Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Mungu anawaogopa nini Wanadamu mpaka awatolee Sadaka ya Mwanae?

Ukifikia kwa kina kweli kuna contradiction za kutosha kwenye maandiko yetu haya, lakini haitoshei kuhitimisha moja kwa moja kwamba ni udanganyifu.

Pia kuna mbegu imepandwa ndani yetu kwa muda mrefu sana ambayo imesha mea na kustawi na kuzaa sana maishani mwetu ya neno la Mungu kupitia vitabu hivi tunavyoviongelea hapa.

Kwa hivyo haitakuwia rahisi sana kueleweka hata kama unaongea ukweli kiasi gani.

Na mimi ni mmoja wapo ambae siwezi kukuelewa kwa urahisi japo unaongea ukweli.
Jamii yetu inaitaji msaada mkubwa sana wa kubadilisha mbegu iliyopandwa na udanganyifu wa hizi dini. Ila naamini huu udanganyifu una mwisho wake. Tatizo pia jamaa wana mizizi milefu sana kisiasa na kiuchumi. Ukiwapinga hadharani hawachelewi kukuondoa
 
Ndugu yangu huoni Unazidi kujipotosha. Mungu haongei na Wala haandiki chochote kile. Ukiona Umeambiwa Usichunguze maana Yake Yana Uongo humo Ndani yake.
Mungu anaongea na ndio maana hata wewe umeweza kumjua kuwa yupo na yote yanayomuhusu bila hivyo we unafikiri huyo Mungu tungemuonea wapi ili tujue kuwa yupo na yote yanayomuhusu?
 
Mungu anaongea na ndio maana hata wewe umeweza kumjua kuwa yupo na yote yanayomuhusu bila hivyo we unafikiri huyo Mungu tungemuonea wapi ili tujue kuwa yupo na yote yanayomuhusu?

Wewe ndio uniambie Umeshamuona Wapi na Kusikia Akiongea maana Mie Sijawahi
 
Soma Historia za Wazee wako na Babu zako na Jadi utajua Ukweli. Adam na Hawa si Binadamu wa Kwanza

Afrika Kulikuwa na Watu na Ulaya Pia Kulikuwa na Wa

Tuanzishe mchakato wa kutengeneza kitabu chetu cha imani ya Mwafrika. Abacho kitaelezea mazuri ya fufuata na mabaya ya kuacha. Kitaelezea vizuri Historia ya Africa na kuwaelezea kwa ufasaha viongozi wetu wa zama hizo.

Kiukweli maisha ya watu Weusi hadi sasa yana mateso makubwa sana kuliko maisha ya waizlaeli yanayoongelewa kwenye biblia. Tukiweza kutengeneza kitabu ambacho kiwe mwongozo wa maisha ya mtu Mweusi, hizi propaganda za dini zitakufa na jamii yetu ita stawi. Maana mchawi wa Mtu Mweusi ni Mzungu ambaye kampandikiza fikra mbovu kichwani. Bila kufuta hizi fikra hatuwezi kutoboa.

Na tujenge nyumba za ibada ya Weusi ambazo tukisali tuwe tunaongelea maisha yetu pekee, yaani tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Bila kubadili imani zetu hatutaweza kujikomboa.
 
Hayo mambo yote yanafanyika na Yapo tayari Toka zamani Na Kitabu Kipo kinachoelezea Mwanzo wa Utu na Binadamu wa Kwanza na Hata Historia za Watu wa Kale wa Afrika. Imani yao kwa Mungu ilikuwa ni ipi na Mambo kadha wa kadha

Ila Kabla Hujajua Yote hayo unatakiwa Kuingia Kwenye Darasa Maalumu usikilize kwanza na Upate masomo ndio ununue kitabu Ujisomee
 
Kuna Utata mkubwa Sana Katika kuzaliwa kwa Yesu kutokana Na Maandiko ya Biblia. Ila Kwa Akili Timamu Binadamu yeyote lazima Azaliwe kwa Mifumo maalumu ya Mbegu ya Kiume kuungana Na Mbegu ya Kike Tofauti na Hapo Binadamu hawezi Kutokea
Mambo ya yai na kuku nani nani wa kwanza.
 
Wewe ndio uniambie Umeshamuona Wapi na Kusikia Akiongea maana Mie Sijawahi
Sasa kama hujawahi kumuona wala kumsikia ina maana hayo unayoyajua kuhusu huyo Mungu ni vitu ulivyojitungia tu, unaanzaje kueleza vitu vya kuhusu kitu ambacho huna mawasiliano nacho wala njia yeyote ya kuweza kujua kuwepo kwa hicho kitu?

