Mungu aliyesubiri wanasayansi wagundue meli ndipo tumjue

Ibn Unuq

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2020
Posts
5,508
Reaction score
10,086
Walisema sisi ni washamba.
Tukaacha ngozi zetu, tukavaa suti.
Tukaacha ngoma, tukavaa saxophone.
Tukaacha majina yetu, tukaitwa Yohana wa Pili.
Ajabu leo Wamasai, Wahamer, na BaTwa waliobaki washamba ndiyo kivutio cha dunia.

Mungu mmoja alitoka Asia,
akapita Ulaya,
akaruka Mediteranea,
akaruka bara zima
akaja kutufundisha kuwa Afrika hatuna Mungu.
Kwa nini asingetua Afrika moja kwa moja bila kusubiri Majahazi ya wanasayansi?

Walikuja na Biblia mkono wa kushoto
na risasi mkono wa kulia.
Tulipofunga macho tukiomba,
walifungua ramani na kugawa ardhi.
Tuliposema Amina,
walikuwa tayari na mkataba wa madini wa miaka isiyo na kikomo.

Tukaambiwa
"Heri kuwa maskini wa moyo",
Wao wakajenga benki.
"Haya Yote ni mavumbi",
Wao wakaanza kuchimba hayo mavumbi kwa excavators.

Wakatuambia tutazame mbinguni, wokovu waja.
Lakini wao waliangalia ardhini, mali zilipo.
Sisi tukarithi mbingu ya nadharia,
wao wakarithi ardhi kwa vitendo.

Majina nayo yakabadilika bhana,
Shimanyi akawa Petro.
Linda akawa Maria.
Kaniki ikaitwa ushenzi,
Suti ya bluu ikaitwa Nguo ya aliyeokoka.

Tulifundishwa
“Mtii mamlaka, maana imewekwa na Mungu.”
Kisha mkoloni akawa ndiyo huyo mtumishi wa Mungu.
Ukigoma, hauipingi serikali, unapinga mipango ya mbinguni hivyo utachomwa kwenye moto mkali.

Watu wetu wakawa washika Biblia,
lakini si washikaji wa hati za ardhi.
Waombaji wa mbinguni,
lakini si warithi wa mashamba.
Waumini wa kweli,
lakini si wamiliki wa chochote.

Makanisa kwasasa yamekuwa kila mita 50,
Kila kona kuna huduma ya kiroho
lakini huduma za kimazingira, kiuchumi, na kisiasa ni uzoefu wa mtu binafsi tu.

Wakasema mbinguni kuna tiketi, Lipeni nauli[sadaka] wakajenga vyumba kwa pesa hizo hizo kisha wakatupangisha hivyo vyumba sisi wenyewe tena.
Wakalima mashamba makubwa halafu wakatulipa pesa hizohizo tulizotoa kama nauli ya mbinguni.

Kwa kifupi,
Tulirithi imani,
tukapoteza ardhi.
Tuliletewa bikira Maria,
tukanyang’anywa mama zetu wa mila na wakunga wa jadi.
Tulipewa mkate wa uzima,
tukanyang’anywa mashamba ya mahindi.

Msije mkasema Kobazi mmesalimika kwenye uzi huu…

Tulilia uhuru,
Tukapewa Uislamu.
Tukapoteza ardhi,
Tukapewa dua za kuondoa uchungu.
Tulipiga magoti,
Wao wakatupiga mihuri ya biashara ya utumwa.

Wakatuchukua kama watumwa,
Wakatupa Qur’an tujifunze kusamehe wanayatufanyia.
Halafu wakatufundisha
“Subira ni fadhila ya waumini.”

Tukafungwa kwenye muda ili tusali sala tano kwa siku na Tukafundishwa kupendana kwa ajili ya Allah.
Tuliuza wake na waume zetu kwa bei ya chumvi, wakatuambia.
Watumwa wenu wapeni haki zao.

Wakasema mahali tunazotoza za ng'ombe 3,4,5...10 si haki wakati zilikuwa zinachochea vijana kutafuta kwa bidii.
Kisha - Wakaoa binti zetu watatu kwa wanne, wakavinjali nao kingono na walijichukulia kiurahisi chini ya kivuli cha Allah anataka mke ndiye apange mali.
Wakawalaghai dada zetu wataje bei za sabuni, wakajichukulia kama kusukuma mlevi mteremkoni.

