Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Yeah!
Tuanzishe dini yetu ya kitanzania🤝💪🏿
 
Sasa hao nao wanafaa kuwahubiria ili wafuate ili waujue ukweli na kuufuata na hata kama wanaujua ukweli pia muwahubirie waufuate kwa vitendo na sio kujiweka pembeni. Tena hao ndio ingekuwa ni wepesi kuwahubiria maana hawajafungwa na imani za dini wapo huru ila matokeo yake mmewaacha hao na kupambana na watu wa dini.
 
Unanielewa lakini mkuu?

Nachosema ni kwamba tuanzishe sasa dini yetu waafrika na itambulike kuwa hii ni dini ya waafrika kama zilivyo dini za wazungu na waaarabu, maana hizo si za kuletewa basi tuanzishe za kwetu kwa hiki kipindi chetu na tuachane na hizo za urithi ambazo zilikuwa ni imani za mababu zetu katika kipindi chao huko na mazingira yao.

Tuanzishe cha kwetu chenye kuendana na mazingira yetu ya sasa.
 
Sasa hayo si mambo ya kawaida sana, au huelewi unachokisoma? wapi alipoitwa "mwana wa Mungu"? Mbona biblia ina wana wa Mungu wengi kwa matani (wengi sana) huwaelewi?

Binaadam yeyote ameumbwa kwa ubora wa kuweza kuamua jema na baya, ni ubora ambao hakupewa malaika.

Hilo la mwisho mbona ni haki yetu wote kumsifu Mungu?

Sioni ushahidi hapo, unajidanganya tu mpaka sasa. Kinaandikwa kingine unataka kukitia maana nyingine.
 
Nimesema hakuna miungu ila Kuna Mungu na ana nafsi tatu , alafu Mungu ata akisema nipo kumi shida ni nini?
Baba sio kwa jinsi unavyoelewa wewe na wala Haina maana yoyote ya jinsia , ndio maana unakuta nchi inaitwa mama, na wala haimanishi nchi ina jinsia

Musa alifundisha wakati wake na Sheria za kipindi hicho ambacho Mungu aliona zinafaa kwao
Kwa ukristo tunaamini Mungu anapatiliza dhambi toka kizazi mpaka kizazi,
Dhambi tunairithi toka kwa adamu

Unapotosha makusudi soma ukristo na uelewa wanavyo elewa ,
Shida Iko wapi Yesu akiongea na Elia na musa?

Isaya alisema Emmanuel , Emmanuel maana yake ni Mungu pamoja nasi , Yesu mwili wake ulikuwa na nafsi moja ya mwana ndani yake ambayo nafsi hiyo ni devine ni Mungu ndani ya mwili wa Yesu ndio alicho maanisha Isaya

Ndio maana nakwambia you are demonic possessed ,

Na acha kuingiza nature ya Mungu wako kwa Mungu wa wengine
 
Sasa Ndugu unaanzishaje wakati Binadamu wa Kwanza keshawapa Watu(Wabantu) utaratibu wa Kumwabudu Mungu katika Jadi.
 
Aisee mbona unachukua aya moja tu katafute aya toka ya kwanza ndo utajua maana yake
Si uweke ili Kuweka mambo wazi na uoneshe nilivyo danganya mbona simple Sana

Ila kwa sasa msaidie FaizaFoxy
Jibu Aya maswali bila Hadith wala tafsir

Mfano Aya hii
Koran 66:4. Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake muhammad, basi hakika Allah ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

maswali
1. hao wawili ni kina nani? ,
2. Wamefanya dhambi gani mpaka waambiwe watubu? ,
3. Wakisaidiana dhidi ya Muhammad kwani Muhammad kafanya nini? ,
4. Kwa nini Allah asaidiane na Malaika wote , jibril na waumini wote kupambana na hao wawili?
5. Awa wawili wana nguvu gani mpaka Allah asaidiwe
 
Mungu haubiriwi ndugu yangu. Mahubiri na Kusambaza Imani Zimeletwa na Hao Watu kutoka Huko Ukoloni. Afrika Mungu alikuwa haubiriwi popote pale

Bali kulikuwa na Taarifa za Jadi. Kufundishana Taratibu za Kuishi si Kumhubiri Mungu
 
1) Kasome hiyo sura kuanzia mwanzo mpaka ukifika hapo aya ya 4 utakuwa umeshapata majibu ya maswali yako yote.

Soma kijana.
 
Hizo lugha walizoongea ndizo unazotumia leo kwenye biblia yako?

Au kwa ufupi, Biblia yako ipo kwa lugha aliyoitumia Yesu?
Biblia ipo kwa lugha yake original , ndio maana ata Allah akatumia neno injil ambalo sio la kiarabu kuelezea kitabu Cha issa
 
1) Kasome hiyo sura kuanzia mwanzo mpaka ukifika hapo aya ya 4 utakuwa umeshapata majibu ya maswali yako yote.

