Mungu aliyesubiri wanasayansi wagundue meli ndipo tumjue

Walisema sisi ni washamba.
Tukaacha ngozi zetu, tukavaa suti.
Tukaacha ngoma, tukavaa saxophone.
Tukaacha majina yetu, tukaitwa Yohana wa Pili.
Ajabu leo Wamasai, Wahamer, na BaTwa waliobaki washamba ndiyo kivutio cha dunia.

Mungu mmoja alitoka Asia,
akapita Ulaya,
akaruka Mediteranea,
akaruka bara zima
akaja kutufundisha kuwa Afrika hatuna Mungu.
Kwa nini asingetua Afrika moja kwa moja bila kusubiri Majahazi ya wanasayansi?

Walikuja na Biblia mkono wa kushoto
na risasi mkono wa kulia.
Tulipofunga macho tukiomba,
walifungua ramani na kugawa ardhi.
Tuliposema Amina,
walikuwa tayari na mkataba wa madini wa miaka isiyo na kikomo.

Tukaambiwa
"Heri kuwa maskini wa moyo",
Wao wakajenga benki.
"Haya Yote ni mavumbi",
Wao wakaanza kuchimba hayo mavumbi kwa excavators.

Wakatuambia tutazame mbinguni, wokovu waja.
Lakini wao waliangalia ardhini, mali zilipo.
Sisi tukarithi mbingu ya nadharia,
wao wakarithi ardhi kwa vitendo.

Majina nayo yakabadilika bhana,
Shimanyi akawa Petro.
Linda akawa Maria.
Kaniki ikaitwa ushenzi,
Suti ya bluu ikaitwa Nguo ya aliyeokoka.

Tulifundishwa
“Mtii mamlaka, maana imewekwa na Mungu.”
Kisha mkoloni akawa ndiyo huyo mtumishi wa Mungu.
Ukigoma, hauipingi serikali, unapinga mipango ya mbinguni hivyo utachomwa kwenye moto mkali.

Watu wetu wakawa washika Biblia,
lakini si washikaji wa hati za ardhi.
Waombaji wa mbinguni,
lakini si warithi wa mashamba.
Waumini wa kweli,
lakini si wamiliki wa chochote.

Makanisa kwasasa yamekuwa kila mita 50,
Kila kona kuna huduma ya kiroho
lakini huduma za kimazingira, kiuchumi, na kisiasa ni uzoefu wa mtu binafsi tu.

Wakasema mbinguni kuna tiketi, Lipeni nauli[sadaka] wakajenga vyumba kwa pesa hizo hizo kisha wakatupangisha hivyo vyumba sisi wenyewe tena.
Wakalima mashamba makubwa halafu wakatulipa pesa hizohizo tulizotoa kama nauli ya mbinguni.

Kwa kifupi,
Tulirithi imani,
tukapoteza ardhi.
Tuliletewa bikira Maria,
tukanyang’anywa mama zetu wa mila na wakunga wa jadi.
Tulipewa mkate wa uzima,
tukanyang’anywa mashamba ya mahindi.

Msije mkasema Kobazi mmesalimika kwenye uzi huu…

Tulilia uhuru,
Tukapewa Uislamu.
Tukapoteza ardhi,
Tukapewa dua za kuondoa uchungu.
Tulipiga magoti,
Wao wakatupiga mihuri ya biashara ya utumwa.

Wakatuchukua kama watumwa,
Wakatupa Qur’an tujifunze kusamehe wanayatufanyia.
Halafu wakatufundisha
“Subira ni fadhila ya waumini.”

Tukafungwa kwenye muda ili tusali sala tano kwa siku na Tukafundishwa kupendana kwa ajili ya Allah.
Tuliuza wake na waume zetu kwa bei ya chumvi, wakatuambia.
Watumwa wenu wapeni haki zao.

Wakasema mahali tunazotoza za ng'ombe 3,4,5...10 si haki wakati zilikuwa zinachochea vijana kutafuta kwa bidii.
Kisha - Wakaoa binti zetu watatu kwa wanne, wakavinjali nao kingono na walijichukulia kiurahisi chini ya kivuli cha Allah anataka mke ndiye apange mali.
Wakawalaghai dada zetu wataje bei za sabuni, wakajichukulia kama kusukuma mlevi mteremkoni.

Wakatuambia tufuate Sunna,
Tukaacha mila zetu.
Tukafundishwa kuvaa kwa mfano wa mji wa Makka,
Tukaambiwaa haramu kuvaa kikoi cha bibi yetu na kuacha wazi kichwa kilichosukwa twende kilioni.

