Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Ila kuthibitisha kama Dunia ilikuepo milele ndiyo huwezi?
Hakuna wakati wowote ule ambapo dunia haikuwepo kisha ikawepo.

Huu ni uthibitisho tosha dunia ilikuwepo.

Ukija na uthibitisho kwamba Dunia iliumbwa na ikathibitika ni kweli basi utaweza kuni prove wrong kwamba dunia ilikuwepo tu.
Kama unaweza kuthibitisha..fanya hivyo ili mjadala uwe mfupi.
Sasa wewe huwezi kuthibitisha dunia iliumbwa halafu unakataa kwamba dunia ilikuwepo tu.

Sasa unataka ni nini?
 
Hakuna kitu kinaitwa "kilikuwepo" kwenye hii universe apart from God himself.

Hicho kisayansi cha nature kinachokusumbua kichwa mimi nna idea nacho kuliko hata wewe hapo.

Labda Kiranga pekee ndiyo anaweza kuongea kuhusu hilo ndiyo nikamwelewa ila siyo wewe ambae hoja zako ni nyepesi sana kama uji wa mtoto
Kiranga ni kilaza hanaga hoja ya msingi
 
Ukweli simple.

Mpaka sasa hakuna mtu aliyethibitisha Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote yupo.

Kwa nini?

Kwa sababu hayupo.

Mtu yeyote anabisha?

Kuni prove wrong anatakiwa kufanya kitu kimoja tu.

Athibitishe Mungu huyo yupo.
 
Wewe thibitisha hayupo
 
Kabla ya kuthibitisha afunike vitabu vyote aje km alivyokuja mikono mitupu asije na Akili za wazazi wake aje na Akili zake
 
Hakuna wakati wowote ule ambapo dunia haikuwepo kisha ikawepo.
Thibitisha kauli hii,..la sivyo utaonekana unaongea tu.

Unasema hakuna wakati wowote ule ambapo Dunia haikuwepo....una uhakika na hilo? Thibitisha.

Mtu akija na kusema kwamba Infropreneur hakuwahi kutokuepo...Je, unadhani tutamuamini kirahisi bila ya kutupa uthibitisho?
 
Wewe thibitisha hayupo
Hivi anaye takiwa kuthibitisha kitu kipo ni yule anayesema kipo au ambaye anasema hakipo?

Ukisema kitu kipo ina maana unajua na una uthibitisho wa uhakika kuwepo kwa hicho kitu ndio maana umesema kipo.

Kitu ambacho hakipo, Hakithibitishiki kwa namna yoyote ile kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.

Una elewa hilo?
 
Kabla ya kuthibitisha afunike vitabu vyote aje km alivyokuja mikono mitupu asije na Akili za wazazi wake aje na Akili zake
Kwangu sizuii kuja na vitabu ila vitabu vitapimwa kimantiki, hakutakuwa na logical fallacy ya "argument from authority" kwamba kitu ni kweli kwa sababu kitabu kimesema.

Vitabu vitaangaliwa mantiki yake, penye mantiki, vitakubalika, ambapo hapana mantiki, vitakataliwa.

Or rather.

Sitaki kuvikubali vitabu kwa sababu ni vitabu tu, na pia, sitaki kuvikataa vitabu kwa sababu ni vitabu tu, nataka kuangalia mantiki ya kinachosemwa bila kujali kama kimetoka kwenye kitabu au la.
 
Hivi anaye takiwa kuthibitisha kitu kipo ni yule anayesema kipo au ambaye anasema hakipo?

Ukisema kitu kipo ina maana unajua na una uthibitisho wa uhakika kuwepo kwa hicho kitu ndio maana umesema kipo.

Kitu ambacho hakipo, Hakithibitishiki kwa namna yoyote ile kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika kipo.

Una elewa hilo?
Wote wanatakiwa kuthibitisha

Umesomaga hesabu? Advanced maths? Unaweza thibitisha kama kitu sio sahihi unless na wewe elimu yako ni H kunani

Kusema kipo au hakipo ni 100% certain... sijui ndio hatakiwi kuthibitisha
 
Kwangu sizuii kuja na vitabu ila vitabu vitapimwa kimantiki, hakutakuwa na logical fallacy ya "argument from aithority" kwamba kitu ni kweli kwa sababu kitabu kimesema.