Soma kijana.
Mutah girl Jibu hapa Aya maswali acha kuleta janja janja ya kitoto

Mfano Aya hii
Koran 66:4. Kama nyinyi wawili hamkutubia kwa Mwenyezi Mungu, basi nyoyo zenu zimekwisha elekea huko. Na mkisaidiana dhidi yake muhammad, basi hakika Allah ndiye kipenzi chake, na Jibrili, na Waumini wema, na zaidi ya hayo Malaika pia watasaidia.

maswali
1. hao wawili ni kina nani? ,
2. Wamefanya dhambi gani mpaka waambiwe watubu? ,
3. Wakisaidiana dhidi ya Muhammad kwani Muhammad kafanya nini? ,
4. Kwa nini Allah asaidiane na Malaika wote , jibril na waumini wote kupambana na hao wawili?
5. Awa wawili wana nguvu gani mpaka Allah asaidiwe
 
Nimesema hakuna miungu ila Kuna Mungu na ana nafsi tatu , alafu Mungu ata akisema nipo kumi shida ni nini?

Ndugu yangu sasa Si Atakuwa Amejipinga Mwenyewe na Amri yake ya USIABUDU MIUNGU mingine. Wakati Yeye Kumbe wapo Kumi.

Na Wewe ukisema Ni Mmoja kumbe Wapo Watatu kwenye Nafsi Tatu huoni unajichanganya Mwenyewe. Nafsi Moja Ikiwa Duniani Nyingine zipo Mbinguni hapo Utasema Kuna Mungu Mmoja Tena?

Baba sio kwa jinsi unavyoelewa wewe na wala Haina maana yoyote ya jinsia , ndio maana unakuta nchi inaitwa mama, na wala haimanishi nchi ina jinsia

Twende Kwenye Maana Halisi ya Baba Na Mama. Ukiambiwa Maana Halisi ya baba na Mama huwezi kusema Si Jinsia. Maana Halisi ni Jinsia ya Kiume ya Viumbe na Mama Maana Yake Halisi ni Jinsia ya Kike ya Viumbe. Na Mungu zamani kabla ya Yesu Kuja Hakujulikana Kama Baba aliitwa Mungu tu bila Kumwita Baba

Musa alifundisha wakati wake na Sheria za kipindi hicho ambacho Mungu aliona zinafaa kwao

Kwahiyo Amri Kumi Wewe huzifuati!?

Kwa ukristo tunaamini Mungu anapatiliza dhambi toka kizazi mpaka kizazi,
Dhambi tunairithi toka kwa adamu

Ndugu kama Dhambi tunarithi wewe umebeba Dhambi ngapi hapo Toka Adam mpka wewd upo 2022. Huo mzigo unauweza Kuubeba

Unapotosha makusudi soma ukristo na uelewa wanavyo elewa ,
Shida Iko wapi Yesu akiongea na Elia na musa?

Shida Ipo Kama Yeye ni Mungu anaongeaje na Mizimu ya Musa na Elia. Maana tunajua Musa na Elia hawakuwa Malaika. Walikuwa binadamu Na Walikufa.

Maana Umesema Nafsi mbili zilibaki Inakuwaje tena Anaenda Kuwasiliana na Viumbe waliofariki Nyuma

Na Nyie Mkiwa Mnasali mnakemea Mizimu halafu kumbe Hata Yesu aliwafuata Mzimu wa Babu zake wa Zamani

Isaya alisema Emmanuel , Emmanuel maana yake ni Mungu pamoja nasi , Yesu mwili wake ulikuwa na nafsi moja ya mwana ndani yake ambayo nafsi hiyo ni devine ni Mungu ndani ya mwili wa Yesu ndio alicho maanisha Isaya

Tatizo siyo Maana Ya Jina. Swali langu ni Hili Isaya alisema Mtoto ataitwa Emanueli ila Kwanini Hakuitwa Hilo Jina hilo akaja Kuitwa Jina Yesu? Hilo ndilo swali langu

Ndio maana nakwambia you are demonic possessed ,

Na acha kuingiza nature ya Mungu wako kwa Mungu wa wengine

Kukuuliza Maswali Haimaanishi anayekuuliza Ana Demon ndani yake. Wewe kama Una Mungu Ndani Basi Jibu. Mbona Hata Mungu alikuwa anapiga Stori na Mungu Kipindi cha Ayubu kwenye kitabu unachoamini
 
Mada imeisha
 
Ni ngumu kwao kukubali Hilo ingawa Moyoni wanajua Ukweli Ulipo ila Hawataki kukubaliana Na Ukweli kwamba Wamepotoshwa sana na Wameharibikiwa

Hata Jina La Yesu Halikutabiriwa katika Maandiko ila Aliyetabiriwa alikuwa ni Emanueli

Sasa kwanini wamwite Yesu badala ya Emanueli?
 
Kwanza hii sadaka aliitoa kumpa nani? Na pili je upande mmoja anatoa mwenyewe na upande wa pili anapokea mwenyewe???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…