Tulifundishwa kuosha miguu kabla ya swala,
Lakini hatukuwahi kuosha historia yetu ya kunyimwa utu.
Tkafundishwa kujifunika hijjab,
Tukafunika sura zetu.
Lakini hatukufunika makovu ya ukoloni wa kiarabu.

Wakatufundisha kufunga Ramadhan,
Lakini walifungua milango ya Zanzibar ya soko la watumwa ili tusione.
Wakatufundisha kutosengenya,
Lakini wakasema mila zetu ni ushirikina.

Tuliambiwa Qur’an inahifadhi kila kitu,
Tukasahau kumbe ilihifadhi na unyonyaji.
Tukajua aya za adhabu,
Tukasahau historia ya kuadhibiwa.

Tukawa waumini wa kweli,
Lakini si waafrika wa kweli.
Tukavaa joho la ustaarabu,
Lakini ndani tumejazwa hofu ya moto wa Jehanum.

Wakatufundisha maadili ya familia,
Kisha wakazipeleka familia zetu hizohizo kwenye biashara ya utumwa.
Wakatufundisha ndoa halali,
Lakini waliwageuza wasichana wetu wake wa masultani.

Na hata leo,
Tukivaa asili yetu tunaambiwa ni kafir, muasi na mfuasi wa shetani.
Tukicheza ngoma za jadi tunaambiwa ni haramu.

Wakasema dini inaleta uhuru wakajisahaulisha kuwa walitupa uhuru wa kuishi tu akini siyo wa sisi kubaki kuwa sisi.

Uislamu wa Kiarabu na Ukristo wa Ulaya walikuja kwa njia tofauti,
lakini wote walitaka kitu kimoja,
Kutufanya tuwe watu wao, kwa jina la Mungu.

Swali la msingi kwa wote.
Je, Mungu wa kweli anaogopa majina ya asili?
Anaogopa lugha zetu?
Anaona mizimu ya mababu kama uchafu, lakini anaheshimu historia mbaya ya waarabu au wayahudi?

Mungu ambaye anahitaji ubadilike na kuwa mtu mwingine wa nje ambaye si wewe halisi ndio akutambue,
Huyo si Mungu wa kweli.
Huo ni mfumo uliowekwa.

Dini Inayokufundisha utii huku yenyewe haitii mila na tamaduni zako huo ni utii au upendeleo?

​

Tambua kuanzia leo kuwa Mwafrika siyo laana kama tunavyokua tukisikia na kuambiwa bali Uafrika ni nuru na ni nguvu.

Kataa katakata unapoletewa habari za Mungu aliyetumika kama kifuniko cha ukoloni wa kiakili.

Tuna mamilioni ya wafrika wanaoamini kuwa wako huru kwa sababu wamepewa dini huku wakisahau maana kamili ya uhuru.

Uhuru siyo kufanya kilakitu unachokitaka, Uhuru ni kutolazimika kufanya jambo ambalo litakuondolea amani na utulivu.

Je kufanya tu kila unachokitaka bila kujali matokeo kutakupatia amani na utulivu?
Kulazimishwa kufunga na kutoa sadaka ni uhuru?

Hivi kuamini Mungu na dini kwasababu usipofanya hivyo hutakwenda mbinguni bali unatishwa kupelekwa kwenye moto mkali ni uhuru?

kuambiwa ukimuabudu Mungu mali zako zitakua nyingi na maisha yako yatakuwa bora huo ni uhuru?
Au ni kulazimika kufanya kwasababu ya?

Ndiyo maana huwa nasema Afrika haijapata uhuru ila waafrika wachache ndiyo wapo huru.

Swali langu ni moja - Hivi huyu Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, na aliyepo kila mahali kwa nini alisubiri mpaka meli za waarabu na wazungu zivuke bahari, ndipo tumjue?

Ikiwa yuko kila mahali - Je, hakuwa Afrika kabla ya meli kugundulika wakati huo?

Mimi ni Agnostiki Mstoiki.
Ibn Unuq
Wafia dini nadhani wameisoma hii article nzuri, tataizo akili zao hazina akili.
 
Bado muda mfupi sana, miaka 20-30 ijayo hizi dini zitakua kituko tu wanaoziamini watapungua na wengine kuachana nazo.

Nasema kila siku, haya majengo ya makanisa na misikiti wayaandalie matumizi mengine nnje ya kufanyia ibada za kipuuzi, maana itafika wakati majengo hayo hayatotumika tena either kwa kukosa waumini au kuchakaa kwa kukosa sapoti ya kuyaendeleza, yatabaki kuwa makazi ya popo, nyoka, mbwa na mapaka mwitu.

Ni muda sasa waafrika wengi wanaamka kutoka ktk huo utumwa wa kiakili (Dini) ambao ndio siraha kubwa wanayoitegemea wakoloni kuitawala dunia.

Afrika si huru kama tunavyodanganywa, uhuru tuliopewa ni ule wa kutotumika kinguvukazi na badala yake tukapewa utumwa mbaya kuliko hata wa kutumikishwa kinguvu,.

Kuamini kuwa kuna Mungu ambaye yuko mbinguni na ana mitume wake ambao kati yao hakuna hata mmoja aliyeleta injili Afrika, ardhi ambayo ni kubwa na kongwe kuliko yoyote je huyo Mungu halijui hili?.

Kuamini kuwa watu weupe ndio njia ya ukombozi wa afrika sababu ya kuleta hizo dini zao, huu ni upuuzi mtupu, haiwezekani na haitowezekana Umtumie mtu wa mbali apeleke ujembe sehemu ambayo hata hajulikani, hafananii nayo wala hana uzoefu na sehemu hiyo, je kuwatumia wakoloni kuleta dini Afrika Mungu huyu alishindwa vipi kuwatumia hata mitume wapya afrika ili waeneze hiyo injili yake kwa njia ya amani?

Kiuhalisia dunia ina maelfu/mamilioni ya miaka huku watu wakiishi kwa zaidi ya mamilioni ya miaka bila kumjua wala kumsikia huyo Mungu wa hizi dini, je inawezekana vipi stories za uislamu na ukristo zibase katka time line ya miaka 7000 pekee? Je dini hizi hazijui kuwa kuna jamii zilishakuwepo kwa zaidi ya miaka 200,000 kabla yake,

Vile vile tunafundishwa kuwa watu wote wametokana na huyo adam+eva, je kiuhalisia inawezekana wazungu kuzaa mtu mweusi?, ukitumia akili vizuri huwezi kuwa mfuasi wa hizi ngonjera za dini za kishamba.
 
Ikiwa kweli unaamini Mungu alishatoa miongozo, na mkombozi atakuja kwa wakati wake, je, si unajidanganya kwa kutulia na kuzembea ukijificha nyuma ya ahadi zisizo na tarehe?

Je, hauoni kuwa uvivu wa wanaadamu na kutochukua hatua ndio uliowapa hawa madhalimu ujasiri wa kuuza ardhi zenu na kuwafanya waishi kama wanyama?

Nani atawajibika kwa upotevu huu, wale waliouza babu zetu au nyinyi mliokaa kimya mkimsubiri huyo mkombozi mlioahidiwa na watesaji wa babu zetu?
Al-hamdulillah Subra Ndo Nguzo Kuu.
Hamna Alie Mzembe Bali Wale wanaontufunza Kuwafata Na Sio Kutufunza Tujiongoze Kama Allah. Atakavyo Wao Wanapindisha Hivyo.
Tuwe Na Subra Usije Mkufuru Aliekuumba.
Kwa Kuona Hajiwezi. Kumbuka pia.
Bado Hujafikia Kipindi Kigumu Alichokipitia Mussa (A.S)
Hivyo Mipaka Izingatiwe.
Allah Hakumuagiza Mtu Wakumnyanyasa Mwenzie.
Ungekuwa Hivyo Asinge Tupa Ujirani Wakaribu Sana.
Yaan Unaambiwa Ujirani Ukianzia Kulia kwako.
Nyumba 70, kushoto 70,Mbele 70, nyuma 70.
Je' Leo Iko hivyo?
Kumbuka Zamani Na Sasa.
 
Tuanze na Huyo Mussa uliyemtaja.

Mussa muandishi wa Torati aliwezaje kuandika historia ya maisha yake na kifo chake wakati tayari ameshakufa?
 
Bado muda mfupi sana, miaka 20-30 ijayo hizi dini zitakua kituko tu wanaoziamini watapungua na wengine kuachana nazo.

Nasema kila siku, haya majengo ya makanisa na misikiti wayaandalie matumizi mengine nnje ya kufanyia ibada za kipuuzi, maana itafika wakati majengo hayo hayatotumika tena either kwa kukosa waumini au kuchakaa kwa kukosa sapoti ya kuyaendeleza, yatabaki kuwa makazi ya popo, nyoka, mbwa na mapaka mwitu.