Vp ikiwa huyo mungu alikuwepo ila sasa hayupo tena, wewe utajuaje hali ya kuwa mwenyewe hasemi haonekani wala hana mawasiliano yeyote?
 
Alikuwaje Mfano wa Binadamu wakati alikuwa na Sifa zote za Binadamu. Mbuzi atafananishwa na Mbuzi Mwenzake na Binadamu atafananishwa na Binadamu mwenzake

1. Alikuwa anamwili
2. Alikuwa anatembea
3. Alikuwa anaongea
4. Alikuwa Ana Hasira
5. Alipigwa Na Kutoa Damu
6. Alikuwa anachoka na Kupumzika
7. Alikuwa anapenda
8. Alipumua
9. Alienda Chooni

Wewe utasemaje alikuwa na Mfano ndugu. Hebu Shirikisha Ubongo wako Vizuri
Haya uliyoandika una uhakika nayo yote? Well Yesu alikuwa mwanadamu na alikuwa Mungu pia. Kuhusu kutolewa kufia wanadamu ni sheria za rohoni. Lazima ujue dunia tunayoishi ni picha ya dunia isiyoonekana ya rohoni. Ndio maana hata shetani alipoasi Mungu hakumuua alimuacha kwasababu its a spiritual world guided by laws. Sadaka ni issue nyeti sana kwenye ulimwengu zote, hii yetu ya mwili na ya roho. Hasa sadaka ya damu. Ndio maana kuna watu wanatoa sadaka wanadamu wenzao ili kufanikiwa. Sasa wewe unashangaaje Mungu kumtoa mwanae sadaka?
 
Sasa kama hujawahi kumuona wala kumsikia ina maana hayo unayoyajua kuhusu huyo Mungu ni vitu ulivyojitungia tu, unaanzaje kueleza vitu vya kuhusu kitu ambacho huna mawasiliano nacho wala njia yeyote ya kuweza kujua kuwepo kwa hicho kitu?

Tofauti mambo Mawili. Kumsikia Yeye mwenyewe na Kusia Masimulizi kutoka Kwa wazee wako

Vp ikiwa huyo mungu alikuwepo ila sasa hayupo tena, wewe utajuaje hali ya kuwa mwenyewe hasemi haonekani wala hana mawasiliano yeyote?
Mungu keshamaliza Alichofanya Amekuwekea Akili. Siyo lazima Mpaka Aongee Yeye hana Hizo sifa Ulizonazo wewe.

Yeye yupo Alipo na Wewe upo Duniani kakuweka
 
Haya uliyoandika una uhakika nayo yote? Well Yesu alikuwa mwanadamu na alikuwa Mungu pia.
Nina Uhakika maana Ndio sifa za Mwanadamu hizo

Mungu hawezi kuwa Mwanadamu na Mwanadamu Hawezi Kuwa Mungu. Chagua Moja Uwe siyo Uwe Vyote. Yesu Alimlilia Mungu maana Yeye Hakuwa Mungu. Yesu alikuwa Anaenda kutafuta Msaada Sehemu Yakimpata Magumu maana Yake alikuwa anaenda Kuomba Mungu na Watu wengine kama Kina Musa Na Elia Maana Ndio walikuwa Mizimu wa Kipindi hicho

Kuhusu kutolewa kufia wanadamu ni sheria za rohoni. Lazima ujue dunia tunayoishi ni picha ya dunia isiyoonekana ya rohoni. Ndio maana hata shetani alipoasi Mungu hakumuua alimuacha kwasababu its a spiritual world guided by laws.
Sisi Hatupo huko Rohoni ndugu yangu Tupo hapa Duniani tunaongea Lugha ya Kiswahili inayoeleweka. Najua hata Wewe unayoyaongea Huyajui manaa Haupo huko. Sasa Ili nikuelewe inabidi Uniambie Mambo yaliyopo hapa. Ukisema Kwa Mafumbo huna Haja ya Kuniambia Kaa nayo Mwenyewe maana lengo ni mimi Nielewe. Siyo unifumbe fumbe Mambo

Kwahiyo Nipe sababu tu Kwanini Yesu alikuja Kukufia Msalabani Wewe Binadamu ulifanya Nini Mpaka yeye Akafia Msalabani?

Sadaka ni issue nyeti sana kwenye ulimwengu zote, hii yetu ya mwili na ya roho. Hasa sadaka ya damu. Ndio maana kuna watu wanatoa sadaka wanadamu wenzao ili kufanikiwa. Sasa wewe unashangaaje Mungu kumtoa mwanae sadaka?