Wakatuambia tufuate Sunna,
Tukaacha mila zetu.
Tukafundishwa kuvaa kwa mfano wa mji wa Makka,
Tukaambiwaa haramu kuvaa kikoi cha bibi yetu na kuacha wazi kichwa kilichosukwa twende kilioni.

Tulifundishwa kuosha miguu kabla ya swala,
Lakini hatukuwahi kuosha historia yetu ya kunyimwa utu.
Tkafundishwa kujifunika hijjab,
Tukafunika sura zetu.
Lakini hatukufunika makovu ya ukoloni wa kiarabu.

Wakatufundisha kufunga Ramadhan,
Lakini walifungua milango ya Zanzibar ya soko la watumwa ili tusione.
Wakatufundisha kutosengenya,
Lakini wakasema mila zetu ni ushirikina.

Tuliambiwa Qur’an inahifadhi kila kitu,
Tukasahau kumbe ilihifadhi na unyonyaji.
Tukajua aya za adhabu,
Tukasahau historia ya kuadhibiwa.

Tukawa waumini wa kweli,
Lakini si waafrika wa kweli.
Tukavaa joho la ustaarabu,
Lakini ndani tumejazwa hofu ya moto wa Jehanum.

Wakatufundisha maadili ya familia,
Kisha wakazipeleka familia zetu hizohizo kwenye biashara ya utumwa.
Wakatufundisha ndoa halali,
Lakini waliwageuza wasichana wetu wake wa masultani.

Na hata leo,
Tukivaa asili yetu tunaambiwa ni kafir, muasi na mfuasi wa shetani.
Tukicheza ngoma za jadi tunaambiwa ni haramu.

Wakasema dini inaleta uhuru wakajisahaulisha kuwa walitupa uhuru wa kuishi tu akini siyo wa sisi kubaki kuwa sisi.

Uislamu wa Kiarabu na Ukristo wa Ulaya walikuja kwa njia tofauti,
lakini wote walitaka kitu kimoja,
Kutufanya tuwe watu wao, kwa jina la Mungu.

Swali la msingi kwa wote.
Je, Mungu wa kweli anaogopa majina ya asili?
Anaogopa lugha zetu?
Anaona mizimu ya mababu kama uchafu, lakini anaheshimu historia mbaya ya waarabu au wayahudi?

Mungu ambaye anahitaji ubadilike na kuwa mtu mwingine wa nje ambaye si wewe halisi ndio akutambue,
Huyo si Mungu wa kweli.
Huo ni mfumo uliowekwa.

Dini Inayokufundisha utii huku yenyewe haitii mila na tamaduni zako huo ni utii au upendeleo?

​

Tambua kuanzia leo kuwa Mwafrika siyo laana kama tunavyokua tukisikia na kuambiwa bali Uafrika ni nuru na ni nguvu.

Kataa katakata unapoletewa habari za Mungu aliyetumika kama kifuniko cha ukoloni wa kiakili.

Tuna mamilioni ya wafrika wanaoamini kuwa wako huru kwa sababu wamepewa dini huku wakisahau maana kamili ya uhuru.

Uhuru siyo kufanya kilakitu unachokitaka, Uhuru ni kutolazimika kufanya jambo ambalo litakuondolea amani na utulivu.

Je kufanya tu kila unachokitaka bila kujali matokeo kutakupatia amani na utulivu?
Kulazimishwa kufunga na kutoa sadaka ni uhuru?

Hivi kuamini Mungu na dini kwasababu usipofanya hivyo hutakwenda mbinguni bali unatishwa kupelekwa kwenye moto mkali ni uhuru?

kuambiwa ukimuabudu Mungu mali zako zitakua nyingi na maisha yako yatakuwa bora huo ni uhuru?
Au ni kulazimika kufanya kwasababu ya?

Ndiyo maana huwa nasema Afrika haijapata uhuru ila waafrika wachache ndiyo wapo huru.

Swali langu ni moja - Hivi huyu Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, na aliyepo kila mahali kwa nini alisubiri mpaka meli za waarabu na wazungu zivuke bahari, ndipo tumjue?

