Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Ni ngumu kwao kukubali Hilo ingawa Moyoni wanajua Ukweli Ulipo ila Hawataki kukubaliana Na Ukweli kwamba Wamepotoshwa sana na Wameharibikiwa

Hata Jina La Yesu Halikutabiriwa katika Maandiko ila Aliyetabiriwa alikuwa ni Emanueli
 
Mkuu me nasoma biblia ila sipotezi mda wangu kusoma story sijui za waisrael, sijui wakina ESTA , au story za makabila ya waisrael ,cjui washeba, mara sijui wanan , Mimi huwa napenda mistari inayoniongezea busara na maarifa kama hekima ,enjili nk
Umechagua Jambo Jema. Tafuta Hekima Itakayokufaa katika Vitabu ila Kuwa Muumini wa Akili Timamu tu Ndugu hakuna Malaika waongo... Majini waongo watakaokusumbua
 
Huo ni ujuha wako tu. Qur'an inajitosheleza. Hakuna neno la Binaadam lishindane na la Allah. Kuamini kuwa hadith (maneno ya binaadam) ndio yanatafsiri maneno ya Mwenyeezi Mungu ni kufanya shirki.

Qur'an ni "criterion", yenyewe inasema imekuja kuweka sawa palipotiwa mikono ya watu, sasa tuendeleze ujinga huohuo wa kutia mikono yetu na kuiona kuwa Qur'an haijitoshelezi? Kwa mtazamo wangu huo ni ujuha tu.

Qur'an haina shaka.
 
Soma uelewe kwanza.. umeambiwa kama unaona Miungu ya babu zenu inafaa nendeni mkaiabudu. HAUJALAZIMISHWA KUIAMINI BIBLIA.
Hujui Kwamba Huko Ndiko kuna Miungu Tofauti tofauti kuliko unaposema Mababu wa Miungu.Mababu walikuwa na Mungu si Miungu

Hamjui kwamba Huko Mnaabudu Miungu mitatu (utatu)
 
Jibu Aya maswali bila Hadith wala tafsir

Mfano Aya hii
Koran 66:4. Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake muhammad, basi hakika Allah ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

maswali
1. hao wawili ni kina nani? ,
2. Wamefanya dhambi gani mpaka waambiwe watubu? ,
3. Wakisaidiana dhidi ya Muhammad kwani Muhammad kafanya nini? ,
4. Kwa nini Allah asaidiane na Malaika wote , jibril na waumini wote kupambana na hao wawili?
5. Awa wawili wana nguvu gani mpaka Allah asaidiwe
 
Haileti maana yoyote pale tunapoambiwa Mungu anajua hadi wakati ujao. Alafu huyo huyo anaweka mpango siku moja aumbe binadamu huku akijua watamuasi na itambidi amtoe mwanae wa pekee kama sadaka.
 
Haileti maana yoyote pale tunapoambiwa Mungu anajua hadi wakati ujao. Alafu huyo huyo anaweka mpango siku moja aumbe binadamu huku akijua watamuasi na itambidi amtoe mwanae wa pekee kama sadaka.
Ndivyo watu wanaishi kwenye Hizo Imani
 
Hujui Kwamba Huko Ndiko kuna Miungu Tofauti tofauti kuliko unaposema Mababu wa Miungu.Mababu walikuwa na Mungu si Miungu

Hamjui kwamba Huko Mnaabudu Miungu mitatu (utatu)
Nilisha kuonya ukitaka kujua Imani ya watu kaisome kwanza uelewe, Mungu wa wakristo unatakiwa uelewe yupoje ili kuepuka maswali ya kitoto

Mungu ni Roho na ana nafsi tatu toka uwepo wake , ana Nafsi Baba , Mwana na Roho mtakatifu na nafsi zake zote ni divine

Mungu alitengeneza mwili humani flesh ambayo ilipitia kwa maria ambayo ndio aliitoa sadaka na kufuta sadaka zote za damu za wanyama

Aliitoa nafsi yake moja ya mwana ndio ikavaa mwili human flesh huo mwili iliopitia kwa maria

Mungu hazai wala hajazaliwa , Mungu hafi
Mwili alikuwa nao nafsi mwana ndio ulikufa na aliufufua mwenyewe huo mwili
Alikuja kwetu kutufunza jinsi ya kuishi utakati na jinsi tunatakiwa kumuabudu Mungu

Kuna mda Yesu alikuwa anaongea kama human flesh na kutenda kama human
Na Kuna mda alikuwa anaongea nafsi ya Mungu ambayo ilikuwa ndani yake kama miujiza , kufufua wafu , kusamehe dhambi n.k

Unaposoma biblia unatakiwa ujue wapi Yesu anaongea kama human flesh na wapi anaongea kama Mungu

Ndio maana Kuna watu niliwakanya hapa wasiingize nature ya Mungu wao kwa Mungu wa wakristo na wewe nakukanya usilete nature ya Mungu wako kwa Mungu wa wakristo

You a demonic possessed
 
Alafu hapo hapo anaweka na moto wa milele. Yani alijua kabisa atamuumba mtu na mtu atazingua na itabidi kumchoma moto ila akamuumba ili aone shoo ya moto wa milele imekaaje.[emoji17]
Wakija Watakuambia Unakufuru. Yaani Unatengeza Kitu kama Gari aj Baskeli halafu Kikikuangusha Unakichoma Moto na Kusema Umekikomesha na Kitasaga Meno
 
Watu hawawezi kuelewa bila mfano....kuzihirishwa kwa yesu ulikkua mfano tosha kwa maisha ya mwandamu.
 