Sawa hapa Tunaenda Pamoja kama Unajua Kuna Binadamu walitoa Sadaka Ili watajirike maana Sadaka za Damu hata Wachawi wanatoa.. Hata Majini wanatoa sadaka za Damu kwa Manufaa yao Wenyewe

Sasa Je Mungu Alimtoa Yesu kwa Ajili yako wewe ili Impe manufaa gani!? Na wewe ulifanya Nini Mpaka ukamfanya Mungu amtoe mwanae?
 
Ungefuatilia niliye mjibu ungeelewa , yeye alidai uislamu watu wanaongezeka , nikamkanya asipingane na Muhammad kasem
wazi
Uislam ulianza kama Strange (Ajabu,kituko) na Utarudi kuwa Strange
Ulianza kama dini ndogo na Utarudi kuwa dini ndogo
Bado unaendelea kupotosha sababu maana iko pale pale, kwamba mtume anamaanisha Uislamu ulianza ukiwa mgeni na kweli ulikuwa mgeni na utaondoka ukiwa mgeni hii inamaanisha siku za mwisho, hii haimaanishi Waislamu hawaongezeki, ni kweli wanaongezeka kila kukicha , lakini katika hao wapo wanao kufa na mfano wake. Katika dalili za Kiyama ni kufa kwa wingi waja wema yaani Wanachuoni na watakao fika karibu na siku ya Kiyama wengi watakuwa waovu na hawana imani.

Kwahiyo huyo uliye mjibu yuko sahihi.
 
Point yangu ni kwamba wewe unaleta ubishani huo wa kuku na yai.
Topic hapo Juu ni Kuhusu Mungu Kukuogopa Wewe kiasi kwamba Hawezi kukuangamiza kama Alivyowaangamiza Sodoma na Gomora na Kipindi cha Nuhu. Ila Sasa Hivi Akakuletea Mwanae Umchape..Umuue..Umvue Nguo.. Umtundike msalabani. Yeye anakuangalia Tu

Wakati kipindi cha Nuhu watu kuzini, kuiba, na Kuuana Aliwafyekelea Mbali ila Wewe akaona Akuache Ila Amlete Mwanae umuue
 
Tofauti mambo Mawili. Kumsikia Yeye mwenyewe na Kusia Masimulizi kutoka Kwa wazee wako

Mungu keshamaliza Alichofanya Amekuwekea Akili. Siyo lazima Mpaka Aongee Yeye hana Hizo sifa Ulizonazo wewe.

Yeye yupo Alipo na Wewe upo Duniani kakuweka
Masimulizi ya wazee wao wameyapata wapi au wao ndio waliyomuunda huyo mungu ndio maana wanajua kuwa ni bubu na haonekani wamemficha huko wanakopajua wao?

Yeye yupo huko alipo wapi na wakati huna mawasiliano nae utajuaje kuwa kweli bado yupo? vitu vyengine haviingii akilini. Unasema kaniweka duniani vp wakati nimezaliwa na wazazi wangu hapa duniani sasa wewe lini uliniona nawekwa hapa duniani na mungu wako umjue wewe?

Mkuu huyo mungu wako asiyeongea hata bado sijamuelewa kabisa.
 
Topic hapo Juu ni Kuhusu Mungu Kukuogopa Wewe kiasi kwamba Hawezi kukuangamiza kama Alivyowaangamiza Sodoma na Gomora na Kipindi cha Nuhu. Ila Sasa Hivi Akakuletea Mwanae Umchape..Umuue..Umvue Nguo.. Umtundike msalabani. Yeye anakuangalia Tu

Wakati kipindi cha Nuhu watu kuzini, kuiba, na Kuuana Aliwafyekelea Mbali ila Wewe akaona Akuache Ila Amlete Mwanae umuue
Nazungumzia kuhusu kwamba binaadamu hawezi kupatikana(kuzaliwa) bila mbegu za kike na kiume.
 
Masimulizi ya wazee wao wameyapata wapi au wao ndio waliyomuunda huyo mungu ndio maana wanajua kuwa ni bubu na haonekani wamemficha huko wanakopajua wao?

Ungejiuliza Wewe kwanza hilo Swali Ndugu yangu maana Wewe upo kwenye hayo Hayo mapokeo ya Wazee wa Israeli na Mababu wa Huko

Kwa Upande wangu Ni Masimulizi ya Wazee wetu Na Binadamu wa Kwanza Na Si kwamba Aliongea na Mungu bali Muujiza Wake Mungu

Yeye yupo huko alipo wapi na wakati huna mawasiliano nae utajuaje kuwa kweli bado yupo? vitu vyengine haviingii akilini. Unasema kaniweka duniani vp wakati nimezaliwa na wazazi wangu hapa duniani sasa wewe lini uliniona nawekwa hapa duniani na mungu wako umjue wewe?

Mkuu huyo mungu wako asiyeongea hata bado sijamuelewa kabisa.