Ikiwa yuko kila mahali - Je, hakuwa Afrika kabla ya meli kugundulika wakati huo?

Mimi ni Agnostiki Mstoiki.
Ibn Unuq
 
Walisema sisi ni washamba.
Tukaacha ngozi zetu, tukavaa suti.
Tukaacha ngoma, tukavaa saxophone.
Tukaacha majina yetu, tukaitwa “Yohana wa Pili.”
Ajabu leo Wamasai, Wahamer, na BaTwa waliobaki washamba ndiyo kivutio cha dunia.

Mungu mmoja alitoka Asia,
akapita Ulaya,
akaruka Mediteranea,
akaruka bara zima
akaja kutufundisha kuwa Afrika hatuna Mungu.
Kwa nini asingetua Afrika moja kwa moja bila kusubiri Majahazi ya wanasayansi?

Walikuja na Biblia mkono wa kushoto
na risasi mkono wa kulia.
Tulipofunga macho tukiomba,
walifungua ramani na kugawa ardhi.
Tuliposema Amina,
walikuwa tayari na mkataba wa madini wa miaka isiyo na kikomo.

Tukaambiwa
"Heri kuwa maskini wa moyo",
Wao wakajenga benki.
"Haya Yote ni mavumbi",
Wao wakaanza kuchimba hayo mavumbi kwa excavator.

Wakatuambia tutazame mbinguni, wokovu waja.
Lakini wao waliangalia ardhini, mali zilipo.
Sisi tukarithi mbingu ya nadharia,
wao wakarithi ardhi kwa vitendo.

Majina nayo yakabadilika bhana,
Shimanyi akawa Petro.
Linda akawa Maria.
Kaniki ikaitwa ushenzi,
Suti ya bluu ikaitwa Nguo ya aliyeokoka.

Tulifundishwa
“Mtii mamlaka, maana imewekwa na Mungu.”
Kisha mkoloni akawa ndiyo huyo mtumishi wa Mungu.
Ukigoma, haumpingi serikali – unapinga mipango ya mbinguni hivyo utachomwa kwenye moto mkali.

Watu wetu wakawa washika Biblia,
lakini si washika hati za ardhi.
Waombaji wa mbinguni,
lakini si warithi wa mashamba.
Waumini wa kweli,
lakini si wamiliki wa chochote.

Makanisa yakawa kila mita 50.
Kila kona kuna huduma ya kiroho
lakini huduma za kimazingira, kiuchumi, na kisiasa ni uzoefu wa mtu binafsi tu.

Wakasema mbinguni kuna tiketi, Lipeni nauli[sadaka] kisha wakajenga vyumba kwa pesa hizo hizo kisha wakatupangisha sisi wenyewe tena.
Wakalima mashamba makubwa halafu wakatulipa pesa tulizozitoa za nauli ya mbinguni.

Kwa kifupi,
Tulirithi imani,
tukapoteza ardhi.
Tulipewa bikira Maria,
tukanyang’anywa mama zetu wa mila na wakunga wa jadi.
Tulipewa mkate wa uzima,
tukanyang’anywa mashamba ya mahindi.

Msije mkasema Kobazi mmesalimika kwenye uzi huu…

Tulilia uhuru,
Tukapewa Uislamu.
Tukapoteza ardhi,
Tukapewa dua za kuondoa uchungu.
Tulipiga magoti,
Wao wakatupiga mihuri ya biashara ya utumwa.

Wakatuchukua kama watumwa,
Wakatupa Qur’an tujifunze kusamehe wanayatufanyia.
Halaf wakatufundisha
“Subira ni fadhila ya waumini.”

Tukafungwa kwenye muda ili tusali sala tano kwa siku na Tukafundishwa kupendana kwa ajili ya Allah.
Tuliuza wake na waume zetu kwa bei ya chumvi, wakatuambia.
Watumwa wenu wapeni haki zao.

Wakasema mahali tunazotoza za ng'ombe 3,4,5...10 si haki wakati zilikuwa zinachochea vijana kutafuta kwa bidii.
Kisha - Wakaoa binti zetu watatu kwa wanne, wakavinjali nao kingono na walijichukulia kiurahisi chini ya kivuli cha Allah anataka mke ndiye apange mali.
Wakawalaghai dada zetu wataje bei za sabuni, wakajichukulia kama kusukuma mlevi mteremkoni.