Vitabu vitaangaliwa mantikibyake, penye mantiki, vitakubakika, ambapo hapana mantiki, vitakataliwa.

Sotaki kuvikubali vitabu kwa sababu ni vitabu tu, na pia, sitaki kuvikataa vitabu kwa sababu ni vitabu tu, nataka kuangalia mantiki ya kinachosemwa bila kujali kama kimetoka kwenye kitabu au la.
Waambie wasije na Vitabu na Wewe weka Vitabu pembeni alafu uthibitisho uwepo bila kufungua Vitabu
 
Thibitisha kauli hii,..la sivyo utaonekana unaongea tu.

Unasema hakuna wakati wowote ule ambapo Dunia haikuwepo....una uhakika na hilo? Thibitisha.

Mtu akija na kusema kwamba Infropreneur hakuwahi kutokuepo...Je, unadhani tutamuamini kirahisi bila ya kutupa uthibitisho?
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika, kuhisika na kupimika.

Ulimwengu ulikuwepo na unapimika ulikuwepo kwa evidences mbalimbali kama time na space.

Ulimwengu upo ndani ya time na space na unapimika kupitia vitu hivi.

Hata infropreneur nipo ndani ya time na space na hata kwa wakati ujao wakihitaji kujua uwepo wangu watarejea kwenye time ambayo infropreneur nili exist...
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Ww ulipomtongoza dem wako uli refer kwa dem yupi
 
Kwan yule aliyebuni jengo lililowavutia wengine Ali refer kwa nan
Mambo ya kuwaza kwa kutumia F yako ya mathematics ndo madhara yake hayo
 
Waambie wasije na Vitabu na Wewe weka Vitabu pembeni alafu uthibitisho uwepo bila kufungua Vitabu

Kwa nini unanipangia cha kuwaambia?

Kwa nini unakataa vitabu?

Kataa hoja, usikatae kitabu.

Kwa sababu hata kitabu kibaya kinaweza kuwa na hoja nzuri.
 
Wote wanatakiwa kuthibitisha
Kama kitu sidai kipo ila wewe ndiye unayedai kipo, Uta takaje mimi ni kuthibitishie madai yako?
Umesomaga hesabu? Advanced maths? Unaweza thibitisha kama kitu sio sahihi unless na wewe elimu yako ni H kunani

Kusema kipo au hakipo ni 100% certain... sijui ndio hatakiwi kuthibitisha
Ukisema kitu kipo unatakiwa wewe ndio uthibitishe kipo, Kama huwezi kuthibitisha kipo ni kwamba kitu hicho hakipo.
 
Mawazo ndo yaendesha dunia. Ndio maana ubora wa mawazo yako ndio ubora wa maisha yako.

Mbona hujasema gunduzi kubwa waliona wapi gari, ndege, meli, simu, bulb, umeme

Yote ni mawazo. Mungu ni roho na alitumia neno kuunda dunia kwa kuliamrisha neno.

Ndio maana neno linaweza kuwa silaha ya kuponya au kuangamiza binadamu.
 
Unajuaje mawazo yanaendesha dunia? Mawazo ya nani?

Dunia inavyozunguka jua mawazo ndiyo yanaifanya izunguke jua?
 
Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika, kuhisika na kupimika.

Ulimwengu ulikuwepo na unapimika ulikuwepo kwa evidences mbalimbali kama time na space.

Ulimwengu upo ndani ya time na space na unapimika kupitia vitu hivi.
Vizuri,..Kwahiyo kwa kutumia time na space kama ulivyosema,..Je, Dunia ilikuepo milele?

Hata infropreneur nipo ndani ya time na space na hata kwa wakati ujao wakihitaji kujua uwepo wangu watarejea kwenye time ambayo infropreneur nili exist...
Na,Je kwa wakati uliopita wakipima watagundua Infropreneur ulikuepo milele au kuna wakati hukuwepo?

Yaani wewe ulikuepo milele au kuna wakati hukuepo?
 
Back
Top Bottom