Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Upo JF ndio maana una uthibitisho kwamba upo na unaweza kujitetea mwenyewe upo

Sasa wewe unahangaika kumuongelea Mungu ambaye hawezi na hajawahi kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo.

Huoni kwamba una mtetea na kumuongelea Mungu Mdhaifu ambaye hayupo na Kashindwa kuja kujiongelea mwenyewe na kujitetea?
Mungu asajitetea mbona kupitia vitabu vyake

Unachosahau mkuu ni kwamba Mungu anajiongelea mwenyewe tena kwenye vitabu
 
Hakuna uthibitisho wowote ule unao thibitisha umri wa Dunia.

Hivyo kusema dunia ina umri ni madai tu yasiyo na uthibitisho.

Kama kila kitu lazima kiwe na starting point mbona huyo Mungu mna mu exclude kuwa na starting point?

Kama Mungu hahitaji kuwa na starting point, kwa nini unalazimisha dunia iwe na starting point?
Mbona unahamisha mada sasa?

ulisema Dunia ilikuepo milele,...kisha ukasema Vilivyopo ndani ya Dunia ndiyo vina umri....au sio wewe uliyesema hivyo?

Ndiyo nikakuelewesha kwamba ukishasema kitu kina umri fulani,..that means kitu hicho kina starting point, au hujui kuhusu hili?

ili uelewe usihamishe mada,...ukiruka ruka utatoka bila kuelewa kitu hapa.
 
Mada inahusu nini?

Mada inahusu Mungu.

Wewe ndiye unajaribu kuhamisha mada.
 
Mungu asajitetea mbona kupitia vitabu vyake

Unachosahau mkuu ni kwamba Mungu anajiongelea mwenyewe tena kwenye vitabu
Kama huyo Mungu anajiongelea mwenyewe kwenye vitabu, Mnacho hangaika kumhubiri na kumuelezea kila siku ni nini?

Mnacho hangaika kuja hapa kumtetea ni nini?

Mbona huyo Mungu ameshindwa kuja hapa kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo?

Kwa nini huyo Mungu hatoki huko vitabuni anako jielezea kwamba yupo, Aje hapa mwenyewe ajiongelee na kujidhihirisha yupo?
 
Surah Al-Baqarah (2:117):

"The Originator of the heavens and the earth. When He decrees a matter, He only says to it, 'Be,' and it is."

Surah Az-Zumar (39:62):

"Allah is the Creator of all things, and He is, over all things, Disposer of affairs".

So., hapo unaona wazi kwamba sio tu dunia, bali Mungu ndiye Originator wa kila kitu yaani Dunia na Ulimwengu kwa ujumla.

Ahsante na karibu kwa mtazamo tofauti.
Ulichokiandika Umekisoma kweli??
Na umeelewa Swali langu..

Yeah kweli Kuna Aya Nyingi kwenye Biblia na Kwenye Quran na hata kwenyr Vitabu vingine vinavyosema kaumba Dunia na Mbingu...
Na kila kitu kilichomo Humo...

Lakini usisahau kwamba Jupiter Haipo ndani ya Dunia..

Na mars sio Miongoni mwa Dunia..

Bora ungenipa Aya inayozungumzia Buruji..
Japo buruji ina maana nyingi ukiacha Cerestial bodies..

Hakuna Dunia/World ni Tofauti na Universe ambayo unahusisha Sola system mbalimbali..

So nataka aya inaonyesha kaumbe Ulimwengu na malimwengu mengine..

Tusifanye Siasa twende kwenye Facts
 
Kama huyo Mungu anajiongelea mwenyewe kwenye vitabu, Mnacho hangaika kumhubiri na kumuelezea kila siku ni nini?

Mnacho hangaika kuja hapa kumtetea ni nini?

Mbona huyo Mungu ameshindwa kuja hapa kujidhihirisha mwenyewe kwamba yupo?