Wakatuambia tufuate Sunna,
Tukaacha mila zetu.
Tukafundishwa kuvaa kwa mfano wa mji wa Makka,
Tukaambiwaa haramu kuvaa kikoi cha bibi yetu na kuacha wazi kichwa kilichosukwa twende kilioni.

Tulifundishwa kuosha miguu kabla ya swala,
Lakini hatukuwahi kuosha historia yetu ya kunyimwa utu.
Tkafundishwa kujifunika hijjab,
Tukafunika sura zetu.
Lakini hatukufunika makovu ya ukoloni wa kiarabu.

Wakatufundisha kufunga Ramadhan,
Lakini walifungua milango ya Zanzibar ya soko la watumwa ili tusione.
Wakatufundisha kutosengenya,
Lakini wakasema mila zetu ni ushirikina.

Tuliambiwa Qur’an inahifadhi kila kitu,
Tukasahau kumbe ilihifadhi na unyonyaji.
Tukajua aya za adhabu,
Tukasahau historia ya kuadhibiwa.

Tukawa waumini wa kweli,
Lakini si waafrika wa kweli.
Tukavaa joho la ustaarabu,
Lakini ndani tumejazwa hofu ya moto wa Jehanum.

Wakatufundisha maadili ya familia,
Kisha wakazipeleka familia zetu hizohizo kwenye biashara ya utumwa.
Wakatufundisha ndoa halali,
Lakini waliwageuza wasichana wetu wake wa masultani.

Na hata leo,
Tukivaa asili yetu tunaambiwa ni kafir, muasi na mfuasi wa shetani.
Tukicheza ngoma za jadi tunaambiwa ni haramu.

Wakasema dini inaleta uhuru wakajisahaulisha kuwa walitupa uhuru wa kuishi tu akini siyo wa sisi kubaki kuwa sisi.

Uislamu wa Kiarabu na Ukristo wa Ulaya walikuja kwa njia tofauti,
lakini wote walitaka kitu kimoja,
Kutufanya tuwe watu wao, kwa jina la Mungu.

Swali la msingi kwa wote:
Je, Mungu wa kweli anaogopa majina ya asili?
Anaogopa lugha zetu?
Anaona mizimu ya mababu kama uchafu, lakini anaheshimu historia mbaya ya waarabu au wayahudi?

Mungu ambaye anahitaji ubadilike na kuwa mtu mwingine wa nje ambaye si wewe halisi ndio akutambue,
Huyo si Mungu wa kweli.
Huyo ni mfumo uliowekwa.

HITIMISHO:​

Tafakari kwanini dini ikufundishe kutii huku yenyewe isipotii mila na desturi zako na kuziharibu? Je huo ni utii?​

Tambua kuanzia leo kuwa Mwafrika siyo laana kama tunavyokua tukisikia na kuambiwa bali Uafrika ni neema, ni nguvu.

Kataa katakata unapoletewa habari za Mungu aliyetumika kama kifuniko cha ukoloni wa kiakili.

Tuna mamilioni ya wafrika wanaoamini kuwa wako huru kwa sababu wamepewa dini huku wakisahau maana kamili ya uhuru.

Uhuru siyo kufanya kilakitu unachokitaka, uunapaswa kukuletea amani na utulivu.
Je kufanya tu kila unachokitaka kutakipatia amani na utulivu?
Je, kuwa mlevi wa kamari ni uhuru?

Uhuru pia ni kutokulazimika kufanya jambo kwa nguvu mfano Usipolazimishwa kupiga kura huo ni uhuru hata usipolazimishwa kuoa ni uhuru ila kuoa sababu umri unaenda siyo uhuru ni kulazimika.

Hivi kuamini Mungu na dini kwasababu usipofanya hivyo hutakwenda mbinguni ni uhuru?

Na kuambiwa ukimuabudu Mungu mali zako zitakua nyingi na maisha yako yatakuwa bora huo ni uhuru?
Au ni kulazimika kufanya kwasababu ya?

Swali langu ni moja - Hivi huyu Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, na aliyepo kila mahali kwa nini alisubiri mpaka meli za waarabu na wazungu zivuke bahari, ndipo tumjue?

