Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Mungu aliona wapi mfano wa ulimwengu ndiyo akauumba hivi?

Unaposema MUNGU aliona wapi mfano wa dunia ndipo akaumba, hivi unamfananisha BWANA MUNGU na Mwanadamu?

Umekosa akili, umekosa adabu kwa MUUMBA wako kiasi unaona hawezi kufanya chochote mpaka kwanza awe ameona?

Na kama mpaka aone kwanza, unataka kusema yupo mwingine aliye mkuu kumzidi YEYE?

Kijana kuwa na adabu kwa MUUMBA wako. Usifikie hatua ya kumdharau MUNGU kuwa hawezi kutenda, hawezi kuumba mpaka awe ameona kwanza.
Asnte umenijibia vyema
 
Thibitisha haya maneno yako
Unataka uthibitisho kwa kitu ambacho hakipo?

Mimi napinga madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu, Ninyi mnaodai huyo Mungu yupo ndio mnatakiwa mthibitishe madai yenu.

Mkishindwa kuthibitisha madai yenu ya uwepo wa huyo Mungu, Ni kwamba madai yenu ni ya uongo na huyo Mungu mnayedai yupo, Hayupo.
 
Wewe mwenye hoja hiyo, ndio ututhibitishie kwamba hayupo, so thibitisha hilo. Je unaweza kuthibitisha?
 
Wewe mwenye hoja hiyo, ndio ututhibitishie kwamba hayupo, so thibitisha hilo. Je unaweza kuthibitisha?
Huyo Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Huyo Mungu hayupo ndio maana tunahoji uwepo wake.

Ninyi mnaodai huyo Mungu yupo, Hamuwezi na mmeshindwa kuthibitisha uwepo wa huyo Mungu.

Huu ni uthibitisho tosha kwamba Mungu huyo hayupo.

Ukibisha thibitisha uwepo wa huyo Mungu.
 
Bila shaka Post yako hii kwenye page #226 naichukulia ni uthibitisho wako ulioutoa.

Ili twende vizuri kwenye mjadala huu, nakuuliza swali, wewe unaamini katika Sayansi pekee na si uwepo wa Mungu?
 
Bila shaka Post yako hii kwenye page #227 naichukulia ni uthibitisho wako ulioutoa.

Ili twende vizuri kwenye mjadala huu, nakuuliza swali, wewe unaamini katika Sayansi pekee na si uwepo wa Mungu?
Mimi siamini kwenye kuamini.

Sina imani ya aina yeyote ile.
 
Napinga madai yako yanayosema kuna kitu kinaitwa Mungu.

Ndio maana nasema kitu hicho kiitwacho Mungu, Hakipo.
Unafahamu kwamba unavyopinga madai hayo, ni kwamba una uhakika?, na Unafahamu kwamba kuwa na uhakika ni kuamini?
Kama unaamini katika Sayansi, ni vizuri nimejua upo upande gani, na mimi pia naamini katika Sayansi hiyo hiyo ambayo imeumbwa na Mungu.

Sasa tuendelee,

Je unaweza kunithibitishia kwamba hakuna uwepo wa Mungu kisayansi?
 
Unafahamu kwamba unavyopinga madai hayo, ni kwamba una uhakika?, na Unafahamu kwamba kuwa na uhakika ni kuamini?
Uhakika sio suala la kuamini.

Uhakika ni suala la uhakiki.

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho.
Kama unaamini katika Sayansi, ni vizuri nimejua upo upande gani, na mimi pia naamini katika Sayansi hiyo hiyo ambayo imeumbwa na Mungu.
Sayansi haiaminiwi.

Sayansi si imani.

Sayansi ni uchunguzi, utafiti, udadisi na uthibitisho.

Hakuna Mungu aliyeumba sayansi.

Mungu ni Fictional character.
Sasa tuendelee,

Je unaweza kunithibitishia kwamba hakuna uwepo wa Mungu kisayansi?
Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo.
 
Uhakika sio suala la kuamini.

Uhakika ni suala la uhakiki.

Msingi wa imani ni kutokuwa na uhakika wala uthibitisho
Msingi wa imani ni kuwa na uhakika, na uhakika ni kuamini.

Uhakiki ni kupitia au kuchambua jambo fulani ili kujua lina uhakika?

Likishakua na uhakika linaunda imani dhidi ya jambo hilo.
Sayansi haiaminiwi.

Sayansi si imani.

Sayansi ni uchunguzi, utafiti, udadisi na uthibitisho.

Hakuna Mungu aliyeumba sayansi.

Mungu ni Fictional character
Haujui kwamba Sayansi ni uhakika/kuamini katika uchunguzi, utafiti, udadisi na uthibitisho?

Kama kusingekua na uhakika au kuamini katika uchunguzi, utafiti, udadisi na uthibitisho, unafikiri ungekua na uhakika au kuamini katika Sayansi?

Huyo Mungu hayupo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika yupo.

Huyo Mungu hajawahi kuwepo, hayupo na hata uwezekano wa kuwepo kwake Haupo
Haya unayoyasema nithibitishie Kisayansi kwanza kama nilivyokuuliza? Usinijibu kinadharia kwa sababu wewe una uhakika na Sayansi. Thibitisha hakuna uwepo wa Mungu Kisayansi (uchunguzi, utafiti, udadisi na uthibitisho)?

Ukinijibu tu kinadharia au kwa maneno tu, bila kunipa uthibitisho wa Kisayansi, utakua hauna tofauti na mimi ninae amini katika uwepo wa Mungu.
 
Back
Top Bottom