Ni muda sasa waafrika wengi wanaamka kutoka ktk huo utumwa wa kiakili (Dini) ambao ndio siraha kubwa wanayoitegemea wakoloni kuitawala dunia.

Afrika si huru kama tunavyodanganywa, uhuru tuliopewa ni ule wa kutotumika kinguvukazi na badala yake tukapewa utumwa mbaya kuliko hata wa kutumikishwa kinguvu,.

Kuamini kuwa kuna Mungu ambaye yuko mbinguni na ana mitume wake ambao kati yao hakuna hata mmoja aliyeleta injili Afrika, ardhi ambayo ni kubwa na kongwe kuliko yoyote je huyo Mungu halijui hili?.

Kuamini kuwa watu weupe ndio njia ya ukombozi wa afrika sababu ya kuleta hizo dini zao, huu ni upuuzi mtupu, haiwezekani na haitowezekana Umtumie mtu wa mbali apeleke ujembe sehemu ambayo hata hajulikani, hafananii nayo wala hana uzoefu na sehemu hiyo, je kuwatumia wakoloni kuleta dini Afrika Mungu huyu alishindwa vipi kuwatumia hata mitume wapya afrika ili waeneze hiyo injili yake kwa njia ya amani?

Kiuhalisia dunia ina maelfu/mamilioni ya miaka huku watu wakiishi kwa zaidi ya mamilioni ya miaka bila kumjua wala kumsikia huyo Mungu wa hizi dini, je inawezekana vipi stories za uislamu na ukristo zibase katka time line ya miaka 7000 pekee? Je dini hizi hazijui kuwa kuna jamii zilishakuwepo kwa zaidi ya miaka 200,000 kabla yake,

Vile vile tunafundishwa kuwa watu wote wametokana na huyo adam+eva, je kiuhalisia inawezekana wazungu kuzaa mtu mweusi?, ukitumia akili vizuri huwezi kuwa mfuasi wa hizi ngonjera za dini za kishamba.
Mkuu unaona mbali.
Kiufupi ukishaijua historia bara bara hoja za wenye kelele huwa kama upepo kujaribu kuangusha mwamba wa Jiwe.
 
Vile vile tunafundishwa kuwa watu wote wametokana na huyo adam+eva, je kiuhalisia inawezekana wazungu kuzaa mtu mweusi?, ukitumia akili vizuri huwezi kuwa mfuasi wa hizi ngonjera za dini za kishamba.
Watakuambia kuna mtu alimcheka baba yake kwa kuwa uchi so akageuzwa kuwa mweusi.
 
Walisema sisi ni washamba.
Tukaacha ngozi zetu, tukavaa suti.
Tukaacha ngoma, tukavaa saxophone.
Tukaacha majina yetu, tukaitwa Yohana wa Pili.
Ajabu leo Wamasai, Wahamer, na BaTwa waliobaki washamba ndiyo kivutio cha dunia.

Mungu mmoja alitoka Asia,
akapita Ulaya,
akaruka Mediteranea,
akaruka bara zima
akaja kutufundisha kuwa Afrika hatuna Mungu.
Kwa nini asingetua Afrika moja kwa moja bila kusubiri Majahazi ya wanasayansi?

Walikuja na Biblia mkono wa kushoto
na risasi mkono wa kulia.
Tulipofunga macho tukiomba,
walifungua ramani na kugawa ardhi.
Tuliposema Amina,
walikuwa tayari na mkataba wa madini wa miaka isiyo na kikomo.

Tukaambiwa
"Heri kuwa maskini wa moyo",
Wao wakajenga benki.
"Haya Yote ni mavumbi",
Wao wakaanza kuchimba hayo mavumbi kwa excavators.

Wakatuambia tutazame mbinguni, wokovu waja.
Lakini wao waliangalia ardhini, mali zilipo.
Sisi tukarithi mbingu ya nadharia,
wao wakarithi ardhi kwa vitendo.

Majina nayo yakabadilika bhana,
Shimanyi akawa Petro.
Linda akawa Maria.
Kaniki ikaitwa ushenzi,
Suti ya bluu ikaitwa Nguo ya aliyeokoka.

Tulifundishwa
“Mtii mamlaka, maana imewekwa na Mungu.”
Kisha mkoloni akawa ndiyo huyo mtumishi wa Mungu.
Ukigoma, hauipingi serikali, unapinga mipango ya mbinguni hivyo utachomwa kwenye moto mkali.