Ikiwa yuko kila mahali - Je, hakuwa Afrika kabla ya meli kugundulika wakati huo?

Mimi ni Agnostiki Mstoiki.
Ibn Unuq
Mungu aliye subiri watu wasome utabibu ndo tuwe na afya njema,Mungu aliyesubiri watu wagundue majembe, tractor nk ndo tupate chakula.

Kanuni ya mungu inafanya kazi as a system,bila uwepo wa kitu Fulani kitu Fulani hakiwezi kuwepo au kutokea.

Huwezi kwenda kwenye maombi ya kupata mtoto huku huna mume,hii ndo kanuni ya miujiza ya the so called Supernatural Power

Mwisho ,sio kweli kuwa kabla ya ugunduzi was meli,Africa hatukuwa tukimujua mungu,dhana ya mungu imekuwepo hata kabla ya wazungu na waarabu.

Ushahidi wa dhana hii umejikita kwenye uwepo wa maneno mungu kwa lugha zetu za asili,mfano Kyala kwa kinyakyusa, lyoba/ sebha kwa kisukuma,
 
Mungu aliye subiri watu wasome utabibu ndo tuwe na afya nje,,Mungu aliyesubiri watu wagundue majembe, tractor nk ndo tupate chakula.

Kanuni ya mungu inafanya kazi as a system,bila uwepo wa kitu Fulani kitu Fulani hakiwezi kuwepo au kutokea.

Huwezi kwenda kwenye maombi ya kupata mtoto huku huna mume,hii ndo kanuni ya miujiza ya the so called Supernatural Power
Kama unaweza tumia kanuni tu na usimwamini huyo Mungu hautapata matokea? na shida yake ni nini?
 
Kwa tulipofika wameshatuweza tumesha haribia kiasi kwamba kurudi kwenye misingi yetu ya hasili ni ndoto.

Wamehakikisha their beliefs zimetuingia hadi kwenye nerve systems zetu asilimia 100%.
Kiufupi tuna sema shashooo...!
 
Dini ni upuuzi sana.

Mtume Muhammad alisema:

Siku moja Musa alikwenda kuoga, akaweka nguo zake juu ya jiwe. Ghafula lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza akisema: ‘Ewe jiwe, nguo zangu! Ewe jiwe, nguo zangu!’

Hana akili timamu mtu mzima anayeamini jiwe lilikimbia na nguo za Musa.
 
Mungu aliye subiri watu wasome utabibu ndo tuwe na afya njema,Mungu aliyesubiri watu wagundue majembe, tractor nk ndo tupate chakula.

Kanuni ya mungu inafanya kazi as a system,bila uwepo wa kitu Fulani kitu Fulani hakiwezi kuwepo au kutokea.

Huwezi kwenda kwenye maombi ya kupata mtoto huku huna mume,hii ndo kanuni ya miujiza ya the so called Supernatural Power
Mungu yupi huyo na yuko wapi?
 
Kama unaweza tumia kanuni tu na usimwamini huyo Mungu hautapata matokea? na shida yake ni nini?
Kwa upande wangu hakuna shida,Mimi naamini baada ya creation , Mungu (the supernatural power) alijitenga na ulimwengu,akaacha the so called system ifanye kazi,ndo maana tunaona mauaji na machafuko Kila sehemu,hii yote ni kuwa mungu amejitenga na ulimwengu na kuacha Mfumo ufanye kazu
 
Dini ni upuuzi sana.

Mtume Muhammad alisema:

Siku moja Musa alikwenda kuoga, akaweka nguo zake juu ya jiwe. Ghafula lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza akisema: ‘Ewe jiwe, nguo zangu! Ewe jiwe, nguo zangu!’

Hana akili timamu mtu mzima anayeamini jiwe lilikimbia na nguo za Musa.
Yaani unafundishwa kutolewa ujinga kwa kutumia ujinga.
 
Yona 1:17

“Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona alikuwa katika tumbo la samaki siku tatu, mchana na usiku.”

Mtu mzima na watoto wako unakaa, unaamini binadamu anaweza kukaa ndani ya samaki siku tatu halafu samaki akamtapike huko pwani.!

Akili za kitoto.
 
Back
Top Bottom