Mungu atawaadhibu kwa dhambi za wazazi wenu, hata kizazi cha tatu mpaka cha nne

Mungu atawaadhibu kwa dhambi za wazazi wenu, hata kizazi cha tatu mpaka cha nne

Habari waugwana

Rejea kichwa cha mzizi;
Inanifikirisha kidogo na simpingi Mungu bali nahitaji msaada zaidi kwenye hili, Mungu anakazia katika biblia HESABU 14:18 BHN
View attachment 2503098
Tena kwenye KUTOKA 20:5 BHN
View attachment 2503099

Atawaadhibu watoto na wajukuu hadi kizazi cha tatu na cha nne kwa dhambi za wazazi wao

Hizi hadhabu kwa makosa ya wazazi wetu ni hadhabu gani? Na kwa makosa yapi? Hasa ya wazazi wetu!!!

Mtoto kuzaliwa tu na ulemavu na kupata tabu palee anapozaliwa mpaka kufa kwake- inaogopesha na kutia huruma

Kufa kifo kibaya kama kusagwa sagwa kwa kugongwa na gari kubwaa na kutoka kama chapati ilee hali ya mtu kutokukutambua wewe ni nan?

Kuwa na maisha magumu pindi unazaliwa mpaka kufa kwako yaani wewe chakula chako cha shida una pa kulala wala cha kuvaa mpaka unaiaga dunia!!

Kuzaliwa una jinsia mbili ya kike na yakiume na pengine zote zinafanya kazi au mojawapo ilimradi tu ufedheheke

Nb; nilitaka nijue kutoka kwenu wakuu, dhambi ipi hiyo Mungu anaichukia mpaka akaamisha laana kwa watoto mpaka wajukuu yaani mpaka kizazi cha tatu mpaka cha nne!!

Sina haja ya kumpangia Mungu!! Kwann? Asingewapa laana hao hao waliofanya hizo dhambi yaani wazazi mpaka kuamishia laana kwa watoto na wajukuu nn? Kilimkwaza Mungu

Eeee Mungu usituangamize!!!
if God is all good (all benevolent) then God has the desire to end suffering, and if God is all-powerful (omnipotent) then God has the ability to end suffering. Therefore if God does not end suffering, then God is either not all good, or is not all-powerful, and is therefore not God”.
 
MTU ni yuleyule Mkuu.
Wakati mzazi wako anafanya dhambi wewe ulikuwa katika mwili wake. Wewe ni yeye, version yake.

Hata wewe ukifanya kosa hapo, ndani yako wapo Watoto wako ambao haujawazaa, lazima wawajibishwe [emoji3]

Hamna hizi hadithi zisahaulike mzee
 
Kutubu hakuondoi adhabu Mkuu[emoji23][emoji23]

Kwa hivyo laana ipo pale pale duuh ya kizazi chatatu mpaka channe! Watoto mpaka wajukuu

Makosa hasa hayo ambayo yapo hapo ambayo yanafanywa na wazazi na kuja kupelekea laana kwa watoto ni yapi? Haswa
 
Sasa mkuu hao wana na wajukuu wana kosa gani?

Sio kwamba ni ‘fair’ kama alitefanya ndio afanyiwe?

Sio fair Kwa kweli mkuu, yaani mtu akikuona unapata tabu ya magonjwa na tabu zingine ajisemee mtaaani huko unamuona huyo wazazi wake walifanya kitu fulani hiyo ni laana kutoka Kwa Mungu Kwa sababu ya makosa ya wazazi wake... hata haiji yaani
 
Mungu wetu sisi alitaka yale maovu unayowafanyia watu wengine ukiona furaha na kujigamba yawapate na wanao na wajukuu zako kama unaona ni mazuri na wao wayavune.

Nimeshasikia kwa wauza madawa ya kulevya kwamba ukiwa unauza unga si unaharibu kizazi yaani watoto wa watu unawauzia Kwa hivyo na wewe kwenye uzao wako lazima ikukute hiyo yaani kama sio mwanao ni mjukuu lazima imkute nae apate tabu kama unavyowatesa wengine.. sasa nilikuwa najiuliza Kwa nn? Isikukute wewe mwenyewe ili uumie zaid
 
Hivi vitabu vya dini za kutungwa na watu jamani, shida kweli kweli.....Hivi Yesu si alikufa msalabani kufuta dhambi zetu, sasa kwanini bado tunazaliwa tuna dhambi ikiwa Yesu alishajitolea kutufutia? Waafrika tuamke jamani, ujinga mwingine tunajitakia sie wenyewe. Kumbukeni tuliishi miaka kibao bila hizi dini kuja hapa duniani na tukaishi vizui tu, tukapata laana baada ya kuletewa hizi dini (Ukristu na Uislam), hizi dini hazina mantiki yeyote kwetu sie waafrika, tunachezewa tu akili.

Waafrica tuamke
 
Pole kwa ndugu zetu wakristo.

Waislam hatuamini kabisa kwenye msingi wa dhambi ya kurithi, tunaamini kila mtu atabeba msalaba wake, kama unazini ni wewe mzinifu ndiye utakaeadhibiwa tena kwa dhambi hiyo hiyo ya kuzini, kama umeua ni wewe muuaji utahukumiwa kwa dhambi hiyohiyo ya uuaji.

Haiingii akilini kabisa kosa afanye babu adhabu aje aipate kitukuu ambae hata hamjui huyo babu mdhambi anafananaje. Huu ni uonevu wa hali ya juu sana.