Hizo porojo zako binafsi, weka ushahidi wa maandiko, kama huna ni heri ukae kimya tu.

Waebrania : 1 : 4 - amefanyika bora kupita malaika, kwa kadiri jina alilolirithi lilivyo tukufu kuliko lao.
Waebrania : 1 : 8 - Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

Maandiko hayo hapo
Baba anamuita mwana Mungu.
 
Aisee mbona unachukua aya moja tu katafute aya toka ya kwanza ndo utajua maana yake
 
Nilisha kuonya ukitaka kujua Imani ya watu kaisome kwanza uelewe, Mungu wa wakristo unatakiwa uelewe yupoje ili kuepuka maswali ya kitoto
Una Ucha Mungu Mkubwa Sana ila Unatetea Imani Za Wengine ambazo huzijui ndugu yangu. Unapomuita Mungu Baba na Kumwita Yesu Mungu Mwana Hao Ni Miungu Miwili tayari

Na Ki Utu... Baba Ni Jinsia ya Kiume ya Viumbe. Mungu Hawezi akawa na Sifa za Kiumbe yeye Hafanani na Chochote kile wala Kiumbe chochote kile




1.Mungu hakuwa na Haja Ya Kufanya Hayo Yote wakati aliweza Kumuumba Adam unayemwamini kama Mwanadamu wa Kwanza Kutoka Kwenye Udongo. Mimba ya Mariam ina utata maana Malaika Aliyekuja Kumjuza Alimwambia Mtoto atamwita Yesu wakati Isaya Alitabiri ataitwa Emanueli angetakiwa Kumuita Kama ilivyotabiriwa na Isaya kwanza

2. Wayahudi waliendelea na Ibada za Wanyama na Kuendelea na Torati. Yesu Hakuziondoa Hizo Sadaka



Acha Kupanic ndugu yangu
Mie Maswali yangu Ndugu ni Haya

1. Wewe ulifanya Nini Mpaka Akatoa Nafsi yake Ije Duniani na Aitoe Sadaka

2. Alikuja Kukufundishajw Kuabudu wakati Musa Alikuwa na Torati tayari iliyokuwa na Miongozo Mingi

3. Na Inakuwaje Yesu alipopatwa na Magumu alienda Kuongea na Musa na Elia wakati nafsi mbili aliziacha Mbinguni. Kwanini Asingeongea na Mungu mwenyewe
 

Maandiko yanasema Baba anaitwa Mungu na mwana pia anaitwa Mungu

Waebrania : 1 : 8 - Lakini kwa habari za Mwana asema, Kiti chako cha enzi,Mungu,ni cha milele na milele; Na fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
 
Hivi kwanini huwa mnawatazama watu wa dini tu tena wakristo na waislamu tu, wenye imani tofauti na hizo mbona hamuwatizami? na wale wasioamini Mungu au dini mbona hamuwaubilii?
 
Hivi kwanini huwa mnawatazama watu wa dini tu tena wakristo na waislamu tu, wenye imani tofauti na hizo mbona hamuwatizami? na wale wasioamini Mungu au dini mbona hamuwaubilii?
Wapagani- hawa ni Watu wasioegemea Upande wowote ule wa Ki dini. Wanaweza Wakawa wanajua Ukweli ila Wakaa pembeni tu Hawajihusishi na Chochote

Wakristu na Waislamu wao Hujinadi wanamjua Mungu na Ndio wenye Mungu wa Kweli kuliko Wengine na uwahubiria Watu wengine wamepotea na Watachomwa Moto kama Hawatomwamini Mungu wao

Wakati Ukweli ni Kwamba Ni Dini zilizoletwa na Viumbe wapotofu na Hazina Ukweli ndani yake. Ukweli upo kwenye Jadi na Elimu ya Mwanzo ya Wazee wetu waliomjua Mungu kabla ya Hizo Dini Kuja
 
Utaanzishaje Dini Yako au Imani yako Ndugu wakati hujui Mwanzo kulikuwaje. Hata Watu wakikuuliza Umetokea Wapi utawajibuje Wakati Dini yako Umeianzisha 2022.
Kwani hao wazee wetu afrika tunajua hizo imani zao walizipata wapi na kwa vp? hapa kinachoonekana lengo ni kuwa na kitu chetu wenyewe waafrika na kuacha kutumia vitu vya kuletewa ndio maana uislamu na ukristo tunaita ni imani za kuletewa sio asili yetu. Kwahiyo na sisi tuanzishe dini yetu yenye kubeba mambo ya kiafrika na kwa sasa tuna nafasi nzuri tunaweza kuandika hivyo hata vizazi vyetu vijavyo watakuta maandiko ya dini ya mababu zao.
 
Kwani hao wazee wetu afrika tunajua hizo imani zao walizipata wapi na kwa vp?
Kwani Wewe ndugu yangu Tz Mbongo. Unajua Elimu za Mababu wa Israeli kina Musa.. Elia.. Isaya walizipataje.!? Au umesoma Tu kwamba Walipata Kwa Mungu na Wewe ukaamini Bila Kuhoji


Elimu Yetu ipo Inaitwa SENDE ESUPRY DEWO OCHI. Ni Kibantu kikimaanisha NGUVU ILIYODUMU KATIKA JADI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…