Hakuna kisichoeleweka hapo ni wewe tuu hutaki kuelewa
Unavyojivuruga mwenyewe kwa kushindwa kusoma maandiko na kuyaelewa badala ya kubeba mistari michache na kukimbia nayo ndivyo unavyozidi kuvurugika
Aliyezaliwa na Mariam ni Kristo ambaye malaika alitumwa amwambie akishazaliwa amwite jina lake Yesu, Sio Yusufu wala Mariam walimpa hilo jina
Mathayo 2: 3-4
"Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, KRISTO azaliwa wapi?"
Luka 1: 26-27; 30-33
Malaika Gabrieli alitumwa na Mungu kwenda mpaka mji wa Galilaya, jina lake Nazareti,
kwa mwanamwali bikira aliyekuwa ameposwa na mtu, jina lake Yusufu, wa mbari ya Daudi; na jina lake bikira huyo ni Mariamu.
Malaika akamwambia, Usiogope, Mariamu, kwa maana umepata neema kwa Mungu.
Tazama, utachukua mimba na kuzaa mtoto mwanamume; na jina lake utamwita Yesu.
Huyo atakuwa mkuu, ataitwa Mwana wa Aliye juu, na Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake.
Ataimiliki nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake utakuwa hauna mwisho.
Ijue maana ya jina Imanueli. Baada ya jina hilo kutajwa kwenye Isaya 7:14 nenda kasome Isaya 9:6. Usisome biblia vipandevipande ukatoa hitimisho, jitahidi kusoma uelewe. Ila kama imani yako sio kwa biblia basi nyamaza tuu sababu utaongea hata yasiyokuwako
Isaya 7:14
"Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara. Tazama, bikira atachukua mimba, atazaa mtoto mwanamume, naye atamwita jina lake Imanueli."
Isaya 9: 6
"Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani."