SIERA
JF-Expert Member
- Apr 11, 2011
- 2,789
- 3,413
Kaka inabidi umjue Yesu vizuri kwa kumsoma katika kitabu cha biblia. Wewe unamjua Yesu baada ya kuzaliwa na mariam lakini Yesu alikuwepo kabla ya mariam. Yeye ndiye MWANZO. Ameshiriki uumbaji wa Adam na hawa.
Mwanzo : 1 : 26 - Mungu akasema, Na tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama, na nchi yote pia, na kila chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi.
Kwenye hilo andiko Mungu anaposema na TUMFANYE mtu, alikuwa na nani?
Hapo unaposema kwenye andiko Mungu alisema TUMFANYE mtu Ni Mungu Yesu au Mungu yupi hapo anaongea? Na kusema kumfanya mtu kwa mfano wetu si sisi wote wanadamu au so sisi wote ni mfano wa Mungu ?! Mungu Yesu au Mungu yupi