Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Komenti nyingi naona wamemuandama sana mleta mada..pasipo kujibu hoja kwa hoja..
 
Sema wakristo wengi hatusomi biblia kikamilifu, matokeo ni kupwaya pale zinapoibuka hoja kinzani kama hizi, unakuta swali moja linaleta majibu 40, na hayajitoshelezi. Tusomeni Biblia na kuielewa vyema wakuu.

Kabisa hii topic imejibiwa na majibu tofauti tofauti sana
 
Haya sawa
 
Komenti nyingi naona wamemuandama sana mleta mada..pasipo kujibu hoja kwa hoja..
Nawewe unafuatia humo humo, toa majibu yako huenda yakafanya warudi kwenye hoja ya mtoa mada.
 

Huyo mungu wa sumerians alikuwa mungu wa mchongo na ndio maana alishindwa kuwithstand the test of time na kupelekea hadi wewe mwenyewe kuja na kihoja cha kila zama na kitabu chake.
Kama angekuwa Mungu wa kweli tungemjua hata leo.
Kati ya Nuhu wa kwenye biblia na sumerians nani alitangulia?
 
Mungu wangu !!! So Adam na Hawa nao walizaliwa na Yesu [emoji51][emoji3][emoji23]

Kaka inabidi umjue Yesu vizuri kwa kumsoma katika kitabu cha biblia. Wewe unamjua Yesu baada ya kuzaliwa na mariam lakini Yesu alikuwepo kabla ya mariam. Yeye ndiye MWANZO. Ameshiriki uumbaji wa Adam na hawa.
Mwanzo : 1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Kwenye hilo andiko Mungu anaposema na TUMFANYE mtu, alikuwa na nani?
 
Alikuwepo wp ? Why akaja kuzaliwa na Maria si angeshushwa tu? Unaposema ni mfano wa Mungu kwahiyo yeye sio Mungu ni mfano wake?

Hahahahahah Tatizo unakuja na majibu yako kichwani kwamba si angeshushwa tuu. Tujadili maandiko ndugu sio vioja.
Yesu ndio ni mfano wa Mungu asiyeonekana.
Kama nilivyosema toka awali Mungu wa biblia aliye baba ana mwanawe anaitwa Yesu. Hakuna aliyewahi kumuona baba ila mwanawe Yesu ndio kamfunua kwa watu. Ukimuona Yesu umemuona Baba.
 
kama hujui hata aliyetangulia inaonekana wewe Bado Sana Kwenye masuala ya Accient civilizations,
Sasa unachobishana na Mimi ni Nini hapa wakati hata hujui
Mungu wako Elohim/YWH/Jehovah
Alikuja miaka zaidi ya elfu Tano mbele nyuma Mungu mkongwe na wa Mwanzo kuabudiwa na Sumerians, Assyrian, Babylon, Egyptian aitwaye ANU?

Mungu wenu alijitambulisha Kwa mara ya kwanza Kwa jamaa anayeitwa Abraham!
 
Umejuaje kua kulikua na binadam kabla ya hao?
 

Mada imeisha
 
We tatizo lako nikuwekea maandiko unayakataa, unakuwa na vioja si hoja za maandiko
Ndugu Olando sisi Tupo katika Mjadala wa Fikra Huru. Nayakataa Maana Unasimamia Maandiko ya Watu wanaokupotosha. Na Maandiko ambayo yanamakosa Ndani yake. Unachotakiwa ni Kusimamia Akili yako Inasemaje Kuhusu Jambo Fulani ninalokuuliza tu

Mfano Mimi nakuuliza Mungu alikuogopa Nini wewe mpaka Akakutolea mwanae Awe Sadaka ila Wewe unaniletea Andiko ambalo halijibu Swali langu. Maana Kama Ni Dhambi ndio sababu hizo Dhambi hazijaisha. Na Dhambi hata Sodoma na Gomora walitenda Ila Aliwaunguza na Moto hakuwatumia Mtoto wake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…