Mungu yupo alipo na Hakai na Viumbe vyake. Muujiza Wake ndio upo Na Unatenda Uumbaji Mpka Dakika Hii tunayoongea. Unaumba Viumbe kila Siku na Haujawahi kuchoka.

Wewe unamtegemea Mungu Ila Kumtii ni Jukumu lako mwenyewe hakulazimishi. Unamtegemea Yeye ambaye Humuoni Maana Ukilima Unapata Mazao ukienda Hapo Nje utachuma Mchicha Ambao hujui umetoka wapi na Utakula ukienda sehemu utachuma Embe Utakula Ambalo hujui Limefikaje hapo. Utakuta uyoga umejiotea Utachuma na Utakula. Utaenda Kwenye Vyanzo vya Maji utakunywa Maji yake bila Kujua Yametokea Wapi. HAPO unakuwa umemtegemea Mungu. Manaa hivyo vyote aliviumba na akakuwekea Wewe kiumbe hata Kma Ni muovu utavipata

Sasa Ukiniuliza Mungu nimejuaje kwamba Yupo au Hayupo wewe ndio ujiulize Kwanini Ninaweza Kula Bila kujua Chakula hiki kimefikaje Hapa ninaweza Kunywa Maji yaliyopo bila Shida
 
Nazungumzia kuhusu kwamba binaadamu hawezi kupatikana(kuzaliwa) bila mbegu za kike na kiume.
Upo sahihi kwamba Binadamu wa Sasa Hawezi patikana bila hivyo (mbegu ya Kike na Kiume). ila Binadamu wa kwanza Alipatikana Bila Hivyo maana Aliumbwa. Viumbe vyote vya Kwanza Viumbwa na Vilivyofuata Vilizaliana kwa Mifumo yao ilivyowekewa na Mungu

Binadamu wa Kwanza aliumbwa na Kuwekewa Mifumo ya Uzazi na Mifumo hiyo ndio inayoweza Kuzaa na Mungu aliweka Hivyo Ili watu waongezeke

Ukiwa na Mawazo kwamba Lazima Alizaliwa Maana Yake hakuna atakayepata Jibu la Mzazi wake ni nani. Maana Yake kama Ww unaamini Adam na Hawa Hata Wao walikuwa na Wazazi na Hao wazazi walikuwa na Wazazi na Hao wazazi walikuwa na Wazazi
 
Bado unaendelea kupotosha sababu maana iko pale pale, kwamba mtume anamaanisha Uislamu ulianza ukiwa mgeni na kweli ulikuwa mgeni na utaondoka ukiwa mgeni hii inamaanisha siku za mwisho, hii haimaanishi Waislamu hawaongezeki, ni kweli wanaongezeka kila kukicha , lakini katika hao wapo wanao kufa na mfano wake. Katika dalili za Kiyama ni kufa kwa wingi waja wema yaani Wanachuoni na watakao fika karibu na siku ya Kiyama wengi watakuwa waovu na hawana imani.

Kwahiyo huyo uliye mjibu yuko sahihi.
Nimeshawakanya mnapo debate msilete takiya , andiko liko wazi mbele ya macho yako na unapinga kwa kuleta maelezo yako ambayo Muhammad hajasema,
Unapo sema uislamu unaongezeka ni wazi unakri mbele za watu Muhammad katoa unabii wa uongo, Unakiri alafu tukimuita nabii wa uongo unarusha mateke

He also reported Muhammad saying, “Islam began as a small religion and will return to the state in which it began. Then blessed will be the few Mishkat al-Masabih 159

Muhammad akasema Uislamu ilianza kama dini ndogo na utarudi kwenye hali yake ya kuwa dini ndogo.
 
Nimeshawakanya mnapo debate msilete takiya , andiko liko wazi mbele ya macho yako na unapinga kwa kuleta maelezo yako ambayo Muhammad hajasema,
Unapo sema uislamu unaongezeka ni wazi unakri mbele za watu Muhammad katoa unabii wa uongo, Unakiri alafu tukimuita nabii wa uongo unarusha mateke
Hakuna taqiyyah hapo, sasa nikuulize ni kwamba Watu hawaingii katika Uislamu ?

Allah aliye juu anasema :

1. Itakapo kuja nusura ya Mwenyezi Mungu na ushindi,

2. Na ukaona watu wanaingia katika Dini ya Mwenyezi Mungu kwa makundi,

3. Zitakase sifa za Mola wako Mlezi, na umwombe msamaha; hakika Yeye ndiye anaye pokea toba. (an-Nasr : 1-3)

Sasa usiwe mjinga na kuandika maana unazotaka wewe.
 
Back
Top Bottom