtu amezaliwa ndani ya dunia na kuikuta tayari ipo.

Hakuna binadamu aliyezaliwa nje ya dunia halafu akaona dunia ikiumbwa.
Wakati anaona dunia ikiumbwa yeye akuwa kakaa kwa Mangi au wapi?
 
Mpaka pale imani hiyo itakapo thibitishika ndipo itakuwa ukweli.

Vinginevyo imani bila uthibitisho ni uongo.
Kwahiyo wewe ile imani yako kwamba ulimwengu ulikuepo tu milele na haujaumbwa ni uongo?

Maana umeshindwa kuthibitisha.

NB:- Hiyo kauli kwamba imani mpaka pale itakapothibitishika ndiyo itakua kweli,..inakuonyesha wazi kwamba imani hiyo ilikua kweli from the start na ndiyo maana mwishoni baada ya kuwa kwenye hali na wakati sahihi imeweza kuthibitishika.

Imani ya uongo kamwe haiwezi kuthibitishika,..so kuanzia mwanzo mpaka mwisho imani hiyo itabaki kuwa ya uongo!
 
Najua sentensi hiyo haizungumzii mwanzo wa Mungu.

Nachotaka mimi kujua kabla ya Mungu kuanza kufanya huo uumbaji, yeye alikuwa akiishi wapi au makazi yake yalikuwa wapi?

Kwasababu yeye ni wa milele alikuwepo tangu na tangu. Sasa kama saizi vitabu vya dini vinadai makazi ya Mungu yapo mbinguni je kabla ya mbingu na ardhi havijaumbwa yeye alikuwa wapi?

Na hapo alipokuwa paliumbwa na nani?
Nimekujibu hili swali lako. Soma vizuri utaona jibu lake
 
Concerning yangu mimi ni kujua mazingira gani aliyokuwepo Mungu kabla ya uumbaji.

Yani aliumba huu ulimwengu akiwa wapi, kwasababu logic inakataa kufikiri kuwa Mungu aliumba ulimwengu akiwa ndani ya ulimwengu.

Hapo alipokuwa kabla ya huo uumbaji ndio mimi napopataka, ni wapi?
Hata hili pia nimeshakujibu. Tatizo lako husomi reply kwa kutulia.
 
Back
Top Bottom