Watu wetu wakawa washika Biblia,
lakini si washikaji wa hati za ardhi.
Waombaji wa mbinguni,
lakini si warithi wa mashamba.
Waumini wa kweli,
lakini si wamiliki wa chochote.

Makanisa kwasasa yamekuwa kila mita 50,
Kila kona kuna huduma ya kiroho
lakini huduma za kimazingira, kiuchumi, na kisiasa ni uzoefu wa mtu binafsi tu.

Wakasema mbinguni kuna tiketi, Lipeni nauli[sadaka] wakajenga vyumba kwa pesa hizo hizo kisha wakatupangisha hivyo vyumba sisi wenyewe tena.
Wakalima mashamba makubwa halafu wakatulipa pesa hizohizo tulizotoa kama nauli ya mbinguni.

Kwa kifupi,
Tulirithi imani,
tukapoteza ardhi.
Tuliletewa bikira Maria,
tukanyang’anywa mama zetu wa mila na wakunga wa jadi.
Tulipewa mkate wa uzima,
tukanyang’anywa mashamba ya mahindi.

Msije mkasema Kobazi mmesalimika kwenye uzi huu…

Tulilia uhuru,
Tukapewa Uislamu.
Tukapoteza ardhi,
Tukapewa dua za kuondoa uchungu.
Tulipiga magoti,
Wao wakatupiga mihuri ya biashara ya utumwa.

Wakatuchukua kama watumwa,
Wakatupa Qur’an tujifunze kusamehe wanayatufanyia.
Halafu wakatufundisha
“Subira ni fadhila ya waumini.”

Tukafungwa kwenye muda ili tusali sala tano kwa siku na Tukafundishwa kupendana kwa ajili ya Allah.
Tuliuza wake na waume zetu kwa bei ya chumvi, wakatuambia.
Watumwa wenu wapeni haki zao.

Wakasema mahali tunazotoza za ng'ombe 3,4,5...10 si haki wakati zilikuwa zinachochea vijana kutafuta kwa bidii.
Kisha - Wakaoa binti zetu watatu kwa wanne, wakavinjali nao kingono na walijichukulia kiurahisi chini ya kivuli cha Allah anataka mke ndiye apange mali.
Wakawalaghai dada zetu wataje bei za sabuni, wakajichukulia kama kusukuma mlevi mteremkoni.

Wakatuambia tufuate Sunna,
Tukaacha mila zetu.
Tukafundishwa kuvaa kwa mfano wa mji wa Makka,
Tukaambiwaa haramu kuvaa kikoi cha bibi yetu na kuacha wazi kichwa kilichosukwa twende kilioni.

Tulifundishwa kuosha miguu kabla ya swala,
Lakini hatukuwahi kuosha historia yetu ya kunyimwa utu.
Tkafundishwa kujifunika hijjab,
Tukafunika sura zetu.
Lakini hatukufunika makovu ya ukoloni wa kiarabu.

Wakatufundisha kufunga Ramadhan,
Lakini walifungua milango ya Zanzibar ya soko la watumwa ili tusione.
Wakatufundisha kutosengenya,
Lakini wakasema mila zetu ni ushirikina.

Tuliambiwa Qur’an inahifadhi kila kitu,
Tukasahau kumbe ilihifadhi na unyonyaji.
Tukajua aya za adhabu,
Tukasahau historia ya kuadhibiwa.

Tukawa waumini wa kweli,
Lakini si waafrika wa kweli.
Tukavaa joho la ustaarabu,
Lakini ndani tumejazwa hofu ya moto wa Jehanum.

Wakatufundisha maadili ya familia,
Kisha wakazipeleka familia zetu hizohizo kwenye biashara ya utumwa.
Wakatufundisha ndoa halali,
Lakini waliwageuza wasichana wetu wake wa masultani.

Na hata leo,
Tukivaa asili yetu tunaambiwa ni kafir, muasi na mfuasi wa shetani.
Tukicheza ngoma za jadi tunaambiwa ni haramu.

Wakasema dini inaleta uhuru wakajisahaulisha kuwa walitupa uhuru wa kuishi tu akini siyo wa sisi kubaki kuwa sisi.

Uislamu wa Kiarabu na Ukristo wa Ulaya walikuja kwa njia tofauti,
lakini wote walitaka kitu kimoja,
Kutufanya tuwe watu wao, kwa jina la Mungu.

