Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

FabNXTzqEtcgazfbjjfo

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2019
Posts
1,486
Reaction score
1,874
Kuna Mambo Yapo Ulimwenguni ukiyatafakari kwa Kina hayaingii Akilini ndugu waafrika wenzangu

Kuna Historia katika Vitabu kwamba Mungu alimtoa Mwanae Ili aje Kuikomboa Dunia katika Dhambi (ambazo zipo mpaka Leo)

Ukiangalia kwa Undani Historia hii ya kuzaliwa kwake inatia Shaka sana kabla ya Kujua Majibu ya kuzaliwa kwake inakuja Historia kwamba hana Baba. Kabla hujapata Majibu ya Baba ni nani Inakuja Kwamba ni Uwezo wa Mungu ndio akazaliwa. Yanakuwa Maswali juu ya Maswali

Kumbuka Yusufu na Mariam si kwamba Walikuwa ni Wachumba la hasha bali walikuwa tayari wapo Ndani (wameoana) wanaishi pamoja. Hakuna wachumba Wanaoishi pamoja kwa Utaratibu wa Kuishi. Ukichumbia wewe utakaa kwako na Huyo mchumba atakaa kwao. Kama Waliishi pamoja maana Yake waliweza Kushiriki Tendo la Ndoa yao na Ukifuatilia kwa Makini Yusuf alikuwa Pamoja na Mariam kila Sehemu hakuna Sehemu inayosema Alikuja Kumuoa mariam Ikiwa na Maana Kwamba Tayari alikuwa keshaoa maana yake ule uchumba ulio andikwa Tayari ukayeyuka

Binadamu huzaliwa Kwa Mwanaume na Mwanamke hili halina ubishi. Ila Kuna Kuja Utata wa Hapa Kwamba Yesu alizaliwa bila Mfumo maalumu wa Uzazi wa Baba na Mama ila Roho Mtakatifu kama Wanavyodai (kumbuka Hata Huko india Wapo Watu wenye Hadithi hizi hizi za Kuzaliwa bila Baba)

Sasa Hapa Unajiuliza Maswali. Mungu huyo aliyeweza Kumuumba Mwanadamu wa Kwanza Bila Kutumia mifumo ya Uzazi Inakuwaje leo aje Aanze Kumuumba Binadamu mwingine anayedaiwa ni Mwanae kwa Mifumo ya Uzazi na Akaenda kwa Mariam ambaye alikuwa teyari ana Mume(kumbuka Hapa Mungu hazai na Wala Hakuzailiwa)

Sasa Anamzaa mwanae kupitia Mariam mara Yusufu atake kumkimbia Mariam maana Kuna Siri May be Yusufu aliiona akaona Hapa Nimepigwa na Baada ya Yesu kuzaliwa Yusuf Anapotea Ghafla kwenye Maandiko na Historia yake inaishia Hapo hapo

Mungu anamtoa Mwanae. Anakuja Mnamkataa, mnampiga, mnamtesa anawahubiria mnagoma Kukubali maneno yake mnamfukuza kwenye masinagogo yake, Anaenda Kusali mlimani peke yake, anakusanya wanafunzi wake. Hao wanafunzi nao mnawakataa mnawafukuza. Hivi Mungu hapo anawaogopa Nyie kisa Nini mpak Awafanyie Haya Yote Nyie Viumbe wake

Yaani Mungu mpaka Anatoa Mtoto wake Wa Pekee ili awabembeleze nyie mmrudie Yeye na Mnakataa. Sasa Hapo Mungu Anakuwa na Ule Uwezo na Kutoshindwa Kitu kweli. Kama Kawatumia Mwanae na Mmemgomea kawatumia Manabii na Mitume mmemgomea Tena na hamtaki kumrudia. Hivi Mungu anawalemba Hivyo Ili Iweje

Si kila Mtu anayezaliwa bila Baba Yake basi Baba Yake ndio Mungu. Wachawi wanazini na Binadamu kila Siku na Wachawi hao hao ndio Binadamu wenzenu. Wanawake wanabeba Mimba zingine wasizozijua zimetoka wapi

Basi Mjue Kwamba Hapo Mwenye Enzi Mungu hayupo na Mnaozeshwa Akili zenu ndugu zangu. Kaeni Chini Mtafakari kwa Akili zenu Timamu. Mungu hawezi kufanya hayo Kwa Viumbe wake. Yeye hayupo Hivyo

