Mungu anaweza kuua watu wengi ili tu amtetee mtu wake

Mungu anaweza kuua watu wengi ili tu amtetee mtu wake

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!

Mbele za Mungu sisi wanadamu ni kama majani na upepo tu.

Yes ametuumba na anatulinda ila kuna wakati anatutazama kwa namna nyingine. Yaani anatusort kulingana na agano lake na mtu husika, au anatusort kulingana na maisha na mienendo yetu.
Kama humchi Mungu , Mungu anaweza kukutumia wewe ili kufanikisha jambo la mtu mwingine huku wewe akikuacha umeumia, kuteseka au hata kufa.

Siku moja nilishikwa na polisi Songea stand asubuhi na mapema kwa kosa nisilolifahamu, nilihisi ni uzurujaji.

Ndo nilikuwa nimefika Songea kwa mara ya kwanza kama mtafutaji huku nikiwa sina hata sh. Mia, pesa yote iliisha , ni stori ya kutia hudhuni na baadaye ilileta furaha, nililala nje siku 5 baadaye nikapata mpenyo nikaishi vizuri.

Ndani ya selo tulikuwa kama 15 hivi.
Sikuwa na simu, kitabu changu chenye namba za simu kiliibiwa pamoja na vitu vichache nikiwa safarini.
Sikuwa na ticket maana niliingia usiku na Lori.
Sikuwa na ndugu Songea

Sikuwa na namba ya simu kichwani labda niwajuze ndugu zangu nyumbani.
Pasi na shaka nilikuwa nakwenda kufungwa miezi 6 kwa sheria ndogo za manispaa chap.
Sasa huku nataka nijitetee roho wa Mungu akanizuia nisiongee chochote.

Mara Nikasikia sauti kutoka desk la nje ambapo mkuu wa kituo mama mmoja mwenye cheo cha MRAKIBU kama sijakosea akiongea na radio call . Alikuwa akijuzwa kuwa basi la super Feo limepata ajali nje kidogo ya manispaa ya Songea na watu kadhaa wamekufa papo hapo.

Akaamuru dereva aje haraka atuchukue tupelekwe central police station Songea ili Askari wa pale wakasaidie huko kwenye ajali .

Ikaja gari haraka tukaamuliwa tutoke nje kwa mstari kisha tupande karandinga haraka.
Mimi nikawa wa mwisho katika mstari ule wa kuelekea nje kupanda karandinga.
Wakapanda wote about 10 na ushehe hivi .

Imefika zamu yangu kupanda nikasimama tu karibu na gari huku nimekaa kimya.
Wakapanda maaskari kwenye gari kisha ikawashwa ikaondoka na watuhumiwa huku Mimi wameniacha chini. Askari wengine walibaki pale kituoni kuendelea na shughuli zingine.

Kwa kweli sikujua nini kiliendelea.

Nilichogundua ni kuwa Mungu humpa thamani kubwa sana mtu wake mwenye agano naye, yuko tayari aue wengi ili akutetee.

Kwa tukio Lile, niliuona utukufu wa Mungu.

Nikasepa zangu.
 
Kama hii sio chai mkuu basi siku hiyo ilikuwa ni bahati yako tu kukosa kuingia jela na walio sio kweli kwamba Mungu aliua watu kukuokoa wewe.
 
Ndugu ule ulikuwa mkono wa Mungu.
Polisi akushike then akusahau tena walikuwa zaidi ya 5 .
Kama hii sio chai mkuu basi siku hiyo ilikuwa ni bahati yako tu kukosa kuingia jela na walio sio kweli kwamba Mungu aliua watu kukuokoa wewe.
 
Dah
Pole mkuu Kila maswahibu yanayotukuta yana maana yake
 
Sioni kama hayo matukio mawili yametokea kwa muunganiko zaidi naona ni ule uharaka na ukosefu wa umakini wa jeshi la polisi ukapelekea mhalifu akaja kupost jamiiforums
 
Kwanini Mungu wako asizuie tukio la kukamatwa kwako kabisa?

Tayari una amini ana nguvu, hana haja ya ku prove

Kwanini aue watu wasio na hatia kwa ajiri yako mzururaji, wakati alikua na uwezo wa kuzuia usikamatwe in the first place?

Kama alitaka uone, kwanini hio part ya pili isitokee bila ajari?

Ndio hivi anavyoongoza vitu siku zote?
 
Sioni kama hayo matukio mawili yametokea kwa muunganiko zaidi naona ni ule uharaka na ukosefu wa umakini wa jeshi la polisi ukapelekea mhalifu akaja kupost jamiiforums
Mkuu usirahishishe kufikiri.

Rai ya mtoa mada ni kuwa kila mstari tuliopo kimaisha tumefikishwa na nguvu fulani na si kwa uwezo wetu.

Je na stori za namna nilivyompata ma'watoto wangu, chanzo kikiwa ni baada ya kumburuza raia mpita njia kwa ajali ya pikipiki kwa uzembe wake wa kuingia barabarani kichwa kichwa kisha kupelekana Polisi.

Na katika mchakato wa kutibishana tukajikuta tunapendana na majeruhi wangu na kupelekea kuoana, waweza kusemaje kwa ishu yenye ukakasi kama hiyo?

Hakuna nguvu ya Mungu kweli hapo?
 
Back
Top Bottom