Kwa nini huyo Mungu hatoki huko vitabuni anako jielezea kwamba yupo, Aje hapa mwenyewe ajiongelee na kujidhihirisha yupo?
Mimi nishawahi kuja kwako kujidhihirisha kama nipo? Si unasoma comments zangu tu?
 
Nimegundua uelewa wako ni mdogo sana. Unapenda kubishana bila kujua unataka nini
Hapana, wewe ndiye huelewi kuwa dunia inajiendesha yenyewe bila kujali wanadamu wanataka nini.

Mnaposema mawazo ya wanadamu ndiyo yanaendesha dunia mnamaanisha nini?

Wanadamu wote wakifa, dunia itaendelea kuzunguka jua.

Dunia haizunguki jua kwa sababu ya mawazo ya wanadamu.

Unabisha?
 
All is in the mind of the ALL,and this Universe is just the mental creation of the ALL,and that ALL is GOD!
 
Ulichokiandika Umekisoma kweli??
Na umeelewa Swali langu..

Yeah kweli Kuna Aya Nyingi kwenye Biblia na Kwenye Quran na hata kwenyr Vitabu vingine vinavyosema kaumba Dunia na Mbingu...
Na kila kitu kilichomo Humo...

Lakini usisahau kwamba Jupiter Haipo ndani ya Dunia..

Na mars sio Miongoni mwa Dunia..

Bora ungenipa Aya inayozungumzia Buruji..
Japo buruji ina maana nyingi ukiacha Cerestial bodies..

Hakuna Dunia/World ni Tofauti na Universe ambayo unahusisha Sola system mbalimbali..

So nataka aya inaonyesha kaumbe Ulimwengu na malimwengu mengine..

Tusifanye Siasa twende kwenye Facts
Mkuu,..Nyota na Sayari zote unazoambiwa zipo fahamu kwamba zipo ndani ya Anga la Dunia.

Then, hapo kwenye hizo verses umeona kwamba Mungu ni ORIGINATOR OF ALL THINGS,...sasa kwanini una exclude Mars na objects nyingine ambazo kimsingi zipo humu humu kwenye anga la dunia na ni sehemu ya Solar system....?
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Kwani wewe huwezi fanya kitu bila desa?
 
Mada inahusu nini?

Mada inahusu Mungu.

Wewe ndiye unajaribu kuhamisha mada.
Mimi sijahamisha mada,...nilikua nakupa shule tu kwamba haupo sahihi kusema Dunia ilikuepo milele wakati ukiambiwa uthibitishe huwezi.

Sasa nadhani hutorudia tena kusema Dunia ilikuepo milele,..mpaka pale utakapopata uthibitisho usio na shaka ndani yake.
 
Hata ninyi hamuwezi kusema Mungu huyo kaumba ulimwengu mpaka pale mtakapo pata uthibitisho usio na shaka.

Kwa hivyo Dunia ipo tu.

No one knows ilianzaje.
 
yaani Mungu aigilizie
huyo sasa kweli atakuwa Mungu
Warumi 4:17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
wakolosai1:16 Kwa kuwa katika yeye vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbinguni na vilivyo juu ya nchi, vinavyoonekana na visivyoonekana; ikiwa ni vitu vya enzi, au usultani, au enzi, au mamlaka; vitu vyote viliumbwa kwa njia yake, na kwa ajili yake.
 
Mkuu,..Nyota na Sayari zote unazoambiwa zipo fahamu kwamba zipo ndani ya Anga la Dunia.

Then, hapo kwenye hizo verses umeona kwamba Mungu ni ORIGINATOR OF ALL THINGS,...sasa kwanini una exclude Mars na objects nyingine ambazo kimsingi zipo humu humu kwenye anga la dunia na ni sehemu ya Solar system....?
Mkuu samahani kidogo, Ulisoma Geography au hata Geophysics??
Au hata Science ya Elimu Ya Msingi??

Hivi kweli kabisa kwamba Kwenye Anga la Dunia Kuwa na Sayari zote..?