[emoji3507]Mungu si Mmoja
[emoji3507]Mungu si Wengi
[emoji3507]Mungu si Baba
[emoji3507]Mungu si Mama
[emoji3507]Mungu si Kiumbe
[emoji3507]Mungu hachukii Viumbe
[emoji3507]Mungu hapendi Viumbe wake ila Ana Enzi na Viumbe wake (usijione wewe Kiumbe Mtu unapendwa na Mungu Kuliko Viumbe wake wengine aliowaumba)
[emoji3507]Mungu hakuzaa wala Kuzaliwa

Yachunguzeni maandiko Yenu mtajua kwamba si Maandiko ya kiucha Mungu ila Maandiko ya Viumbe wenye Tamaa

ASANTENI
 
Hili andiko lako Mungu alishatoa jibu kwamba "msichunguze maandiko maana mnatafuta ubatili"!
Mungu alijua upo na utachunguza lutafuta makosa tuu Wala hutafuti usahihi.
Yesu ni Mungu.
Ndugu yangu huoni Unazidi kujipotosha. Mungu haongei na Wala haandiki chochote kile. Ukiona Umeambiwa Usichunguze maana Yake Yana Uongo humo Ndani yake.
 
Kwa hiyo unataka kutuambia Yesu ni mtoto wa Yusufu na hakufanyika kwa uwezo wa Roho mtakatifu?
Kuna Utata mkubwa Sana Katika kuzaliwa kwa Yesu kutokana Na Maandiko ya Biblia. Ila Kwa Akili Timamu Binadamu yeyote lazima Azaliwe kwa Mifumo maalumu ya Mbegu ya Kiume kuungana Na Mbegu ya Kike Tofauti na Hapo Binadamu hawezi Kutokea
 
Kuna Utata mkubwa Sana Katika kuzaliwa kwa Yesu kutokana Na Maandiko ya Biblia. Ila Kwa Akili Timamu Binadamu yeyote lazima Azaliwe kwa Mifumo maalumu ya Mbegu ya Kiume kuungana Na Mbegu ya Kike Tofauti na Hapo Binadamu hawezi Kutokea
Kwanin ukaendelea na maisha yako ukaachana na ukristo nauhakika ujashikiwa fimbo uiamin biblia, waache wanaoamini waendelee kuamini
 
Alimtoa sadaka mwanaye mpendwa akamuacha apigwe kichapo cha aibu mpaka kifo

Fikiria huyo ni mwanaye mpendwa na hakuna mwingine kwa Mungu mwenye kuzidi viwango vya upendo kama huyo

Na bado belivers wanaendelea kutaka tuamini kuwa anatupenda

He killed his own son so that he can forgive us... but if we don’t believe he killed his own son he is gonna kill us too

What a joke but I ain't laughin?
 
Soma Bible Sana uokoke. Mungu ni mwema.
Kusoma Biblia hakuwezi kukuokoa anayekuokoa ni Binadamu mwenzako tu. Ukizama majiini utaokolewa, ukipata ajali utaokolewa, Biblia imejaa utunzi wa Binadamu

Ni bora ukakombolewa maana anayekukomboa ni Yule anayekuambia Ukweli. Kumbuka Adam na Hawa si Binadamu wa kwanza Kama Biblia inavyosema mana Adam na Hawa waliwakuta Binadamu Duniani kitu ambacho Biblia haijakisema
 
Sasa ikiwa mnaona ni vibaya kumtumikia Yehova chagueni leo yule mtakaemtumia, iwe ni miungu ambayo mababu zenu waliabudu nga°ambo ya mto. Yoshua 24:15

HULAZIMISHWI KUMWAMINI YEHOVA, CHAGUA MUNGU UTAKAE ONA ANA KUFAA.
 
Kwanin ukaendelea na maisha yako ukaachana na ukristo nauhakika ujashikiwa fimbo uiamin biblia, waache wanaoamini waendelee kuamini
Ndugu yangu ni Sawa na Kusema Yesu angebaki kuwa huko huko alipo awaache Wayahudi waabudu watakavyo(kama Madai ya Biblia yasemavyo).

Huwezi kuona Watu wanaharibikiwa leo hii kuna Madhehebu 1000 yanapotoshwa Duniani halafu ww ukae kimya. Waambie Ukweli ndugu yangu wao watachambua Wenyewe kwa Akili zao
 
Back
Top Bottom