Mungu hana msaada wowote katika maisha yangu

Bado una safari ndefu sana ya kumjua Mungu.. Mungu anatafutwa.. Sijui umefanya jitihada gani katika kumtafuta Mungu..??
 
Logical non sequitur.

Hata nisipoweza kuthibitisha uwepo wangu, hilo halithibitishi Mungu yupo.

Thibitisha Mungu yupo.
Tayari ushathibitisha uwepo wa Mungu, neno "hata nisipothibitisha" tayari ni kukubaliana kutokukubaliana kwa uwepo wa Mungu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Tayari ushathibitisha uwepo wa Mungu, neno "hata nisipothibitisha" tayari ni kukubaliana kutokukubaliana kwa uwepo wa Mungu.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
Hapana, wewe huelewi logical non sequitur fallacy unayoifanya tu.

Na huo ni uthibitisho Mungu hayupo.

Angekuwepo, asingeumba mtu mjinga kama wewe.
 
Kama MUNGU hana msaada wowote kwako,,hivi hiyo pumzi unayovuta unailipia kiasi gani kwa siku?

Yule anayekulaza na kukuamsha kila siku asubuhi unamlipa kiasi gani?

Viungo vyako vya mwili kuendelea kufanya kazi vikiwa salama unalipia kiasi gani?

Kama basi huna shukran kwa muumba wako inapasa kusema kwamba FIRAUNI na wafuasi wake bado wanaishi duniani.
 
Acha porojo...huyo Mungu hayupo ni story tu.
 
Umeandika vizuri..hongera..ingawa kuna sehemu umechapia.
Mungu sio Hamisi (Mwanadamu), upendo wa Mungu ni zaidi kwa mbali kulinganishwa wa upendo wa mzazi kwa mtoto.Je mzazi anaweza mchukia mtoto wake hata kama anamapungufu kama yote, jibu ni hapana.
Hapo umemuongelea Mungu as if ni mwanadamu kuwa anatoa baada ya kupokea, umemuweka Mungu kama kiumbe chenye hisia na UMEMUHUKUMU HUYU NDUGU KUWA SABABU YUKO MBALI NA MUNGU NDO MAANA ANAPITIA MATATIZO. Umekosea sana...nani alikudanganya kuwa watu waliokaribu na Mungu hawapati matatizo, nani huyo - kuna mwanadamu yupi ambaye anamaisha yamenyooka na hana matatizo ???Vipi wewe mwenzetu unamaisha mazuri from all angles kama malaika???
Mungu yuko sawa kwa watu wote, hana upendeleo, Mungu katupa karama kila mtu na kila mtu kwa kupitia karama yake anaweza kujipatia mahitaji yake hapa duniani bila kumuingilia mwenzake.
Tumuombe Mungu atusaidie kuwa wastahimilivu pale tunapopitia changamoto - EMOTIONAL INTELLIGENCE. Hivyo usimtishe et sijui kamkosea Mungu...n.k huo ni uongo..muombe Mungu ampe ustahimilivu kama wewe hapo mpaka unafikiri wenzio wanamatatizo sababu wako sinful. Kwa hiyo ukienda OCEAN Road ukiona watu wanavyoteseka na Cancer - akili yako inakwambia hao ndi wakosefu sio???
 
Faida pekee ya rushwa kwenye jamii ni kuua imani, is one of the symptom enlightment, endelea na ulozi mpaka uijue lugha, inawezekana, welcome to the highest culture
 
Inabidi afanyeje aweze ku experience hizo nguvu za Mungu zilizopo ndani yake.
 
Mungu anafahamu kuna watu akiwapa balaa lake sio dogo, ndiomaana kakunyima.
 
Afya ya akili haipo sawa...kujiona wewe ndio una matatizo kuliko watu wote ni shida ya akili inawezekana kabisa hayo matatizo uliyonayo ni madogo sana kulinganisha na hao wenzako unaosema wana Neema Tele.
Wahi kwa wataaamu wakusaidie.
 
MUNGU sio fikra. God is real. Hatumjifunzi au kumwamini ili kuhakikisha kama kugusa. Kila mtu ana maswali kumhusu. Ila majibu, msaada na Imani kwa Mungu ni halisi. Ni vigumu kugawiana Imani kama keki. Binafsi nimemuona MUNGU kwa Imani na aliyonitendea.
 
Nan anaefanya upumue kama kakupa pumzi kwann useme hana msaada🙂
 
Kunbe mungu wako na yeye ni kiumbe?

Huyo hafai, hata mimi nakuunga mkono.
 

“kwa mtoto.Je mzazi anaweza mchukia mtoto wake hata kama anamapungufu kama yote, jibu ni hapana;
ni hapana. Hapo umemuongelea Mungu as if ni mwanadamu kuwa anatoa baada ya kupokea,

God is so principled, ni wa kanuni:

1. Kwa Neema na Upendo wake alituletea Wokovu bure; lakini unajua kwamba “Lazima umkubali Yesu ndiyo upokee wokovu? Huo ndo utaratibu aliouweka.

2. Mtu anajuwaje Kumuelewa Mungu? Ni kwa kujifunza na kumfaham, ni hatua ya kwenda kujifunza, soma Warumi 12: 1 ( Ina mambo ma 3:

- Mwili unautoa dhabihu kumuelekea Mungu, ni bidii.

- Nia/nafsi inageuzwa ili Kuwa mamlaka ya mwisho.

- Baada ya kutoa Mwili na kugeuzwa nia kumfuata Mungu then ndo unajua MAPENZI ya Mungu…..

Swali: Hizo hatua 3 hapo mimi ndo namsadia?

Upo sahihi, ila uelewa wako umeishia kwenye Upendo wa Mungu tu, elewa Mungu ana upande wa pili!!
 
Kwangu hajafanikiwa kunisaidia chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…