Mungu anatumiaje pesa wanazompa Waafrika makanisani na misikitini?

Ni Dini gani uliwahi kuona Mungu akipewa hizo Pesa? Lini Mungu alipewa Pesa?

Wanaopokea hizo Pesa, ndio huwa wanazitumia.

Unawalipa kwa kuacha kazi zao nyingine na kuja kukufundisha neno la Mungu, na sio unamlipa Mungu.
Mapadre wanalipwa kwa kuacha kazi zao zingine!
 
Msikitini hawatoi pesa kwa ajili ya Mungu bali ni kwa ajili ya kusaidia jambo fulani. Kupitia wema wako huo ndiyo Mungu atakupa thawabu.

Kuna michango ya kuendesha shughuli za msikiti kama vile huduma ya maji na vitu vingine. Hata umeme wenyewe ukinunua kupitia mita namba ya msikiti na ukawapa tokeni za Luku inatosha. Unaingia msikitini unakuta kuna umeme, maji, matandiko safi na mashine z.a kusafisha. Jua hiyo michango ndiyo inafanikisha vyote.

Mambo ya kumchangia Mungu hayapo hayo, unachangia kwa ajili ya kusaidia jambo fulani kwa ajili ya kufanikisha shughuli za ibada au kumsaidia mwenye haja
 
Ila mashekh wana njaa sana aisee.ndo maana wanagombania hadi ubwabwa kwenye shughuli.
Na mbaya zaidi ni wavivu,wenyewe wanachojua ni kulala tu misikitini muda wa kazi.
 
Waafrica badala wachangishane wafanye biashara na shughuli za kiuchumi wapate maendeleo, wanaishia kuwapa makanisa na misikiti huku wao wakibaki maskini,tubadilike
 
Ila mashekh wana njaa sana aisee.ndo maana wanagombania hadi ubwabwa kwenye shughuli.
Na mbaya zaidi ni wavivu,wenyewe wanachojua ni kulala tu misikitini muda wa kazi.
Hawana tofauti na wakristo au dini nyingine, wote wanafanana kwa shida
 
Ukitoa sadaka unaongezewa kile ulichonacho maradufu amini nakuambia.
Wewe ulitoa nini ambacho baadae ukashihudia kukipata tena mara mbili acha ujinga utoe milioni halafu upate milioni 2 umekaa tu bila kifanyakazi eti
 
Wewe ulitoa nini ambacho baadae ukashihudia kukipata tena mara mbili acha ujinga utoe milioni halafu upate milioni 2 umekaa tu bila kifanyakazi eti
Acha ubishi usio na maana sijasema usifanye kazi toa kile ulichonacho unaweza ukawa na shida Lakini Kuna watu wanashida zaidi yako unadhani matajiri wanavyotoa misaada wanafanya hivyo kwa bahati mbaya?
 
Watumishi wake ndio wanazozitumia kwa niaba yake. Unataka kumuona Mungu mwenyewe akizitumia? we ni mtu wa mwilini hutamuona Mungu kwa mtazamo ulio nao
Hivi ndivyo mlivyojazwa ujinga na wajanja wachache ili waweze kujihalalishia urasimu wao
 
Hili swali kijana wangu wa miaka 10,analijibu vzr tu, kama wewe huna jibu,
Ni, dalili mbaya kwa mfumo wetu wa, elimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…