Habari waugwana
Rejea kichwa cha mzizi;
Inanifikirisha kidogo na simpingi Mungu bali nahitaji msaada zaidi kwenye hili, Mungu anakazia katika biblia HESABU 14:18 BHN
View attachment 2503098
Tena kwenye KUTOKA 20:5 BHN
View attachment 2503099
Atawaadhibu watoto na wajukuu hadi kizazi cha tatu na cha nne kwa dhambi za wazazi wao
Hizi hadhabu kwa makosa ya wazazi wetu ni hadhabu gani? Na kwa makosa yapi? Hasa ya wazazi wetu!!!
Mtoto kuzaliwa tu na ulemavu na kupata tabu palee anapozaliwa mpaka kufa kwake- inaogopesha na kutia huruma
Kufa kifo kibaya kama kusagwa sagwa kwa kugongwa na gari kubwaa na kutoka kama chapati ilee hali ya mtu kutokukutambua wewe ni nan?
Kuwa na maisha magumu pindi unazaliwa mpaka kufa kwako yaani wewe chakula chako cha shida una pa kulala wala cha kuvaa mpaka unaiaga dunia!!
Kuzaliwa una jinsia mbili ya kike na yakiume na pengine zote zinafanya kazi au mojawapo ilimradi tu ufedheheke
Nb; nilitaka nijue kutoka kwenu wakuu, dhambi ipi hiyo Mungu anaichukia mpaka akaamisha laana kwa watoto mpaka wajukuu yaani mpaka kizazi cha tatu mpaka cha nne!!
Sina haja ya kumpangia Mungu!! Kwann? Asingewapa laana hao hao waliofanya hizo dhambi yaani wazazi mpaka kuamishia laana kwa watoto na wajukuu nn? Kilimkwaza Mungu
Eeee Mungu usituangamize!!!