Wakati Dunia Ni sayari ya Nne kwa Ukubwa kwenye Solar system means Kuna Sayari zingine ni Kubwa kuliko Dunia..

Halafu unaniambia Kuwa Zipo kwenye Anga la dunia???

Kuna Solar system nyingi ambazo zipo kwenye Galaxies mbalimbali..

Unataka kuniambia kuwa Solar system ya Jua hili letu nayo ipo kwenye Anga la dunia..

Ok sawa Vipi kuhusu Solar system zingine na Galaxy zingine..

Galaxy zote zikiwa Pamoja na system zote zikiwa Pamoja Unafahamu nini Kuhusu Effects of Singulary...
Unafahamu kuhuus Warm holes na Black holes??
 
Mkuu samahani kidogo, Ulisoma Geography au hata Geophysics??
Au hata Science ya Elimu Ya Msingi??
Yeap,. nimesoma hizo nadharia lakini nikahusisha na akili ili kufikia hitimisho..........yaani sijahitimisha kwamba kila nilichosoma ndiyo uhalisia ulivyo 100%.

Hivi kweli kabisa kwamba Kwenye Anga la Dunia Kuwa na Sayari zote..?

Wakati Dunia Ni sayari ya Nne kwa Ukubwa kwenye Solar system means Kuna Sayari zingine ni Kubwa kuliko Dunia..

Halafu unaniambia Kuwa Zipo kwenye Anga la dunia???
Kwanini unaona haiwezekani kwa Sayari na nyota zote kuwa kwenye anga la dunia? ukubwa wa hizo sayari hakuzifanyi sayari na makundi hayo ya nyota kuwa nje ya anga la dunia bali tunaweza tu kusema kwamba kuna sayari na nyota ambazo zipo anga la karibu na anga la mbali la Dunia. yaani kuna ambazo unaweza kuona hata kwa macho na nyingine kwa msaada ya vifaa saidizi kulingana na umbali.
 
Kwa sababu hakuna wakati wowote ule ambao umethibitishwa dunia haikuwepo.
okay vizuri,..mwanzo ulisema Dunia haina umri ila vilivyopo ndani ya dunia ndiyo vina umri.........Sasa nina swali 'Umethibitisha vipi kama Vililivyopo ndani ya Dunia sasa hivi kuna wakati havikuwepo, mpaka ukasema vina umri??

ili tuone kama una consistency kwenye kujenga hoja zako......
 
Level za Mungu ni kubwa sana bwana mdogo. Deal kwanza na level za walimwengu, hao wanaochora ramani za hizo nyumba, magari nk wanapata wapi hayo mawazo? Au nao lazima wawe wameiga sehemu!?

Nadhani utakubaliana na mimi kuwa ni ubunigu right! Sasa huyo aiyebuni ramani na akiamua kujenga kitu alichokibuni bila kuiga popote tumuiteje?
 
Eti wakuu.

Ebu mnieleweshe kidogo kuhusu hili.

Mfano : Mtu anapotaka kujenga nyumba, lazima kuna kuwa na ramani ya nyumba aliyo iona mahali labda akavutiwa nayo na yeye akaenda kujenga ki namna ile.

Je, Mungu wakati anaumba ulimwengu na kila kilichopo (viumbe hai na visivyo hai) na universe ki ujumla, aliona wapi mfano wa huo ulimwengu na vitu vyake hadi akaamua aviumbe kwa namna vilivyoonekana hivi.

Au hakuwa na ramani yeyote na namna uliwengu utakavyokuwa bali alianza tu kuumba ukawa hivyo ulivyo ndiyo hivo.

Kama alishakuwa na ramani tayari, je allitoa wapi, nani aliisanifu hiyo ramani ?

Naomba niishie hapo kwa leo.

NB : hapa nazungumza na wanao amini tu kuwa kuna Mungu, sizungumzi na wasio amini
Ushashiba makande sio
 
Back
Top Bottom