Swali la msingi kwa wote.
Je, Mungu wa kweli anaogopa majina ya asili?
Anaogopa lugha zetu?
Anaona mizimu ya mababu kama uchafu, lakini anaheshimu historia mbaya ya waarabu au wayahudi?

Mungu ambaye anahitaji ubadilike na kuwa mtu mwingine wa nje ambaye si wewe halisi ndio akutambue,
Huyo si Mungu wa kweli.
Huo ni mfumo uliowekwa.

Dini Inayokufundisha utii huku yenyewe haitii mila na tamaduni zako huo ni utii au upendeleo?

​

Tambua kuanzia leo kuwa Mwafrika siyo laana kama tunavyokua tukisikia na kuambiwa bali Uafrika ni nuru na ni nguvu.

Kataa katakata unapoletewa habari za Mungu aliyetumika kama kifuniko cha ukoloni wa kiakili.

Tuna mamilioni ya wafrika wanaoamini kuwa wako huru kwa sababu wamepewa dini huku wakisahau maana kamili ya uhuru.

Uhuru siyo kufanya kilakitu unachokitaka, Uhuru ni kutolazimika kufanya jambo ambalo litakuondolea amani na utulivu.

Je kufanya tu kila unachokitaka bila kujali matokeo kutakupatia amani na utulivu?
Kulazimishwa kufunga na kutoa sadaka ni uhuru?

Hivi kuamini Mungu na dini kwasababu usipofanya hivyo hutakwenda mbinguni bali unatishwa kupelekwa kwenye moto mkali ni uhuru?

kuambiwa ukimuabudu Mungu mali zako zitakua nyingi na maisha yako yatakuwa bora huo ni uhuru?
Au ni kulazimika kufanya kwasababu ya?

Ndiyo maana huwa nasema Afrika haijapata uhuru ila waafrika wachache ndiyo wapo huru.

Swali langu ni moja - Hivi huyu Mungu anayejua kila kitu, anayeweza kila kitu, na aliyepo kila mahali kwa nini alisubiri mpaka meli za waarabu na wazungu zivuke bahari, ndipo tumjue?

Ikiwa yuko kila mahali - Je, hakuwa Afrika kabla ya meli kugundulika wakati huo?

Mimi ni Agnostiki Mstoiki.
Ibn Unuq
Moja ya adhari kubwa kabisa ya UKOLONI iliyotuathiri pakubwa sana hadi leo hii ni DINI

Juzi kati nilikua namsikiliza Nabii koko mmoja anahubiri kwamba msiwape watoto wenu majina ya ajabu ajabu ya ukoo na mababu zenu eti yamebeba laana😳

Dini hizi hazitaki matumizi sahihi ya akili..... zinataka uamini tu
Huu ni UJINGA kama ujinga mwingine tu
 
Mungu kwanini aombwe, anatakiwa atimize majukumu yake kikamilifu,
Mungu ni mzembe na hapaswi kutegemea ,.

Tujitegemee tuache uvuvi wa kufikiri
 
Mkuu Mungu ni roho,na mungu yuko Kila mahali,na Wala mungu hayuko katika physical being bali yuko katika spiritual being,so everywhere Kuna Mungu
Imethibitishwa wapi kwamba Mungu yuko kila mahali?

Mbona mimi simuoni?
Spiritual being maana yake nini?
 
Eti Mungu alimuumba adam na hawa akamuweka bustan ya Eden ili ale bata eti humo humo na li shetan akaliweka then udanganyifu ukatokea ndo yeye akajitokeza akiwa amepanic na kufoka as if alikuwa hajui kinachoendelea mara ghafla mapovu yakamtoka akaanza kuporomosha ma laana kwa Mwanaume,mwanamke hadi kwa nyoka.
Inashangaza sana yaani Mungu aliwaza nini kuliweka sehemu moja shetani na watoto wake pendwa(Adam n Eve).
DINI NI KIFURUSHI CHA UPUUZI KWA WAPUUZI
 
Mungu mjuzi wa yote ajuaye mwanzo hata mwisho hakujua kama Shetani atakuja kuasi kabla hajamuumba.

Mungu mwenye nguvu zote, wa haki alishindwa kumuadhibu shetani moja kwa moja kwa kuasi akaishia kumtupa duniani kwa viumbe dhaifu.

Mungu mwenye upendo akawapa wanadamu adhabu ya milele kwa kushindwa kumshinda shetani aliyempa nguvu na utambuzi kuliko wao.
 
Eti jamani
 
Back
Top Bottom