Nzuri kwa waislam kwa kweli, haiwezekani kwa kosa la mwengine aazibiwe mwengine

Hata serikali leo ukifanya kosa mtoto hakamatwi mama yaani atatafutwa mtoto popote alipo atumikie kifungo
 
Hiyo Kwa Sasa hivi haipo kulingana na maandiko,mtoto hatakufa Kwa dhambi za baba yake,ukifanya uovu laana itakupata wewe,Haina nafasi ya kumpata mtoto kama ataamua kumcha Mungu
 
Hiyo Kwa Sasa hivi haipo kulingana na maandiko,mtoto hatakufa Kwa dhambi za baba yake,ukifanya uovu laana itakupata wewe,Haina nafasi ya kumpata mtoto kama ataamua kumcha Mungu

Kama ni kweli ni vizur tatzo maandiko bado yapo
 
Hawa wanaofanya maovu dhidi ya wenzao ni watu wenye nguvu hasa za kimamlaka na fedha. Na huwa wanadumu muda mrefu. Sasa Mungu hawezi kusubiri hadi wakati wa Kyama. Ikiwa hivyo watu watakuwa hawajifunzi. Ndio maana anataka awaadhibu hapa hapa. Na dhambi hiyo igawanywe kwenye uzao wako kama unaona ni nzuri basi waivune.
Sijui kuhusu wewe ila kiuhalisia ‘that’s not fair’
Haiwezekani aue baba yako adhabu upewe wewe.
 
Inafikirisha sana, kumbe kuna mahali hata watu wakisaidiwa haina maana kwa sababu ile laana inafanya kazi bado. Mungu atusaidie kugundua laana kwenye familia ili tuweze kuomba toba maana kwa kweli kuna vizazi na familia zinapitia mazito kiasi akili ya kibinaadam inafikia ukomo wake.

Kweli kabsa unaweza kumsaidia mtu kumbe laana inatoka kwa Mungu moja kwa moja unakuwa Kama unapambana na Mungu sasa akichukia anaweza akakupiga laana na wewe
 
Sio fair Kwa kweli mkuu, yaani mtu akikuona unapata tabu ya magonjwa na tabu zingine ajisemee mtaaani huko unamuona huyo wazazi wake walifanya kitu fulani hiyo ni laana kutoka Kwa Mungu Kwa sababu ya makosa ya wazazi wake... hata haiji yaani
Kabisa mkuu, utetezi wa ndugu yangu Rasterman hauingii akilini.
 
Mungu humhukumu kila mtu kadiri ya matendo yake
1Neno la Mwenyezi-Mungu lilinijia: 2 “Kwa nini mnarudiarudia methali hii katika nchi ya Israeli:
‘Akina baba wamekula zabibu mbichi,
lakini meno ya watoto wao yakatiwa ganzi!’
3Lakini, kama niishivyo mimi Bwana Mwenyezi-Mungu, nasema kwamba methali hii haitatumika tena katika Israeli. 4Jueni kwamba uhai wote ule ni wangu, uhai wa mzazi na uhai wa mtoto. Yeyote anayetenda dhambi, ndiye atakayekufa.
5“Kama mtu ni mwadilifu, anafuata yaliyo haki na sawa, 6kama hashiriki tambiko za sanamu za miungu mlimani wala kuzitegemea sanamu za miungu ya Waisraeli, kama hatembei na mke wa jirani yake wala kulala na mwanamke wakati wa siku zake, 7kama hamdhulumu mtu yeyote, bali hurudisha rehani, kama hanyanganyi watu mali zao, bali huwapa chakula wenye
 
Ikiwa hawatoziacha njia zao mbaya. Ukizisoma hizo aya(aya na sio sentens fupi fupi) utagundua kuna kichagizo kiashiria cha hiyo adhabu itaendelea kwao hao waendeleao kuzitenda dhambi zilezile.

Mfano 1. Mababu wakaendekeza uzinzi, matokeo yake ugonjwa wa zinaa ukaingia katika jamii hiyo. Madhara ya jamii yao kusumbuliwa na magonjwa ya zinaa yataendelea vizazi vyote endapo vitauendeleza huo uzinzi. Tu.
Mfano 2. Wazazi wakawa watu wema/mafisadi basi watoto wana uwezekano mkubwa wa kurithi tabia husika na kuyapata matokeo husika.

Ndio maana unaona maneno kama 'kizazi cha wanichukiao'. Maana ya wazi kabisa kwamba hicho kijamii ni cha wenye chuki naye. Lakini katika hali ambapo hao watu watabadili mtizamo wao, na ufikiri wao (tafsiri halisi ya kutubu); papo kwa hapo wanakoma kuvaa uhusika wa kizazi cha wanichukiao. Wanakuwa kizazi cha wanipendao na wanapata heri zote

Remember usipende kuchukulia kama Mungu ndo anaadhibu, mambo meeeengi ni kiotomati. We make shit happen. Sisi tukishirikiana na kani zote Mungu included

Mstari umeeleza wazi kuwa yeye Mungu ndio ataazibu yaani atatoa laana yeye mwenyewe
 
Hawa wanaofanya maovu dhidi ya wenzao ni watu wenye nguvu hasa za kimamlaka na fedha. Na huwa wanadumu muda mrefu. Sasa Mungu hawezi kusubiri hadi wakati wa Kyama. Ikiwa hivyo watu watakuwa hawajifunzi. Ndio maana anataka awaadhibu hapa hapa. Na dhambi hiyo igawanywe kwenye uzao wako kama unaona ni nzuri basi waivune.
Kwenye hili nimualike ndugu yangu Al Habib MrPhilosopher Kanju

Atueleze kimaadili imekaaje kumtumia mtu ‘as mere means to an end’.
 
"Life span" ya dhambi ni miaka mia 400.Itaendelea kuoperate mpaka kwenye uzao huo mpaka iexpire.

Hatari sanaa, aliyetuandikia haya maandiko ametuathiri pakubwa sana sisi wasomaji
 
Back
Top Bottom